• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Wednesday, April 29, 2015


Tuesday, April 28, 2015

tiwa-tj-wedding-tent-setup-dubai-600x600 
Ni couple ya mastar kutoka Nigeria Tiwa Savage na Tunji Balogun imeingia kwenye Headlines wametimiza mwaka mmoja tangu wafunge ndoa April 26 2014.
Tiwa kwa sasa ni mjamzito, jana alipost picha nyingine jinsi walivyo enjoy siku yao pamoja na maneno haya;
 “lol at this is how we ended up creating you Hey baby, look what daddy did for mummy today. Breakfast in bed, church, romantic dinner, candles and rose petals all over our hotel room, lots and lots of gifts and love. This is how we ended up creating you in the first place oooo lol. We love you daddy, thank you for a magical day”@
IMG_1869 
Wakaona siku isipite hivi.. surprise kwa fans wao ni hizi picha nyingine za harusi yao ambazo hawakuwahi kuzitoa kabisa…



IMG_1815
IMG_1816
IMG_1817
tiwa-tj-wedding-tent-setup-dubai-600x600
IMG_1816
Un

Monday, April 27, 2015


A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari


B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
Bonyeza  Hapo Chini Kuona  Orodha  Ya  Majina:

1.Ajira za Walimu wa Cheti (Shule za Msingi) 2015BOFYA HAPA KUYAPATA YA CHETI/SHULE ZA MSINGI

2.Ajira za Walimu wa Sayansi wa Shahada na Stashahada kwa Mwaka 2015BOFYA HAPA KUYAPATA YA SAYANSI NA STASHAHADA

3.Ajira za Walimu wa Masomo ya Sanaa na Biashara Ngazi ya Shahada na StashahadaBOFYA HAPA KUYAPATA YA SANAA NA BIASHARA NGAZI YA SHAHADA NA STASHAHADA

Thursday, April 23, 2015


Leo Jumanne 21 Aprili 2015 mida ya saa 8 mchana watu wanne wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamekamatwa baada ya kumuibia mzungu ambaye jina lake halikufahamika mara moja, karibu na benki ya Stanbic Kinondoni jijini Dar es salaam, watuhumiwa hao walifanikiwa kukimbia lakini walikamatwa mtaa wa Redcross jijini Dar es salaam.
.
 



Watuhumiwa hao walikuwa na bunduki mbili, na baada ya tukio hilo mtu mmoja ambae naye jina halikufahamika mara moja aliamua kuwafuatilia watu hao nyuma nyuma mpaka hapo redcross kwenye mataa ndio akawaziba njia kwa sababu kuna askari.

Watuhumiwa hao walizobwa njia wakashuka na bunduki ndipo askari waliokuwepo eneo hilo wakawaweka chini ya ulinzi. na kuwakamata na kupelekwa kituo cha polisi…..Watuhumiwa hao walikuwa wanne.




Sunday, April 19, 2015


 BEST TANZANIAN UNIVERSITIES 2015: Latest Rankings 23 February 2015.
A list of best universities has just gotten out and the result is something removed from the old ones we have seen before. Most universities have however worked extremely harder to make the list of top 51 best universities in Tanzania while some others have skimmed off the list because they couldn’t increase their pace of improvements on certain things forming criteria for ranking.


Note that in ranking these universities, four  major factors have been considered:
i. their presence,
ii. rate of Impact,
iii. openness and
iv. academic excellence


Based on the world ranking web of universities, below are the 20 best universities in Tanzania and also their world ranking in bracket.

1. University of Dar Es Salaam (World rank: 2475)
2. Sokoine University of Agriculture (World rank:
4244)

3. Muhimbili University of Health and Allied
Sciences (World rank: 4642)

4. Open University of Tanzania (World rank:
5786)

5.University of Dodoma (World rank: 8368)
6. Hubert Kairuki Memorial University (World rank: 10813)
7. Mzumbe University (World rank: 12170)
8. Institute of Finance Management (World rank:14298)
9. Mkwawa University College of Education
(World rank: 14320)

10. Nelson Mandela African Institute of Science and Technology (World rank: 15090)
11. Ardhi University (World rank: 16008)
12.Weill Bugando University College of Health Sciences (World rank: 16071)
13. Dar Es Salaam Institute of Technology (World rank: 16185)
14.Kilimanjaro Christian Medical University College (World rank: 16508)
15. Saint John’s University of Tanzania (World rank: 16516)
16. Saint Augustine University of Tanzania (World rank: 16534)
17. Tumaini University Makumira University
College (World rank: 17267)

18. State University of Zanzibar (World rank: 17365)
19. Moshi University College of Co-operative and Business Studies (World rank: 18253)
20. Mount Meru University (World rank: 18477)

Sunday, April 12, 2015

Mohamed Badie

Mahakama moja nchini Misri imethibitisha hukumu ya kifo ya kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na watu wengine 13 kwa kupanga mashambulizi dhidi ya serikali.
Pia mahakama hiyo imemfunga maisha raia mmoja mwenye uraia wa Marekani na Misri na watu wengine 36.
Badie alipewa hukumu hiyo mnamo mwezi Machi na pia anakabiliwa na mashtaka mengine.
Hatahivyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Mamia ya watu wamehukumiwa kifo katika msako dhidi ya wanachama wa kundi hilo kufuatia kuondolewa kwa rais Mohammed Morsi mwaka 2013.
Hatahivyo ,kufikia sasa ni mtu mmoja pekee aliyenyongwa.
Uamuzi huo wa mahakama ulitangazwa moja kwa moja na runinga za taifa hilo.
Hukumu hizo ni za mwisho katika kesi ambayo viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood walishtakiwa kwa kuwachochea wanachama wa kundi hilo kuanzisha ghasia dhidi ya serikali kufuatia maandamano ya mwaka 2013.


Familia za wanafunzi 142 kati ya watu 148 waliouawa katika shambulizi la kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab katika chuo kikuu cha Garissa wameruhusiwa kuchukua miili ya wapendwa wao.
Familia zimeanza harakati za safari ya mwisho ya wapendwa wao baada ya serikali ya Kenya kuwaruhusu kuzichukua miili kutoka kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo jijini Nairobi.
Huu hapa mukhtasari wa matukio baada ya shambulizi hilo.
1.Shambulizi
Takriban wanamgambo 5 wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab washambulia chuo kikuu cha Garissa alfajiri.
Waliwapata wanafunzi wakiwa wamelala.
Waliingia chuoni baada ya kuua walinzi wawili langoni.
Walionusurika wanasema kuwa wavamizi hao waliwabagua wanafunzi waislamu na kuwaua wakristu.
2.Uhuru ahakikisha taifa
Serikali ilitangaza kuwa watu 70 walikuwa wameripotiwa kuuawa na wengine 79 kuripotiwa kujeruhiwa.
Waziri wa usalama wa taifa generali mstaafu Joseph Nkaissery alitangaza idadi ya waliouawa kuwa ni 148 na kusema kuwa operesheni ilikuwa imekamilika
3.Idadi ya waliouawa yatangazwa
Wanafunzi 500 wameokolewa na maafisa wa usalama
Rais Uhuru Kenyatta ahutubia taifa na kutuma risala za rambirambi kwa wale waliouawa.
Serikali ilionyesha hadharani miili ya wanamgambo waliouawa na kuonyesha picha ya raia mmoja kutoka Tanzania aliyekamatwa.
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa Serikali yake itachukua hatua kali dhidi ya wakenya wanaolisaidia Al Shabaab.
Serikali yakiri kuwa mmoja kati ya washambuliaji hao alikuwa ni mwanawe Chifu wa kata ya Mandera.
Chifu huyo yamkini alikuwa ameripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwake mwaka uliopita.
4.Maswali yaibuka kuhusu Operesheni
Maswali yaibuka kuhusu hatua zilizochukuliwa na polisi baada ya kuarifiwa kuhusu shambulizi hilo.
Wananchi waizomea serikali kwa kutumia ndege kuwasafirisha waziri wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery na Inspekta mkuu wa polisi Joseph Boinett
huku kikosi maalum cha kupambana na magaidi al maarufu (RECCE) kikilazimika kusafiri kwa gari kwa zaidi ya saa saba.
Kikosi hicho kilitumia chini ya dakika 15 pekee kukamilisha operesheni hiyo.
5.Makurutu 10,000
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa makurutu 10,000 wa polisi waliokuwa wamepigwa marufuku na mahakama kufuatia madai
ya rushwa sasa hawatakuwa na budi ila kuingia katika chuo cha mafunzo ya Polisi ilikuimarisha idadi ya polisi na vilevile usalama wa taifa.
Mahakama ilikuwa imeharamisha kusajiliwa kwao kufuatia madai ya rushwa katika usajili.
6.Waliotekeleza Shambulizi watajwa
Raia wa Kenya Mohamed Kuno kwa jina jingine Mohamed Dulyadin,atajwa kuwa ndiye mshukiwa mkuu.
Serikali ya Kenya imetoa ruzuku ya shilingi milioni 20 za Kenya yaani dola $215,000 za kimarekani.
Kuno aliwahi kuwa mwalimu katika eneo la Garissa kabla ya kustaafu na kujiunga na kundi hilo.
Mwengine aliyetajwa ni wakili Abdirahim Abdullahi aliyeongoza uvamizi huo.
Wanafunzi walionusurika Rais Uhuru Kenyatta aonya kuwa wale wanaoendeleza sera za Al Shabaab wako miongoni mwa wakenya.
7.Maiti yaletwa Nairobi
Maiti ya wahanga wa mauaji hayo yaletwa mjini Nairobi kwa ndege za kijeshi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi mjini Nairobi.
Kituo cha kuwapokea waathiriwa wa mauaji hayo na jamaa zao kinaundwa katika uwanja wa michezo wa Nyayo mjini Nairobi.
Orodha ya wanafunzi waliouawa na wale waliojeruhiwa inapachikwa katika lango la uwanja wa Nyayo.
8.Serikali yafunga miundo mbinu ya uchumi wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya yatangaza orodha ya mashirika kumi na tatu na akaunti za watu
binafsi wapatao 86 wanaoshukiwa kuhusika na ufadhili wa kundi la kigaidi la Al Shabaab Garissa.
Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa wakifuatiliwa mienendo yao.
kampuni 13 za ubadilishaji na usafirishaji wa fedha nazo zimefungwa.
Jamii ya wasomali yalalamikia hatua hiyo ikisema ni mtego ambao umenasa waliokuwemo na wasiokuwemo.
9.Utambuaji wa maiti Chiromo
Shughuli ya utambuaji wa maiti yaanza huku familia nyingi zikitatizika kutambua miili ya wapendwa wao kufuatia kuharibiwa kabisa kwa miili.
Miili mingi ilikuwa na majeraha ya risasi kichwani.
Serikali ya Kenya yalazimika kutumia mashine maalum ya kutambua chembechembe za damu za DNA ili kuharakisha utambuzi wa miili.
Dukuduku zaibuka kuhusiana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wazazi ambao wamekosa miili ya wapendwa wao.
Muungano wa walimu na wafanyikazi wa vyuo vikuu (UASU) yadai kuwa takriban wanafunzi 166 hawajulikani waliko.
10.Uhuru aomboleza
Rais Uhuru Kenyatta jana aliwaandikia barua kila familia iliyopoteza mpendwa wao.
Wote walioathirika walipewa shilingi laki moja za Kenya,Jeneza na gari la kusafirishia maiti hadi makwao.
Makumi ya raia wa kigeni wakamatwa kote nchini kufuatia msako mkali unaoendelea
Chanzo:bbc swahili

Thursday, April 9, 2015


A man walks past a large pool of water following rains on March 22, 2015 that resulted in flooding around some residential areas of Dar es Salaam. The rainy season, which began this week, is expected to bring ‘normal to moderate’ rain levels to coastal Tanzania, says the Tanzania Meteorological Agency. (Daniel Hayduk/AFP/Getty Images)

I landed in Dar es Salaam over the weekend to prepare for a research workshop on Tanzania’s natural gas sector.  “We need a quote from a government official saying that they think this research is a good idea,” my co-author, Mujobu Moyo, announced.  “Otherwise journalists might be hesitant to cover it.”
Welcome to election year in Tanzania. On March 27, the Tanzanian parliament passed a “new draconian data law” that would allegedlycriminalize the publication of any statistics not endorsed by the National Bureau of Statistics, with minimum penalties of one year in prison or a $6,000 fine. I say allegedly, because nobody seems to be able to find the actual bill. President Jakaya Kikwete hasn’t given any indication yet whether he’ll sign it, though it was rushed through parliament with backing from the ruling party.
Somewhat awkwardly for the Obama administration, Kikwete has also taken a lead role in the Open Government Partnership — a multilateral initiative hatched by the White House to promote government transparency worldwide.
So what is the Tanzanian government trying to hide? The specific provocation behind the bill is unclear. But in the spirit of thumbing one’s nose at government overreach, here’s a sampling of unofficial, but highly reputable statistics about Tanzania that might explain what’s going on.
1. Only a third of children can read in English
Like many other African countries, Tanzania has made huge strides in expanding basic services like health and education. The primary school enrollment rate, for instance, is officially at 94%. But “unofficial” statistics suggest the quality of those services is often quite poor.
Only about a third of kids age 10 and above can read an English paragraph from the second-grade syllabus. And while Tanzania prides itself as the home of Kiswahili in East Africa, Tanzanian children also score lower than their Kenyan neighbors on Kiswahili literacy.

This data comes from Twaweza, a Tanzanian civil society organization that has made a splash by combining independent data collection, rigorous analysis, and strident advocacy around issues like the poor quality of education, access to water, and other basic services. Not surprisingly, organizations like Twaweza, founded and run by Tanzanians, are largely dependent on European aid agencies and U.S. philanthropic organizations for funds (much like my own employer in Washington, D.C.).  That probably protects their ability to keep collecting data, but perhaps not to keep disseminating it locally.
2. Teachers are absent from class most of the time.
Perhaps it’s no surprise kids can’t read, since teachers are never in class. Nationwide, teachers are absent from school about 23 percent of the time, but in random visits to classrooms, they’re absent from their actual classroom more than 50 percent of the time on the days they’re counted as present.
This damning statistic doesn’t come from a rabble-rousing advocacy group, but from the World Bank. Big foreign aid donors like the Bank are increasingly stepping outside their normal mandate of dealing directly with the government as a client, and taking a message of government failure directly to the public.  It’s unclear whether the Tanzanian public has taken much notice, but the new data law suggests the government has.
3. Most doctors can’t correctly diagnose the ailments that kill the most Tanzanians
Lest you think Tanzania’s challenges with basic services were limited to education, here’s an eye-opening statistic on health services, from the same World Bank study cited above. Researchers presented clinicians with hypothetical patients, suffering from a variety of symptoms that commonly afflict Tanzanians, and tested whether they could offer a correct diagnosis.
Shockingly, only 27 percent of doctors could correctly diagnosis malaria with anemia, and 29 percent could correctly diagnose diarrhea with severe dehydration — two leading causes of death for Tanzanians.
4. Nevertheless, Tanzania’s economic growth record has been fairly strong
In some cases, Tanzania’s new statistics law is futile. For instance, lots of interesting data on Tanzania is collected from outer space.  Recent research using NASA’s “Night Lights” shows that increases in luminosity viewed from space correlate pretty well with economic growth.  Researchers can use the night lights to validate official national accounts data, and in the case of Tanzania, the two seem to roughly agree (see Figure 6b here).
Officially, Tanzania has been growing at a healthy 7 percent for the past decade, and Tanzania’s ruling party, Chama Cha Mapinduzi (CCM), is eager to run on that track record.  It seems the party has nothing to fear from independent data collection — though there’s not much the party leaders could do about it anyway.
5. And most Tanzanians are satisfied with their democracy
A majority of Tanzanians support democracy over authoritarian rule, and more than two-thirds consider Tanzania to be a democracy and say they’re satisfied with its performance — even if it may soon be a crime to report that fact.
This finding comes from the Afrobarometer survey run by REPOA in Tanzania, a think tank with a fairly collaborative relationship with the government. Suffice it to say that if the new statistics bill indeed becomes law, selective enforcement is almost guaranteed.
The foreign aid donors who finance much of the independent data on Tanzania’s development are beyond the reach of this new crackdown — but the Tanzanian researchers, journalists, and activists who are pioneering a more open, evidence-based policy conversation may not be so lucky.
As the saying goes, “you are entitled to your own opinion; you are not entitled to your own facts.” Tanzania’s parliament seems to have embraced the message, but missed the point.

Wednesday, April 8, 2015


Kenya imefunga mashirika 13 na akaunti 86 za watu wanaodhaniwa fufadhili Al Shabaab
Jamii ya wasomali nchini Kenya wamelalamikia vikali hatua ya serikali nchini humo kufunga mashirika kumi na tatu ya ubadilishaji wa sarafu za kigeni na usafirishaji pesa maarufu kama Hawala.
Malalamishi yao ni kuwa hatua hiyo itasababisha matatizo makubwa kwa wasomali ambao daima wanategemea njia hiyo, kuwatumia jamaa zao fedha kutoka mataifa ya kigeni.
Hatua hiyo imefanyika baada ya shambulio la Al-Shaabab katika Chuo kikuu mjini Garrisa juma lililopita.
Serikali ya Uhuru Kenyatta inasema kuwa ni mojawepo ya njia ya kuzuia al-Shabaab kupata fedha ili kupanga na kutekeleza mashambulio zaidi.
Hali ya hatari ya kutotembea nje usiku pia imewekwa katika majimbo yaliyo na wasomali wengi kazkazini mashariki mwa Kenya.
Akaunti za Benki za watu themanini na sita zinazodhaniwa kufadhili ugaidi pia zimesitisha.

Gavana wa benki mkuu ya Somalia Bashir Issa Ali ameiambia shirika la habari la Reuters amethibitisha kuwa amepokea ilani hiyo kutoka kwa benki kuu ya Kenya.
Waziri wa maswala ya kigeni wa Kenya Amina Mohamed amesema kuwa nchi yake imeomba msaada wa kijasusi kutoka mataifa ya magharibi
kufuatia shambulizi baya zaidi katika miaka ya hivi punde iliyosababisha vifo vya watu 148 wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa chuo kikuu cha Garissa.

Monday, April 6, 2015

Hilo lilikuja kama swali jingine tena katika E-mail nilotumiwa na Followers wangu na nikaona . Nianze kwa kusema kwamba mfanyabiashara na mjasiriamali wana tabia nyingi zakufanana.Ukiangalia zaidi, neno mfanyabiashara lipo tangu zamani lakini neno mjasiriamali ni jipya.
Wote hawa wanasababisha kuwepo kwa ajira, wanatatua matatizo ya wateja wao na pia wanasaidia maendeleo ya uchumi wa nchi. Tukiangalia maana ya maneno haya, haswa neno mjasiriamali, ndipo tunapoona tofauti. Neno hili ni la Kifaransa kwa asili lenye maana isemayo; Mjasiriamali ni mtu ambae amezungukwa na fursa mbalimbali, anayethubutu kutumia fursa hiyo kupata faida huku akihatarisha kupoteza mtaji wake. Hii ni maana niliojifunza zamani lakini maana yangu ya sasa ni hii; mjasiriamali ni mtu ambae ameanzisha biashara anaisimamia, kupata faida na kubadilisha maisha ya jamii inayomzunguka.
Baada ya kuangalia maana ya neno hili sasa tuziangalie tofauti kati ya mjasiriamali na mfanyabiashara.
Tofauti ya KWANZA ni CHANZO cha biashara. Mfano mfanyabiashara anaweza anzisha biashara inayofanana na biashara nyingine aliyoiona. Kaona mtu ana banda la chips, nae anaanzisha banda la chips pembeni. Huwa wanafanya biashara ya vitu ambavyo wengine wanafanya katika mazingira waliopo, na mara nyingi huwa si wabunifu.
Lakini Mjasiriamali yeye anatumia akili, nguvu zake na pesa katika kuvumbua wazo jipya la kibiashara. Kwa ufupi Mjasiriamali ni mbunifu wa wazo la kibiashara. Na wajasiriamali wa kweli huwa ni wachache. Na hata wakianzisha biashara inayofanywa, wao huhakikisha inatoa bidhaa au huduma bora zaidi (They are very innovative) Mfano mzuri ni mtu kama Mengi, yeye hupenda kuanzisha biashara toka sifuri na ikiwezekana hupenda kufanya biashara ambayo haijawahi kufanywa na mwingine.
Tofauti ya PILI ni jinsi watu hawa wanavyolichukulia swala la USHINDANI. Mfanyabiashara huwa anajitahidi kumshinda mshindani wake, ili yeye asimame kuwa mshindi. Mjasiriamali yeye hujitahidi kumshinda mshindani wake ambae ni yeye mwenyewe. Yaani, anashindana na yeye mwenyewe. Hivyo kwa Mjasiriamali si tatizo kumpeleka mteja wake kwa mjasiriamali au mfanyabishara mwingine kama yeye hawezi kumuhudumia. Mjasiriamali hupenda ushirikiano sio tu ushindani.
Tofauti ya TATU ni namna ya KUHATARISHA au kiwango cha Kuthubutu (Risk Taking). Mara nyingi wafanyabiashara wanaogopa sana kuthubutu, wanaogopa kwamba wanaweza kupata hasara. Lakini kwa wajasiriamali kuthubutu ni kitu cha kawaida kwao. Huwa wanathubutu katika mambo ya hatari mno kwasababu wana ule moyo wa kufanya kile wanachokifanya.
Tofauti ya NNE ni kwa jinsi wanavyoishi au kuwachukulia WAAJIRIWA wao, au wafanyakazi wao. Wafanyaniashara mara nyingi hujisikia kuwa wao ni mabosi kwa kuwa ni wakurugenzi wamiliki na hudharau wafanyakazi wao. Lakini Wajasiriamali wana moyo wa upendo na kujali wafanyakazi wao. Huwa ni marafiki wazuri na viongozi wazuri kwa wafanyakazi wao.
Tofauti ya TANO ni jinsi watu hawa wanavyouona MUDA na PESA. Wafanyabiashara hawataki kupoteza muda wala pesa zao. Wajasiriamali wao hawaogopi kupoteza muda. Mjasiriamali wa kweli huwa kama mwanasanaa au mwanasayansi katika maabara. Bidhaa yao ndio kila kitu kwao. Huduma zao huwa zinawatawala kwa nguvu. Mara zote hufikiria jinsi gani ya kuboresha huduma zao.
Tofauti ya SITA ni kwamba LENGO kubwa la wafanyabiashara ni kujiajiri, kujitawala wenyewe. Lakini lengo la Wajasiriamali ni kuubadilisha ulimwengu. Sio swala tu la kupata hela, ila ni kufikia lengo fulani kwaajili ya kuleta tofauti ulimwenguni.
Mara nyingi sana hawajali kupata hela, ila kuubadilisha ulimwengu kwa kufanya kitu kitakachoacha alama.
Hivyo kama wewe unazingatia kuubadili ulimwengu basi wewe ni Mjasiriamali.
Tofauti ya SABA ni jinsi watu hawa wawili wanavyouona ulimwengu.
Wafanyabiashara wanaona dunia kama fursa, lakini kwa mjasiriamali ni zaidi ya fursa. Kwa mjasiriamali yeye anaona dunia kama ni wajibu wake, kwa kusaidia watu na kutengeneza mazingira bora ya watu kuishi vizuri.
Tofauti ya NANE ni jinsi watu hawa wanavyoyaona mafanikio.
Mfanyabiashara huona mafanikio kwa jinsi ya mafanikio ya biashara yake yanavyokwenda. Lakini mjasiriamali mafanikio kwake ni kwa jinsi anavyoipenda kazi au huduma anayoifanya. Hajishughulishi na muda, au kuangalia jamii inaona nini kwa anachokifanya, ila yeye hujishughulisha na kuhudumia jamii. Na hapo ndipo mafanikio yake yanaonwa na kutangazwa na jamii.
Wote hawa wanahitajika katika jamii. Mfanyabiashara anamuhitaji Mjasiriamali na mjasiriamali anamuhitaji Mfanya biashara.
Sasa, baada ya kusikia haya unajiweka katika kundi gani? Je wewe ni Mjasiriamali au Mfanyabiashara? Una mpango gani wa kujiboresha katika Ujasiriamali wako?
Siku moja mtu mmoja aliniuliza swali "Hivi ujasiriamali ndio njia pekee ya kufanikiwa maishani?" Jibu ni hapana.
Duniani kote ziko njia kuu 4 ambazo watu hufikia uhuru wa kifedha.
1. Kupitia kuwa Afisa wa kampuni kubwa anaelipwa vizuri (Highly paid executive). Ukiwa mkurugenzi mkuu mtendaji wa TBL, CRDB, Cocacola, Vodacom etc mshahara wako ni milioni 20 au zaidi pamoja na marupurupu mengine ya kumwaga kila mwezi. Hivyo hawa mabosi tayari wana nafasi kubwa ya uhuru wa kifedha kama wataweka akiba na kuwekeza kwenye assets. Kama unavutiwa na njia hii jambo pekee ni kufanya bidii ya 'kufufuka mtu and to 'keep your nose clean' throughout your career. Na uwe tayari, sometime, kufanya kazi kwa miaka mingi sana ili kufika juu. Asilimia 10 ya matajiri wote duniani wanatoka kundi hili.
2. Kupitia kuwa Mwanataaluma aliyebobea. Flying doctors, (Think about the Ben Carsons of this world), wanasheria wakuu, top accountants etc! Wanalipwa vizuri. Hapa inabidi uwe umeenda shule kweli kweli ili ufike huko. Kama hauko vizuri darasani, huwezi ku win kwa njia hii. 10% ya matajiri wote wanatoka hapa.
3. Watu wa Mauzo au mameneja wa mauzo. Hawa hufika juu kama wako kwenye makampuni yenye kamisheni kwa wale wanaofanya vizuri! Huwa hakuna kikomo cha idadi ya watu unaoweza kuwauzia kama una ujuzi wa kutosha wa bidhaa unayoiuza, mipango mizuri inayotekelezeka na bidii ya hali ya juu. 5% ya matajiri wote hutokea kundi hili.
4. Watu wenye vipaji maalum; wanamichezo nyota, wanamuziki maarufu (The Diamonds of this world) wachekeshaji kama akina Masanja, Joti, nje akina Jerry Seinfeld, Chris Rock, Chris Tucker etc, waandishi mashuhuri akina John Grisham, Paolo Coelho, kina Shigongo hapa nyumbani n.k. Hawa huwa ni 1% tu ya matajiri wote ulimwenguni. Watu wengi hudhani hawa huwa ni wengi kwa sababu ya kufahamika kwao kupitia vyombo vya habari!
Sasa, guess what? Unajua tumebakisha asilimia ngapi?
74%. Yes 74%!. Asilimia 74 ya matajiri wote duniani ni WAJASIRIAMALI. Kuanzia kuuza mayai ya kanga, kufuga sungura, kuuza mazao, maduka, migahawa, elimu, internet biz, network marketing etc. Wote huo ni ujasiriamali. Watu wengi wana nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kwenye ujasiriamali kuliko hayo maeneo mengine manne. Ndio maana ninahubiri ujasiriamali! Najua ninaweza kuwasaidia watu wengi kupitia njia hii kuliko kupitia kuwa highly paid execs or professionals. But still jambo la muhimu sana kwako ni kufuata kitu ambacho roho yako inapenda. Swali muhimu ni, wewe unachagua mlango gani katika milango hii mitano? You can comment down below and share this na marafiki, ndugu au jamaa unaowajali ili waamue wanata kutokea kupitia mlango upi maishani!
Have a great week

Baada ya Nani Kama Mama - Mzee wa masauti aka King of Melodies Christian Bella ameachia hii ngoma yake mpya iitwayo Nashindwa, na video yake imefanyika Afrika Kusini. Itazame hapa, tupia maoni yako kisha SHARE na washikaji waone

CHRISTIAN BELLA- NASHINDWA
Baada ya Nani Kama Mama - Mzee wa masauti aka King of Melodies Christian Bella leo ameachia hii ngoma yake mpya iitwayo Nashindwa, na video yake imefanyika Afrika Kusini. Itazame hapa, tupia maoni yako kisha SHARE na washikaji waone
Posted by East Africa Television (EATV) on Wednesday, April 1, 2015
Watu wengi hujikuta wakiwa wanahangaika wataanzaje biashara bila kuwa na kiasi kikubwa cha pesa. Wakati huohuo, wengine wana pesa lakini hawana ujuzi wa msingi wa kuweza kupata zaidi ya kiasi walicho nacho.

Baadhi ya nilizoorodhesha hapa chini, ni biashara ambazo zinahitaji msingi (pesa) kidogo au hata bila pesa zinaweza kuanza kukuingizia kipato. Naamini wengine mnaweza kuongezea:

  1. Kuosha magari (Car Wash)
  2. Blogging
  3. Urembaji wa keki (Cake decorating)
  4. Utengenezaji mishumaa
  5. Mama Ntilie (Catering)
  6. Kutembeza vyakula maofisini (Mobile food vendor)
  7. Kazi ya usafi maofisini (kama mkiwa mmejikusanya kama kikundi)
  8. Computer troubleshooting (kwa graduates wa IT, Computer technicians)
  9. Event coordinator
  10. Kutumbuiza kwenye matukio kama DJ (Event DJing)
  11. Exercise/Sports instructor (wengi wanahitaji huduma hii)
  12. Utengenezaji wa fenicha
  13. Utunzaji wa bustani (Gardening, Landscaping etc)
  14. Usafishaji wa nyumba mtaani (House cleaning)
  15. Interior decorating (naona wengine hadi wanajiita 'interior designers')
  16. Kusaidia watu kubeba mizigo wakitoka kwenye manunuzi (Personal shopping assistant)
  17. Uuzaji wa nafaka/mazao toka kwa wakulima mikoani (wanahitaji kiunganishi na wateja wa mijini)
  18. Usahihishaji wa lugha/maandishi kwenye ofisi mbalimbali pamoja na vyombo vya habari (Proofreading)
  19. Kuwa MC kwenye matukio mbalimbali (Unatakiwa kusoma vitabu vya Public speaking zaidi)
  20. Kutengeneza sabuni (Soap making)
  21. Kufundisha (Teaching); hapa namaanisha kila mtu ana kitu anafahamu ambacho anaweza kuwa mwalimu mzuri
  22. Website design (kama ulisomea mambo ya graphics n.k)
  23. Software developer (kama umesomea software engineering n.k)
  24. Wedding planner/Event Cordinator

Natambua kuna watu waliosomea fani mbalimbali, tusaidiane kuwaelimisha wengine juu ya kutumia elimu zao bila kutegemea kipato kikubwa lakini baadae wakanufaika na elimu zao bila kusubiri kuajiriwa na serikali ama makampuni makubwa.
Akon

Mwanamuziki mwenye tuzo la kimataifa Akon amesema kuwa hakuna hata mwanamuziki mmoja wa Kenya ambaye amemuomba kufanya naye 'kolabo'mara zote tano ambazo ameweza kuzuru Kenya.
Akon Hatahivyo ameliambia jarida la Mondayblues nchini Kenya kwamba wasanii wa muziki barani Afrika pia wanafaa kuimarisha viwango vyao ili kutoa changomoto kwa wasanii kama yeye ili kuweza kushirikiana nao.
Tamko la msanii huyo linajiri kufuatia madai kutoka kwa wanamuziki wa Kenya kwamba hayuko tayari kufanya nao Kazi.
Chanzo:bbc swahili

Ndege za kijeshi za Kenya zimeshambulia maeneo ya wapiganaji wa kundi la Alshabaab katika taifa jirani la Somalia ,msemaji wa jeshi ameiambia BBC.
Ndege hizo zililenga maeneo mawili ya jimbo la Gedo,linalotumiwa na wapiganaji hao kuvuka na kuingia Kenya, msemaji huyo ameongeza.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na wapiganaji hao kupanga mshambulizi nchini Kenya.
Wanajeshi wa AMISOM walitarajiwa kupeleka wanajeshi wao katika eneo hilo la Gedo lakini hadi sasa hawajafanya hivyo.
Hili ni shambulio la kwanza la Kenya kwa shambulizi la alshabaab ambalo lilisababisha mauaji ya watu 148 katika chuo kikuu cha Garissa wiki iliopita.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameapa kujibu shambulizi hilo kwa njia mbaya zaidi.
Msemaji wa jeshi la Kenya David Obonyo ameiambia BBC kwamba Jeshi la Kenya lilijibu vitisho kwa kutekeleza mashambulizi ya angani siku ya jumapili usiku katika eneo hilo.
Hakuna maelezo zaidi ya oparesheni hiyo yaliotolewa.
Chanzo:bbc swahili

Willium Ruto

Serikali ya Kenya imeitetea idara yake ya usalama kufuatia shutma kwamba ilichelewa kukabiliana na shambulio la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 150 waliuawa.
Shambulio hilo lilisitishwa baada wapiganaji wanne waliohusika kuuawa na maafisa wa polisi saa 15 baada ya kuvamia chuo hicho.
Wanajeshi wa Kenya
Lakini naibu wa rais William Ruto anasema kuwa kundi la kwanza la polisi liliwasili katika chuo hicho saa moja baada ya shambulizi.
Amelipongeza jeshi la Kenya KDF kwa kile alichokitaja kua hatua za haraka.Lakini vyombo vya habari vimekuwa vikisema kuwa vikosi maalum vilivyowaua wapiganaji hao vilichelewa kufika katika eneo hilo kutokana na mfumo wa usafiri waliotumia.
Wanajeshi wa kenya
Pia kuna madai kwamba maafisa wa polisi walifeli kuchukua hatua za dharura baada ya kupewa habari kwamba mmoja ya wauaji ambaye sasa ametambuliwa kama Abdirahim Abdullahi ni wakili na mwana wa chifu mmoja katika eneo la kazkazini mashariki
Chanzo: bbc swahili

Mahmoud Abbas

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amekataa kukubali mamilioni ya dola ambazo ni fedha za kodi ambazo zilikuwa zimezuiliwa na Israeli.
Bwana Abbas alisema kuwa aliamua kurudisha pesa hizo kwa sababu Israeli ilikuwa imekata kiasi fulani ili kulipa kile ilichosema kuwa ni madeni kwa makampuni ya nchi yake.
Bwana Abbas alisema kuwa pesa zilizokatwa ni kama thuluthi moja ya pesa zote ambazo Israeli imekuwa ikizuia.
Amesema kuwa iwapo Israeli itakosa kulipa fedha zote hizo atapeleka kesi katika mahakama ya haki ya kimataifa ICC.
Chanzo:bbc swahili
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ