• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, April 29, 2016



Wednesday, April 27, 2016


Nyota wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ ambaye hivi karibuni aliuaga ukapera kwa kuamua kufunga pingu za maisha na mzazi mwenzake, Wayda, amedai anatarajia kuachia wimbo mpya ambao amemshirikisha Ali Kiba.

Mr Blue amedai kwamba wimbo huo utajulikana kwa jina la ‘Mboga Saba’

Akizungumza na MTANZANIA, Mr Blue alisema kuwa wimbo huo upo tayari na anatarajia kuuachia wiki ijayo endapo mtayarishaji wake, Man Water atamkabidhi.

“Kiukweli huu wimbo haujawahi kutokea na utakuwa bonge la wimbo kwa kuwa tumekutana wakali wa muziki, ninaamini wimbo huo utakuwa ni historia katika tasnia ya muziki hapa nchini,” alisema Mr Blue.
This song"FREEDOM"Has Been Produced By Daxo Challi (MJ RECORDS) From Tanzania And Written By SUGU 'The Video Was Directed By Hanscana from Wanene Films.
Blue aliachia wimbo huo October 5 mwaka jana na sasa Sugu ambaye ni mbunge wa Mbeya Mjini ameachia video ya wimbo huo akiwa peke yake baada ya kuinyofoa verse ya Blue na Kabayser imemuuma.
“Ndugu zangu nipeni ushauri kwa hili niliona nikae kimya ila limeniuma sana kwa kweli,” ameandika Blue kwenye Instagram.
“SUGU namuheshimu km kaka yangu kimuziki na kiumri pia ..sasa kuna nyimbo nilimshirikisha inaitwa “Freedom” tulifanya pale kwa makochali na hiyo ndo picha ya ushahidi na nyimbo ipo youtube kwa wasioisikia. Sasa kinachonishangaza leo kuona ameitoa verse yangu na kuweka verse zake mbili na kaishoot mpaka video na nyimbo imekuwa yake tena bila kunitaarifu mimi mwenyewe au ridhaa yoyote kutoka kwangu je hii ni haki kweli??? Maana mtu ukiongea unaonekana unatafuta kiki au sijui nn…mi imeniuma kwa kweli jamani je mnanishauri nini ndugu zangu….????,”ameongeza.
Hii ndio single ambayo imeimbwa na BLUE+SUGU

Papa-Wemba
Mtandao wa Kinshasa-makomba.com ametoa shutuma kuwa mwimbaji Papa Wemba aliyefariki wiki iliyopita kwa kuangaka jukwani ghafla hakufariki kwa kifo cha kawaida bali aliwekewa sumu kwenye mic aliyokuwa akiimbia..Mtandao huo umekwenda mbali zaidi na kuweka video ikionyesha tukio zima jinsi alivyobadilishiwa mic na kuwekewa yenye sumu….

Sunday, April 24, 2016

Muimbaji huyo maarufu amefariki akiwa Abidjan, Ivory Coast amefariki baada ya kuanguka ghafla wakati akitumbuiza kwenye tamasha la muziki la Anoumabo (FEMUA). Inadaiwa kuwa alishikwa na kifafa.

Papa Wemba ambaye jina lake ni Jules Shungu Wembadio Pene Kikumba, amefariki akiwa na umri wa miaka 66.

Millen-Magese-Nhlanhla-Diamond-Platnumz-Babalwa
'NdiNdiNdi' is Lady Jaydee’s most anticipated recording to date and is already topping the charts in a myriad of markets. 'NdiNdiNdi' is Lady Jaydee’s 1st official release through her worldwide partnership with her record label and management company ROCKSTAR4000 and Rockstar Publishing. 

Thursday, April 21, 2016

Video mpya ya Kiss Daniel hii hapa,inakwenda kwa jina la Mama.
Enjoy!

Wednesday, April 20, 2016



Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli ambayo imedhamiria kulirejeshea uhai kamili Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya nne, jana imeeleza muda zitakapotua nchini.


Akijibu swali Bungeni, lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Joyce Bitta (Chadema|), kwa niaba ya waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi; Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani alisema kuwa ndege hizo zitangia nchini kwa awamu mbili ndani ya miaka miwili ijayo.


Dk. Kalemani alieleza kuwa ndege mbili za mwanzo zenye uwezo wa kubeba abiria 78 kila moja zitatua nchini mwanzoni mwa mwaka ujao (2017), na nyingine mbili zenye uwezo wa kubeba abiria 120 na 155 zitaingia nchini mwaka 2018.


“Ndege hizo zitaiwezesha ATCL kurejesha safari zake za Johannesburg-Afrika Kusini, Afrika Magharibi, India na Arabuni,” alisema Dk. Kalemani.
Alisema kuwa mbali na ndege hizo, Serikali ina mpango wa kununua ndege nyingine za masafa marefu zitakazokuwa na uwezo wa kwenda katika mabara ya Asia na Ulaya.
Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Azan FC wametupwa nje ya michuano ya hiyo baada ya kuchapwa kwa magoli 3-0 na Esperance ya Tunisia kwenye mchezo wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa Tunis, Tunisia.

Azam walikomaa kipindi cha kwanza na kufanikiwa kwenda mapumziko wakiwa hawajaruhusu goli hata moja licha ya mashambulizi makali ya mara kwa mara kufanywa kwenye goli lao lakini golikipa Aishi Manula alikuwa imara kuondosha hatari zote na kuiweka Azam salama.

Dakika ya 49 kipindi cha pili Esperance walipata bao la kuongoza lililopachikwa kambani na Saad Bguir kisha Jouini akaiandika bao la pili na Ben Yousef akaihakikishia timu yake kusonga mbele baada ya kufunga bao la ushindi dakika tisa kabla ya mchezo kumalizika.

Benchi la ufundi la Azam chini ya Stewart Hall lilifanya mabadiliko kujaribu kubadili matokeo kwa kuwapumzisha Farid Musa, Salum Abubakar ‘Sure Boy’na Wazir Salum huku nafasi zao zikichukuliwa na Hamisi Mcha, Himid Mao na Didier Kavumbagu lakini bado mabadiliko hayo hayakumlipa kocha huyo raia wa England.

Esperance imeitupa Azam nje ya mashindano kwa jumla ya magoli 4-2 baada ya kucheza mechi mbili. Mchezo wa kwanza Azam ikiwa nyumbani ilishinda kwa magoli 2-1 lakini leo imejikuta ikikubali kuchapwa magoli 3-0 ndani ya dakika 32 na kuyaaga mashindano rasmi
Baada ya miaka 10 ya kufanyakazi na muongozaji wa video Justin Campos, Komando Jide au Lady Jaydee amerudi tena kwake kufanyanaye kazi, kutengeneza video ya wimbo wake wa #NdiNdiNdi


Taarifa hiyo ya kufanyakazi na Justin Campos ameitoa Lady Jaydee mwenyewe kwenye ukurasa wake wa Instagram, baada ya kupost video ikimuonyesha Justin Campos akisema ni heshima kwake kufanyakazi na Jaydee ingawa si mara ya kwanza.
“Nilikutana na Justin Campos kwa mara ya kwanza 2006 wakati tunafanya video ya 'Njalo' nilioshirikiana na kundi la Afrika Kusini linalojulikana kama 'Mina Nawe', Justin ndio alikuwa Director wa video hiyo baada ya miaka 10 tumefanyanae kazi tena 2016,” aliandika Jaydee.
Pia Lady Jaydee ameanza kupost picha za video hiyo huku akiandika “#NdiNdiNdi loading Kikomandooooooo #NguvuYaUmma #WananchiWameipokea #NdiNdiNdiMusicVideo”.
A photo posted by Lady JayDee (@jidejaydee) on

Tuesday, April 19, 2016

Tunda
Gari hiyo ilihusisha gari ndogo aina ya Toyota Aurion iliyokuwa ikiendeshwa na Musa ‘Man Katuzo’ Katunzi aliyefariki kwenye ajali hiyo.
Taarifa za awali zilidai kuwa Tundaman alikuwa mmoja wa abiria waliokuwemo kwenye gari hiyo. Lakini sasa imekuja kubainika kuwa, Tundaman hakuwemo kwenye gari hilo, bali alikuwa kwenye gari aina ya Noah.
Tetesi hizo zilikuwa kubwa zaidi kutokana na jinsi gari ilivyoharibika baada ya ajali hiyo huku Tundaman akidaiwa kutopata jeraha lolote ukilinganisha ma majerehi wengine watatu.
Tundaman anasisitiza kuwa alikuwemo kwenye gari hilo kwa kudai kuwa walikuwemo abiria watano. Utata kuhusu kutokuwemo kwa Tundaman kwenye gari hiyo ulianza kusambaa Jumanne hii kwenye mitandao ya kijamii.
Mimi niliiona kupitia HR wa kituo cha redio cha Ebony FM, Luther Akyoo aliyeandika kwenye Facebook: “TUKATAE TAIFA KUJENGWA KWA UONGO UONGO. Tundaman hakuwemo katika ajali hii mbaya, kinachoendelea naweza kuita ni ule ujanja ujanja wa kutafuta “Kiki” kupitia njia ambazo sio sahihi,” aliandika.
“Tundaman alikuwepo katika Noah, na yeye ni mmoja wa watu waliofika katika eneo la ajali hii na kumkuta Dereva na mmiliki wa gari akiwa ameishatutoka. Narudia, TUNDAMAN HAKUWEPO KATIKA GARI HII, watengeneza story yake watengeneze vyema na upya. Sidhani kama ni sahihi kwa upotoshaji huu kuendelea, tusikubali kuwa sehemu ya jamii ya watu kupokea habari zisizokua na uchunguzi wa kina,” alisisitiza.
“Ukweli ni huo, huyu alipata ajali alikuwepo kwenye shoo yake, baadaye aliondoka mapema, Tundaman hata ofisi za radio ebony FM alifika na gari aina ya NOAH, sio hii inayosambazwa mitandaoni. Hii ilipata ajali na mtu mwingine, Tundaman alifika kwenye eneo la TUKIO kama SHUHUDA mwingine,” aliongeza.
Niliamua kufuatilia kwa ukaribu zaidi habari hiyo kwa kuongea na Dj wa Ebony FM aliyekuwa host wa show zao na aliyedai kuwa ni kweli Tundaman hakuwepo kwenye gari iliyopata ajali. Anadai kuwa Tunda alikuwa kwenye Noah pamoja na wasanii wa Khanga Moko, Dj Kman na dereva.
Kujiridhisha nilizungumza na Dj Kman aliyekuwa akizunguka na Tundaman ambaye hata hivyo alisisitiza kuwa Tundaman alikuwemo kwenye gari iliyopata ajali.
Kipindi cha XXL cha Clouds FM nacho kiliamua kufanya uchunguzi wake na awali kiliongea na Tundaman aliyeendelea kusisitiza kuwa alikuwemo kwenye gari hilo.
Kipindi hicho kilizungumza na Kaimu Kamanda Mkuu wa polisi Iringa, John Kauga. Kamanda Kauga amedai kuwa gari iliyopata ajali ilikuwa na abiria wanne ambapo mmoja alifariki. Pia aliwataja majeruhi waliokuwemo kwenye gari hilo na jina la Tundaman halikutajwa.
Kwa maelezo hayo kila mmoja anaweza kujiridhisha kuwa Tundaman hakuwemo kwenye gari hilo jambo linalowashangaza wengi na kuwafanya waulize nini hasa sababu ya Tundaman kusema uongo katika suala kubwa kama hili.
Mimi na wewe hatukuwepo kwenye tukio hili na hatuna mamlaka ya kuhukumu, lakini kwa maelezo hayo yanayozipa ukweli tetesi hizo, Tundaman amenishangaza sana. Kuna mambo mengi mno ya kutafutia umaarufu lakini sio kwa hili.
Inashangaza pale mtu anapokuwa na amani tu kupokea pole pomoni kwa kitu ambacho hakuhusika nacho. Ajali hii imepoteza maisha ya kijana aliyekuwa na mke na familia yake iliyokuwa ikimtegemea – huwezi kuweka mzaha. Si ustaarabu kulaghai katika suala serious kama hili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikata utepe huku viongozi wengine wakiushikilia kuashiria uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipata picha ya kumbukumbu viongozi wengine baada ya uzinduzi rasmi wa Daraja la Kigamboni katika wilaya mpya ya Kigamboni jijini Dar es salaam leo Aprili 19, 2016.

Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. John Magufuli amekataa daraja la Kigamboni lisiitwe ‘Daraja la Magufuli’ na badala yake ameshauri lipewe jina la muasisi wa Taifa hili, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akiongea wakati wa kuzindua daraja hilo leo, Rais Magufuli amesema kuwa awali aliletewa mapendekezo na waziri mwenye dhamana akimtaka aridhie daraja hilo lipewe jina lake, lakini kwakuwa wazo la ujenzi huo lilianza tangu wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, alikataa na kushauri jina la Nyerere litumike .

“Nilikataa lisiitwe kwa jina langu kwa sababu wazo la ujenzi wa daraja hili lilianza mwaka 1979 wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere.

“Wazo hilo halikufanikiwa kutokana na ukosefu wa pesa wakati huo. Mwalimu Nyerere ni kiongozi aliyejenga misingi imara katika taifa letu.
“Alikuwa ni kiongozi asiyebagua mtu kwa misingi ya dini, chama au kabila. Alifanikiwa kutuunganisha watanzania wote bila kujali itikadi zetu.
“Leo hii, daraja hili limekamilika, ni daraja ambalo halitambagua mtu kwa sababu wa CCM watapita hapa, wa Chadema watapita hapa na bahati nzuri mstahiki Meya wa jiji hili ambaye ni Chadema naye yuko hapa na amepita katika daraja hili.
“Ndugu zangu sistahili sifa zozote, najua nimefanikisha ujenzi huu nikiwa waziri wa ujenzi, lakini wakati huo nilikuwa natimiza wajibu wangu kama mtumishi wa umma, hivyo nashauri hili daraja liitwe daraja la Nyerere ili tuweze kumuenzi mwasisi wa taifa hili” alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanalitunza daraja hilo katika kujenga uchumi wa taifa.


TAZAMA HOTUBA YAKE:

Monday, April 18, 2016


Thursday, April 14, 2016



Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ