• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Tuesday, January 29, 2013

Sunday, January 27, 2013

Thursday, January 17, 2013




MASHAIRI YA STAMINA ft. FID Q - WAZO LA LEO.
Song:Wazo La Leo                                              
Artist:Stamina Feat Fid Q
Studio:Bongo Records
Producer: P funk Majani
Song Writters:Stamina (verses) & Fid Q (chorus)

Intro...
U know what majani??nice to meet you homie
Its moro town baby,,,shorobwenzi

Verse 1. (Stamina)
Elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu
Hip hop haijengwi na bifu,underground usijaze fomu
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku hizi hazioti
Maisha njia panda,mtembezi chagua pa kwenda
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe suspenda
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha ushamba
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 2.(Stamina)

Underground panga tenzi,ustar hauji kwa promo
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku punguza ngono
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba
Mapenzi yakikusumbua,tafuta daktari wa kitanga
Vazi unaloishi,mwenyezi yeye ndio disegner
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna
Dunia duara,jitahidi uizunguke
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke
Huna undugu na bakhersa,niaje aje unakula unga
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi
Mwambie na dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje kupewa
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa
Sharo mpe salamu,the great braza kanumba
Mwambie bongo sio tamu,na lulu bado wamemfunga

Chorus(fid q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}

Verse 3.(Stamina)

Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza
Nchi tayari imekonda,mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,kidonda anafanya mtaji
ukipata mazuri,jipange kuikwepa hasara
kijana vazi la msuli,haliwezi kukuvisha busara
ukiishi kwa hisia,kila stone litakubanza
cha msingi ni kuweka nia,ujivue kuwa mtanza
kata ya kijiji,haibebi maji ya maendeleo
katibu tunza mkwiji,msuli ukishuka kimeo
uchumi umeshika tama,kwenye shavu la mlanguzi
raia usilaumu chama,shiriki kwenye uchaguzi
unaweza ukavaa kinga,ila ukafa kwa uaminifu
mzinzi usigawe ujinga,sambaza ujumbe wasifu
hakuna snitch kama pesa,ukiwa nae fanya vya maana
akiondoka atakutesa,utamsaka usiku na mchana

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona,baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo
{Hilo ndo wazo la leo}-inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha.
{hilo ndo wazo la leo}-usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako-{hilo ndo wazo}
 
SAJNA 
“Ni kitambo kirefu sana nimekuwa kimya kutokana na maswala ya shule ila sasa kidogo nimetulia. NImeamua kuuachia wimbo huu unaitwa ROHO MBAYA ambao nimewashirikisha BELLE 9 na PIPI kama zawadi yangu kwa fans wangu, lakini official single ya mwaka huu inafuata siku si nyingi. Beat ilifanywa na Duke wa M-Lab na vocals zilifanywa na Tetemesha Records mwaka juzi.Tegemeeni mengi mazuri kutoka kwangu kwa mwaka huu – Sajna.

Wednesday, January 16, 2013

Snura Mushi

Saturday, January 5, 2013


Hiki ndicho alichokiongea ROMA!!

Habari  Mabibi  na Mabwana!! poleni  na mihangaiko ya  siku!! naam
ijumaa  iliyopita  nilitoa  kibao   changu  maridhawa  kipya  kabisa  kinaitwa  2030!!!
na nilikiachia  kwa radio  stations zote  nchini  kadri  ya  uwezo wangu/wetu, though kutokana na mawasiliano  ni ngumu kufikia  radio  zote kwa wakati, ila  nyingi ziliupata!!!
lakini niliweka  utaratibu  fulani  kwa watakaohitaji  kuupata  huo wimbo 2030 mbali na radio basi wataupata  kwa  kussuport  kuununua  on line  kwa  tsh 3000/=!!nilishatangaza sana  mnafahamu!!ilikuwa  ni trial  ya kuona nani ana love ya kussuport na nani hana kupitia njia  zilizowekwa na sio njia  nyingine.
 zoezi  limeenda  kwa challenge  nyingi sana  asante  wote  waliossuport  katika  hili,  pia  asante  kwa wale  walioliharibu zoezi hili maana  imenifanya  nimtambue  hu z real na hu z fake!!!
imeniuma kuona wapo wasanii wanafanya  biashara  kama hii wanauza mix tapes, album,tisherts  zikiwa  zote  ni movements  za kuleta  changes  ktk mziki wetu, then hao hao wanakuwa mstari wa mbele kupinga hii movement yangu  halafu bila sababu yani dah SHALL WE MAKE IT?????
nway  lilikuwa  ni zoezi  lililopangwa kufanyika  kwa week moja 1 tu ili kuona na kufanya tathmini  kuwa  yanawezekana haya?najua  wengi wanasubiri feed back ya mauzo haya haikuwa  nzuri sana kwa  wingi wa nyomi nililokuwa nalo, lakini pia  haikuwa  mbaya maana  ni mageni haya..kwa  siku 7  za mauzo  ilikuwa kila  siku wananunua watu wasiopungua  50!! so  unaweza  ona  hapo  kuwa  yanawezekana  haya  tukiyawekea  mkazo...ILA SIAMINI KAMA KILA MSANII ANAWEZA  FANYA, INATEGEMEA  NA NGUVU YA MSANII HUSIKA NA KIBAO ALICHOKITOA..(IFIKIE KIPINDI  TUONGEE  UKWELI  TUU!!)wengi wameanza kufanya biashara  kupitia  nyimbo hii na inawanufaisha  wao, wengi wamerecord radio wimbo huu kitu kilichopelekea  kukosa quality na bado wanauzia  wengine so wanapewa kitu kisicho na quality, pia wengi  wanakwazika  na mengi yaliyoongelewa ndani ya wimbo huu na wanakosa majibu maana  wanakosa fursa ya kuusikia  mara  kwa mara kwasababu hawajaunga mkono hii movement!! au pengine  imekuwa ni njia  ngumu kwao kuupata,
basi  kwa  wale  waliossuport  kwa kuinunua  nawashukuru sana na mungu awaongezee mlipopungukiwa, najua  litatokea hili la kujiona wanyonge  kuwa  ROMA amechukua  fedha  zetu  na kisha ameachia  bure, mi naamini ukiwa muelewa na ukiona nilichokisema hapo juu  hautakwazika  as  long umeonyesha  lav yako kwa msanii unayemfeel, samahani sana kama nitakuwa  nimekukosea,nimefanya hivi  kama kuanzisha  hiki kitu  na naamini  wengine watafatia  na kukiboresha  zaidi!!LAZIMA  APOTEE  MMOJA  ILI KUMI WAISHI  VEMA NDIPO YATAPATIKANA MAENDELEO!!  AM SO SORRY!!!
 So leo wiki imetimia na wimbo  umetoka rasmi na hauuzwi tena kama ilivyotangazwa  awali.
unapatikana  bure  kwenye  net, download  via  access yoyote utakayoiona!! nimeutoa rasmi kwenye  blogs  mbali mbali  ANZIA NA YA DJ CHOKA,  na  nyinginezo!!
Na version  iliyopita  kuchezwa  radio  ni  version  ya  ROMA ile beat yake iliyochangamka ambayo ni version ya 1  ambayo  ndiyo ilikuwa ya kwanza kutambulishwa ijumaa pale  clouds fm radio.
kwa  maswali  zaidi  tutameet   kwenye  mainterviewz  huko maradioni na tutawekana sawa!!
samahanini  kwa  wote  niliowakwaza, asanteni  kwa  wote  mliossuport!!
ROMA  2030 INAPATIKANA FREE  SASA!!!


 ANAITWA STORY NDIYO HUYO ALIYEIMBA CHORUS YA 2030 
 (ILE SAUTI YA KITOTO KIDOGO NDO HUYU)
LISTEN / DOWNLOAD HERE!!!
SOURCE :  DJCHOKA BLOG!!!

Wednesday, January 2, 2013


Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ