• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Sunday, May 29, 2016



Saturday, May 28, 2016

Mangwea
Wasanii wa muziki nchini, TID, Izzo B, Mirror, M2 The P pamoja na Billnass Jumapili hii ndani ya Maisha Basement watafanya show maalum kwa ajili ya kumbukumbu ya kifo cha msanii Albert Mangwea aliyefariki dunia Mei 28, 2013 akiwa nchini Afrika Kusini.

Aidha, wasanii mbalimbali kupitia mitandao yao kijamii, wameamua kutoa ya moyoni kuhusu kumbukumbu ya kifo cha Mangwea. Angalia maoni.

M2 The P

Pumzika kwa amani pacha wngu now nipo moro na bi .mkubwa #mama mangweah katika kuazimisha siku yko leo tumemaliza misa salamaa nakumic snaa pacha wngu
Mwana FA
Miaka mitatu leo..pumzika kwa amani Albert RAFIKI yangu…SURNAME YA FREESTYLE..wewe ni mfano halisi wa ‘wazuri hufa mapema’..

Dudu Baya

Albert mangwea.a.k.a mimi. Bongo Fleva imekumis sana.waliokuwa wanabania ngoma zako. Mungu alipotimiza wajibu wake (akakuchua) watu walizipiga sana ngoma zako, walikupamba sana. Uwezo wako ni mkubwa. hata leo tanzania inakukumbuka. Manguruwe nao wanakukumbuka wakiwa na aibu.r.i.p ngwear.

Mirror

Memorial of Ngwear… @maishabasement kesho we Miss you Fo real G.

Billnass

R.I.P Bro Tutakukumbuka Daima….Mpaka 2takapoonana tena….Cowbama

Kala Jeremiah

BONGE LA MSANII. PUMZIKA KWA AMANI BRO TUTAKUKUMBUKA DAIMA.

Friday, May 27, 2016

Video mpya kutoka kwa msanii wako Bilnas "Chafu Pozi"ikiwa tittle ya Single hii...

Chukua dakika zako tatu kuangalia nini hasa katika chafu pozi....

Enjoy!!!
AUDIOVIDEO

Thursday, May 26, 2016

Ikiwa imepita Miaka kumi sasa toka Mbunge na Msanii MR.II a.k.a SUGU kwa mara ya kwanza ataonekana katika Luninga yako kupitia Kipindi cha CLOUDS 360 ya Clouds TV.

Yote haya yalitokea Baada ya Sugu kudai kudhurumiwa Dili la Malaria,ambayo ilikuwa ni project ya SUGU kipindi hicho.

Mengi yatazungumzwa hapo siku ya ijumaa Tarehe 27/05/2016   katika Luninga yako ndani ya Clouds TV.

Allstartz Media ilifuatilia video hii toka siku ilipowekwa mtandaoni mpaka sasa kwa bahati mbaya link ya vipande nilivyotegemea mvione juu ya malalamishi ya Nisher IMEONDOLEWA  , uongozi umeamua kuangalia ubora wa video na creativity hiki ndicho tulichobaini.....
NISHER HANSCANA

Monday, May 23, 2016

Jaribu kuangalia video hizi mbili tofauti zilizofanywa na directors wawili tofauti (NISHER NA HANSCANA) na zikawa uploaded siku moja ingawa mikwaruzo ilianza kitambo bila makubaliano mazuri kati ya G-Nako na director aliyefanya video ya kwanza Nisher.

Maranyingi wasanii wanaposaidiwa toka walipo katika hali ya chini ya audio mpaka video pindi wafanyapo vizuri katika game,huvimba vichwa na kusahau fadhira zote walizofanyiwa pindi walipokuwa hawana kitu mpaka wanacho kwa sasa.Hii haijamtokea Nisher tu kuna mifano mingi ya Producers na Directors waliofanyiwa hivi.Kikubwa kuimarisha terms and conditions katika biashara hizi.

Daima Producers na Directors wengi wenye hekima huwa hawabishani sana na wasanii hawa bali hutoa fact  na kuendelea na mambo yao,sababu "WHAT GOES AROUND COMES AROUND"

Siongei haya kana kwamba ni mimi wa kunukuliwa juu ya malalamiko haya bali ni utafiti uliofanywa na Allstartz Media kutoka katika comments zilizopo katika profile za Msanii huyu na Director Nisher.

Audio:


Video:NISHER ENTERTAINMENT

Video:HANSCANA

Video ya kwanza imefanywa na Nisher na yapili Hanscana.
Maranyingi msanii asiporidhika na kazi ya Director au Producers kabla ya kukabidhiwa hupitiwa terms zilizotumika kufanya video hiyo kisha kuangalia kama kuna ukamilifu wa hizo terms kabla ya kufikia maamuzi mengine,pia mambo kama haya yanaongeleka zaidi ya kufanya kama ilivyoamuriwa na Msanii.

Mfuate DIRECTOR huyu kujua nini alicholalamika juu ya dhuruma aliyoipata kutoka kwa Msanii huyu.


A video posted by NISHER (@nisherx) on

Sunday, May 22, 2016

Nyimbo mpya kutoka kwa Light Fetty inaitwa Jitu Zima ikiwa ni Track yake ya Sita katika muendelezo wa track zake kali,Chukua muda wako wa dakika tatu kusikiliza kipi hasa katika Jitu Zima.
Enjoy!!!!!

Saturday, May 21, 2016

ali-k
AliKiba tayari ameiachia Youtube video ya ngoma yake mpya Aje.
Imeongozwa na Director aliyefanya ‘Chekecha’ Meji alabi, Production ya Wimbo huu ni kutoka Chaiders Records kwa Abby Daddy.
Mayunga ft.Akon - Please don't go away!!!!....| NEW TRACK
Mayunga, winner of the first edition of Airtel TRACE Music Star, releases his new video for "Please Don't Go Away" featuring Akon.

Wednesday, May 18, 2016


Tuesday, May 17, 2016



Saturday, May 14, 2016

 Baada ya Kudhalilishwa kwenye mitandao,Lady Jaydee aitafuta Haki yake kwa njia ya Mahakama...Amtaka Gardner kuomba msamaha mbele ya Umma



Friday, May 13, 2016

Single mpya kutoka kwa Alikiba kutoka Tanzania akimshirikisha M.I toka Nigeria.Bonge moja la Collabo..Enjoy!!!!
Sikiliza track mpya kutoka kwa Pizzaro - Wamesanda,Baada ya YCEE na Dremo kutoka Nigeria kufanya Cover za Single ya Panda ya Desiigner.Sikiliza utofauti ya style alizopita Pizzaro kutoka Tanzania.

Wednesday, May 11, 2016

Grass Ain't Greener (On The Other Side) Lyrics

Advisory - the following lyrics contain explicit language:
[Verse 1]
You ain't the girl that you used to be
You say you're done, you're moving on
This ain't the world that it used to be
Looks like you've won, looks like you've won
Sick of leaving messages on your cell
But you never fuck with none of them
Yeah you have somebody who really cares
How you work it up, it is unfair
[Chorus]
You used to be the one to talk to on the side
Waiting for my love to break up
It's crazy how your ass ain't walk through every night
Acting like you been a player
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah
[Verse 2]
Seems like we ain't nothing cool, never being real
Know it's time to tell about how you feel
Take you whole and try to treat you well
She'll be back up at the club again
I know what you want, but you're not gon' get it
That's enough for sure that you gotten with it
You do what you want with somebody else
I'm gone, baby
[Chorus]
You used to be the one to talk to on the side
Waiting for my love to break up
It's crazy how your ass ain't walk through every night
Acting like you been a player
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah
[Verse 3]
My homie said I need to stop it
My momma said bitches be watching you
They be putting their hands all in your pocket
But the credit card that's in your wallet
Drinking liquor when we celebrating
Calculating all my funds
Tryna get a nigga take the condom off
Cause she want that tax every month, woo
I know what you want, but you're not gon' get it
Take my kindess for weakness
When you act siddity
Keeping it 100
Ain't your forté
You used to be
[Chorus]
You used to be the one to talk to on the side
Waiting for my love to break up
It crazy how your ass ain't walk through every night
Acting like you been a player
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah
That grass ain't greener on the other side
Oh yeah


A photo posted by THE KING OF DANCE IN AFRICA (@mcgalaxymcg) on

Tuesday, May 10, 2016

Serikali imetangaza rasmi kuanza kwa tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita katika daraja la Nyerere kuanzia Jumamosi tarehe 14 ,mwezi huu.


Akizungumzia na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema kuwa kuanzia siku hiyo , vyombo vyote vya usafiri vitatakiwa kulipia ushuru wa kupita katika daraja la Nyerere.


“Tumeanza kutoza tozo hii mara baada ya kufunguliwa kwa daraja hili na kuanza kutumika kwa kupita bila kulipa kwa vyombo vya usafiri tangu Aprili 19 mwaka huu na sasa tunaanza rasmi kutoza tozo kwa ajili ya kukusanya gharama za usimamizi, utunzaji na uendeshaji wa daraja hili.” alisema Mhandisi Nyamhanga.


Mhandisi Nyamhanga amefafanua kwamba watembea kwa miguu watapita bure katika daraja hilo huku wenye baiskeli wakilipia Sh. 300, pikipiki Sh. 600, waendesha maguta ,bajaji na magari ya kawaida(Saloon Cars) watatakiwa kulipia Sh.1500.


Mabasi yanayobeba abiria 15 yatalipia Sh. 3,000, yale ya abiria zaidi ya 15 Sh. 5,000 na yale yanayobeba abiria zaidi ya 29 yatalipia Sh. 7,000.


Aidha magari yenye tani zaidi ya mbili mpaka saba yatalipia Sh. 7,000, tani 7 hadi 15 watalipa Sh.10,000, tani 15 mpaka 20 watalipa Sh.15,000 na yale yenye tani 20 mpaka 30 yatalipia Sh. 20,000.


Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa magari yenye namba za Jeshi la Wananchi(JWTZ), Jeshi la Polisi(PT), Jeshi la Magereza(MT), gari za wagonjwa, magari ya zimamoto na magari yenye vibali maalum yataruhusiwa kupita bure.
Mbunge Apinga Wakunga Wanaume Kuhudumia Wanawake Wakati wa Kujifungua


Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Mngwali amepinga mpango wa Serikali kuajiri wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati kuhudumia wajawazito wakati wa kujifungua kuwa ni udhalilishaji dhidi ya wanawake. 

Mbunge huyo ameitaka Serikali kuzingatia mila za Kiafrika, akisema imezoeleka kuwa huduma ya ukunga kwa wajawazito wakati wa kujifungua hutolewa na wataalamu wanawake.

“Serikali haioni kuwa kwa kuweka wakunga wanaume katika baadhi ya zahanati zake nchini ni kuwadhalilisha wajawazito wanaojifungua?”alihoji Mngwali.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jaffo alisema wakunga wanafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya Uuguzi na Ukunga inayowataka kutoa huduma ya kumsimamia mjamzito wakati wa uchungu, kujifungua na baada ya kujifungua bila kujali jinsia.

Alisema pamoja na sheria hiyo, kumekuwa na changamoto zinazotokana na mila na desturi za jamii ambazo husababisha baadhi ya wahitaji wa huduma hiyo kutokubali kuhudumiwa na wakunga wanaume.

“Kutokana na hali hii, Serikali itaendelea kuajiri wataalamu wengi ili pale penye changamoto paweze kupatiwa ufumbuzi bila kukwaza jamii husika,” alisema Jaffo.

Naibu waziri alisema hiyo ilikuwa ni mara ya pili kwa mbunge huyo kuuliza swali hilo bungeni, lakini tayari amewasiliana na uongozi wa Mkoa wa Pwani ambao umeeleza kuanza kulifanyia kazi jambo hilo na kwa baadhi ya maeneo wameshaanza kupeleka wakunga wanawake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dr. Hamisi Kigwangalla, amemtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner G Habash kumuomba radhi aliyekuwa mke wake, Lady Jaydee kwa ‘kile alichokiita’ kama udhalilishaji kwake na kwa wanawake wote
Wikiendi iliyoisha imesambaa video mtandaoni ikimuonesha mtangazaji huyo akiongea kwenye tamasha alilokuwa mshereheshaji: My name is Captain Gardner G Habash all the way from Clouds FM, Jahazi hatari sana. Na sina neno na yule mtoto wa kike. Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi.”
Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Jaydee na watu wengi kwa ujumla
ITAZAME HAPA!!!



Saturday, May 7, 2016


Friday, May 6, 2016


Thursday, May 5, 2016

Vyombo vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza.
Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti.
Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti.
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
“Ni kweli kwamba Tanzania  bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.
Pop staa Janet Jackson anategemea kupata mtoto wake wa kwanza baada ya kukatisha ziara yake ya show kutokana na ujauzito.
Taarifa hizi nzuri zimekuja wiki mbili kabla staa huyu hajafikisha miaka 50 kwa sasa anamiaka 49 na atakuwa na 50 mnamo May 16 2016.
Janet ameolewa na Wissam Al Mana ’41’ mwaka 2012 kwneye harusi ya siri na hawakuthibitisha taarifa hizi mpaka mwaka 2013.
Mwaka 2008 wakati Janet alikuwa na mpenzi wake Jermaine Dupri, aliulizwa kuhusu watoto na alijibu “Napenda kuwa na watoto ila pia nataka kuasili mtoto”
Hivi karibuni atatoa video mpya ya “Dammn Baby,” kutoka kwenye album ya mwaka 2015 Unbreakable

Tuesday, May 3, 2016




IJUMAA HII NA KILA IJUMAA NDANI YA ESCAPE ONE - QS INTERNATIONAL MUSIC BAND WANAKULETEA LIVE SHOW NA RED CARPET YA MASTAA WA BONGO MOVIE,NA VIONGOZI MBALI MBALI KWA KIINGILIO CHA SHILINGI 10,000/= TU.

PERFOMANCE YA STAGE ITAWAKILISHWA NA:-

> MFALME MZEE YUSUPH NA JAHAZI MODERN TAARABU,
>Q-CHILLAH/Q-CHIEF
>BUSHOKE
>MB-DOG
>KADJA NITO
>MEDDY
>AMOUR GENIUS
>FELLY KANO
>OMMY RADI
>BIBE MELODY
>FONDEE
>BOY ZONE

Ni ndani ya Escape One Mikocheni Jijini Dar es Salaam,QS International Music Band wanakuletea Show ya kijanja ambayo itaunganisha Mastar wa kutosha toka pande zote za Jiji la Dar navitongoji vyake Huku UKIJIBURUDISHA NA NYAMACHOMA,VINYWAJI BARIIDI,MUZIKI MZURI NA KILA AINA YA BURUDANI ni ndani ya Escape One.Nyote Mnakaribishwa.











Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ