• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, September 18, 2015



Sikuzote waswahili wanasema kimya kingi kina mshindo sasa naamini kweli kwamba kimya kingi kina mshindo pale nilipokutana na wakali hawa "BECKA TITTLE na BUI BUI"na kusikilizishwa ngoma yao"UNATAKA NINI?",ngoma ambayo imefanywa ndani ya studio za MOTTO RECORDS.

Video ya Nyimbo hii imefanywa na kampuni yako mama ya "ALLSTARTZ MEDIA".......

Single na Video vitatambulishwa siku ya tarehe 21/09/2015 katika Media zote na Social Media kwa ujumla.
Mashabiki na wapenzi wa Muziki mzuri tutegemee Radha nzuri kutoka kwa wakali hawa tukitega  Masikio katika Radio Stations mbalimbali na Macho yetu katika TV Stations.....

Thursday, September 17, 2015

Nominees wa mwaka 2015 BET HIP HOP AWARDS ni kama ifuatavyo,huku Drake akiongoza kwa Categories 12,Big Sean 10,Nicki Minaj 9,Kendrick Lamar na  J. Cole 8.
Host wa Awards hizi atakuwa SNOOP DOGG kwa mara ya Tatu mfululizo siku ya Tarehe 9 October huko Boisfeuillet Jones Atlanta Civic Center.

LIST NZIMA HII HAPA!!!
Best Hip Hop Video
Big Sean, featuring Chris Brown and Ty Dolla $Ign - "Play No Games"
Big Sean, featuring Drake and Kanye West - "Blessings"
Fetty Wap - "Trap Queen"
Kendrick Lamar - "Alright"
Nicki Minaj, featuring Beyoncé - "Feeling Myself"
___
Best Collabo, Duo or Group
Big Sean, featuring Drake and Kanye West - "Blessings"
Big Sean, featuring E-40 - "Idfwu"
Fetty Wap, featuring Monty - "My Way"
Nicki Minaj, featuring Beyoncé - "Feeling Myself"
Nicki Minaj, featuring Drake and Lil Wayne - "Truffle Butter"
___
Best Live Performer
Drake
J. Cole
Kanye West
Kendrick Lamar
Nicki Minaj
___
Lyricist of the Year
Big Sean
Drake
J. Cole
Kendrick Lamar
Nicki Minaj
___
Video Director of the Year
Alan Ferguson
Benny Boom
Chris Robinson/Lil Chris
Colin Tilley
Director X
___
DJ of the Year
DJ Drama
DJ Envy
DJ Esco
DJ Khaled
DJ Mustard
___
Producer of the Year
DJ Mustard
J. Cole
Kanye West
Mike Will Made-It
Pharrell Williams
Timbaland
___
MVP of the Year
Big Sean
Drake
Future
J. Cole
Kendrick Lamar
Nicki Minaj
___
Track of The Year
"Alright" - Produced by Pharrell Williams and Sounwave (Kendrick Lamar)
"Blessings" - Produced by Boi-1da and Vinylz (Big Sean, Featuring Drake and Kanye West)
"Commas" - Produced by Dj Spinz and Southside (Future)
"Idfwu" - Produced by Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West and Key Wane (Big Sean, Featuring E-40)
"Trap Queen" - Produced by Tony Fadd (Fetty Wap)
___
Album of the Year
Big Sean - Dark Sky Paradise
Drake - If You're Reading This It's Too Late
J. Cole - 2014 Forest Hills Drive
Kendrick Lamar - To Pimp a Butterfly
Nicki Minaj - The Pinkprint
Wale - The Album About Nothing
___
Who Blew Up Award
Bobby Shmurda
Dej Loaf
Fetty Wap
Rae Sremmurd
Tink
___
Hustler of the Year
Dr. Dre
Drake
J. Cole
Jay Z
Nicki Minaj
___
Made-You-Look Award (Best Hip Hop Style)
A$Ap Rocky
Dej Loaf
Drake
Kanye West
Nicki Minaj
___
Best Hip Hop Online Site
Allhiphop.Com
Complex.Com
Hotnewhiphop.Com
Rapradar.Com
Worldstarhiphop.Com
___
Best Club Banger
Big Sean featuring E-40 - "Idfwu" (Produced by Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West and Key Wane)
Dej Loaf - "Try Me" (Produced by Dds)
Fetty Wap - "Trap Queen" (Produced by Tony Fadd)
Future - "Commas" (Produced by Dj Spinz and Southside)
Rich Homie Quan - "Flex" (Ooh, Ooh, Ooh) (Produced by Dj Spinz and Nitti Beatz)
___
Best Mixtape
Future - 56 Nights
Future - Beast Mode
Future - Monster
Lil Wayne - Sorry 4 the Wait 2
Travis Scott - Days Before Rodeo
___
Sweet 16: Best Featured Verse
Drake - "Blessings" (Big Sean, Featuring Drake and Kanye West)
Drake - "My Way Remix" (Fetty Wap, Featuring Drake)
E-40 - "Idfwu" (Big Sean, Featuring E-40)
Kendrick Lamar - "Classic Man Remix" (Jidenna, Featuring Kendrick Lamar)
Lil Wayne - "Truffle Butter" (Nicki Minaj, Featuring Drake and Lil Wayne)
___
Impact Track
Big Sean, featuring Kanye West and John Legend - "One Man Can Change the World"
Common and John Legend - "Glory" (From the Motion Picture Selma)
J. Cole - "Apparently"
J. Cole - "Be Free"
Kendrick Lamar - "Alright"
___
People's Champ Award
Big Sean featuring Drake and Kanye West - "Blessings"
Fetty Wap - "Trap Queen"
Future - "Commas"
Kendrick Lamar - "I''
Rae Sremmurd - "No Type"
Rich Homie Quan - "Flex (Ooh, Ooh, Ooh)"
Story kuhusu Jay-Z na Beyonce kuachana zimechukua sura nyingine baada ya Beyonce kuonekana mja mzito wa mtoto mwingine,Sura hii imetokea baada ya Jay-Z kugundua kuwa Mzazi mwenzake ni mjamzito,alimpeleka ITALY kwa mapumziko ili waweze kurekebisha Mapenzi yao.

Wednesday, September 16, 2015


Tuesday, September 15, 2015


Monday, September 14, 2015

'Nimepania'Single mpya na ya kwanza kutoka kwa Presenter Mkali wa East Africa Radio na Tv SAMMISAGO ni wimbo wa Mapenzi uliotayarishwa Chini ya SWITCH RECORDS na producer LUFA akimshirikisha mkali wa RnB BEN POL....Enjoy!!!!

Friday, September 11, 2015


Tuesday, September 8, 2015


Monday, September 7, 2015

WAKATI akili yangu ikianza kupata ufahamu, nilikuwa natatizika na kuwaza kitu gani hasa katika mapenzi kinaweza kumfanya mtu atulie ndani ya penzi lake. Niliamini kuwa na fedha ndiyo dawa ya mtu kumtuliza mpenzi wake au kwa mwanamke kuwa mzuri na mwenye sifa zote, ndiyo dawa ya kumfanya mpenzi wako atulie.
Baada ya kukua na kuingia katika dunia ya ufahamu wenye mitihani mingi ya mapenzi, nimegundua kuna utofauti mkubwa katika vitu nilivyoviwaza.

Wakati nakua, nilikutana na matukio ambayo niliona kama ngamia kupita kwenye tundu la sindano, lakini baada ya kupevuka, nilipata majibu ya maswali yaliyonisumbua kipindi kile cha utoto.
Sikuamini mke wa tajiri kufanya mapenzi na muuza mchicha, mwanaume mwenye mke mzuri kutembea na changudoa au msichana wa kazi asiyejua kuvaa wala kuoga.
Baada ya kuingia katika kazi hii ya kukumbushana mambo ya mapenzi, nilipata maswali mawili ya watu wawili tofauti lakini yalikuwa na jibu moja.

Mmoja alilalamika ana mke, anamhudumia kila kitu ikiwemo familia yake lakini alichomlipa ni kutembea na mtu asiye na mbele wala nyuma. Mwingine alilalamika kuhusu mpenzi wake kutembea na mwanamke wa nyumba ya pili ambaye haufikii hata mguu wake kwa uzuri.
Kabla ya kulizungumzia hilo, nirudi kwao kuwaeleza kukosa uamini hakuangalii katembea na tajiri au mwanamke anayekushinda uzuri, kutoka nje ya uhusiano au ndoa ni kosa kwa vile penzi ni la watu walioridhiana au kuoana wakiwemo waliooa wake zaidi ya mmoja. 

Leo nawajibu wote kuwa fedha au uzuri wa mtu havibebi ndoa au uhusiano. Nimekuwa muumini mzuri wa kuwaeleza penzi la kweli lipo vipi, mapenzi ni upendo wa dhati kutoka moyoni, kuwa tayari kujilinda na kujiheshimu bila kujali una fedha au ni mwanamke mzuri.
Mapenzi ni mbegu inayohitaji udongo wenye rutuba ya upendo ili mbegu hiyo imee. Siku zote mwenye mapenzi ya kweli humuangalia mtu, si kitu.

Tajiri na fedha zake asipopendwa huwa katika mateso na kukonda wakati ana kila kitu. Penzi la kweli halinunuliwi kwa gharama yoyote.
Tabia ya asili huwa sawa na moto unaowaka kwenye pamba, ukitoa moshi ujue hakuna kilicho salama. Wapo watu wasiokuwa na mapenzi ya dhati, utakuta mtu anajifanya anakupenda ukiwa naye lakini mkiachana hana habari na wewe, hata kama mnakaa nyumba moja na kulala kitanda kimoja.
Mtu anapoamua kutoka nje ya ndoa wakati ndani ana mke mzuri au mume wa ukweli anayempa kila kitu, kuna mawili:
Mosi:
Huenda mwanamke aliyenaye alimtamani kutokana na sura na umbile lake na hakumpenda kwa dhati. Matokeo yake baada ya kumchoka, mwanamke huonekana hafai na hukaa naye kimazoea. 
Upande wa mwanamke, naye huenda amekwenda kwa mwanaume kutokana na kujua ana fedha lakini anakuwa hana mapenzi naye. Hapo lazima atatafuta penzi la nje ili afurahishe nafsi yake, kwa hiyo watu hawa kutoka nje sishangai.
Pili:
Tabia ya kutoridhika na mpenzi mmoja, watu wa aina hii huwa hawajisikii kula kitu cha aina moja kwa muda mrefu, lazima atatafuta mtu wa kumfanya abadili mboga. 
Vitu hivi vyote huwa vinawachanganya watu, hasa wale wanaoamini kuwa mwanaume anapokuwa na fedha au mwanamke anapokuwa mzuri, ni kila kitu katika mapenzi.
Mapenzi ni bahati, hasa kumpata uliyemkusudia, basi muombe Mungu utakayemchagua naye awe kweli amekukubali, hata ukiwa mbali kila mmoja amlindie mwenzake heshima, kwa kutanguliza uaminifu mbele.

Wednesday, September 2, 2015


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ