• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Monday, February 29, 2016

Marcus Rushford awa Man of the Match baada ya kuifunga Arsenal bao mbili hapo jana Manchester United ilishinda kwa bao 3-2
Huu ndio msimamo wa League kwa sasa

Kwa mahitaji ya CCTV CAMERA,DVR,POWER SUPPLY ZA CCTV CAMERA kwa ulinzi wa OFISI YAKO,NYUMBANI,NA BIASHARA YAKO unaweza kuwasiliana nasi Directly 0714 585867,0714 909008 au simu ya mezani 022 2668080 pia waweza fika ofisi zetu zilizopo Kinondoni Studio - Opposite Stereo Bar Dar es Salaam.Pia tunafanya Maintenance kwa ambao mlishafunga Kitambo.

Sunday, February 28, 2016

Staa wa muziki Diamond Platnumz amejipanga kuachia wimbo mpya wa kurap uitwao Simba.
Akizungumza katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, Meneja wa msanii huyo, Babu Tale alisema wimbo huo utakuwa sio wa biashara bali ni zawadi kwa mashabiki.

“Kama Hip Hop ni biashara Diamond amefanya wimbo wa kurap lakini hatujauchulia kama ile ni biashara, wimbo umeshaisha na unaitwa Simba,” alisema Babu Tale.
Diamond kwa sasa anafanya poa na video ya wimbo ‘Make Me Sing’ akiwa na AKA wa Afrika Kusini.

Saturday, February 27, 2016

Baada ya Nay wa Mitego kuwachana wasanii kibao akiwemo Dj.Choka,Shetta, na wengine kibao katika nyimbo yake ya SHIKA ADABU YAKO msanii Kimbunga Mchawi amjibu kwa Single hii NIMCHANE huku akimchana Ney kuwa ameishiwa mashairi na kuamua kuwachana wasanii wenzake kwa Kejeli.

Sikiliza hapa kutoka katika Link hii.

Friday, February 26, 2016


Thursday, February 25, 2016

Official Video ya msanii SULTAN KING. Wimbo unaitwa SHIKILIA, audio imetengenezwa ISLAND RECORD Producer ni ALONEYM. Video imefanywa na KWETU STUDIOS, Directed by Msafiri Shabani.

Video Directed by Pablo
Instagram; Yamoto_band
Facebook; Official Yamoto Band
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali jana jioni.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari dogo kugonga gari alilokuwa akisafiria katika eneo la Kiwira jijini Mbeya.


Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson amenusurika kifo baada ya gari alilokuwa akisafiria kupata ajali jana jioni.

Taarifa za awali zimeeleza kuwa Dk. Tulia alipata ajali hiyo baada ya gari dogo kugonga gari alilokuwa akisafiria katika eneo la Kiwira jijini Mbeya.



Darassa Ft Rich Mavoco 
titled "Kama Utanipenda"
Video Directed by Hanscana
Wanene Films 2016

KILIO cha ukosefu wa fedha za kuonesha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge la Tanzania kupitia Shirika la Utangazaji nchini (TBC) ambacho kimekuwa kikitolewa na serikali, sasa kimepata ufumbuzi.

Mfuko wa Vyombo vya Habari nchini (TMF) umeeleza kwamba upo tayari kutoa fedha zinazohitajika ili kuhakikisha haki ya Mtanzania kupata habari kupitia TBC haiingiliwi wala kubughudhiwa kwa hoja yoyote.

Endapo serikali itakubali ombo hilo, wananchi wataendelea kunufaika na vikao vya moja kwa moja vya bunge tofauti na pendekezo la serikali la kunakili baadhi ya sehemu na kisha kuoneshwa usiku.

Ernest Sungura, Mkurugenzi Mtendaji wa TMF leo jijini Dar es Salaam amewaeleza wahariri wa habari na serikali kupitia mwakilishi wake Assah Mwambene ambaye ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo kwamba, taasisi hiyo imejipanga kusimamia na kuhakikisha Watanzania wanaendelea kupata matangazo ya moja kwa moja kutoka bungeni kupitia TBC kwa kuyagharamia.

Sungura amesema kwamba miongoni mwa malengo ya mfuko huo ni pamoja na kuleta mabadiliko katika tasnia ya habari pia kuhakikisha wananchi wanapata taarifa.

Januari mwaka huu, Nape Nnauye, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alitoa ufafanuzi bungeni kuhusu hatua ya serikali kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kupitia TBC.

Miongoni mwa sababu alizozieleza ni pamoja na kuwepo kwa gharama kubwa ya Sh. 4.2 bilioni zinazotumika katika uendeshaji wa matangazo hayo ya moja kwa moja kwa mwaka pia watumishi wa serikali kushabikia bunge badala ya kuendelea na kazi ofisini.

Hatua ya serikali kusitisha matangazo hayo iliibua mjadala mkubwa bungeni huku Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) akilitaka bunge kusitisha shughuli zake ili kujadili taarifa hiyo ya serikali.

Nje ya bunge mjadala huo uliendelea bila kupatikana kwa ufumbuzi ambapo TMF imedhamiria kugharamia matangazo hayo ili kuruhusu wananchi kuendelea kupata matangazo hayo kupitia TBC.

Katika mkutano huo, Mwambene amesema kwamba, serikali itafikiria namna ya kupeleka maombi TMF ya uwezeshwaji katika maandalizi ya miswada miwili ya sheria za habari ili kupitisha sheria zenye matakwa ya wadau.

Kuhusu hilo, Sungura amesema taasisi yake iko tayari kuisaidia serikali kwenye mchakato huo na hata kuitisha kongamano kubwa la wadau.
Usaili wa kazi ni hatua muhimu kwa kila mwenye ndoto ya kuajiriwa na kupata kazi ya ndoto yake. Lakini ni hatua yenye vikwazo vidogo vinavyogeuka kuwa mlima wa kikwazo pale ambapo msailiwa ataruka hatua hizi nne muhimu katika maandalizi yake.
Kutofahamu mambo haya muhimu kabla ya kuingia kwenye usaili, huwafanya wasailiwa wengi kujikuta wakijuta kuingia kwenye usaili husika au kufikiri kuwa hawana bahati ya kupata kazi wanayoitamani kwa kuwa wamejibu vizuri maswali mengi waliyoulizwa.
Lakini maswali unapaswa kufahamu kuwa mambo haya manne yatakupa asilimia zaidi ya 80 ya ushindi kwenye maswali yoyote utakayoulizwa na wasaili. Hata kama maswali utakayoulizwa unayafahamu vilivyo, lakini kushindwa kuyaunganisha na mambo haya kutakuangusha vibaya na huenda ukambilia kudhani ulinyimwa kazi kwa makusudi.
Fahamu vizuri Kampuni/shirika husika
Hii ni hatua ya kwanza na muhimu sana katika ushindi wa usaili husika. Karibu kila swali utakaloulizwa litakuwa na uhusiano na hili.
Hivyo, unapaswa kufahamu vizuri kazi na huduma au bidhaa zinazotolewa na shirika husika,  dhima na dira na lengo kuu la kampuni/shirika hilo. Unapaswa pia kuhakikisha unafahamu washindani wa kampuni husika hususan kama inafanya biashara yoyote.

Tambua Udhaifu, Uimara, Fursa na Hatari/vitisho ambavyo kampuni husika inakutana navyo. Ni rahisi kufahamu mambo hayo endapo utatumia muda wako kufanya utafiti wenye mantiki kuhusu kampuni husika. Taarifa hizi zote unaweza kuzipata kwa kusoma tovuti ya kampuni husika pamoja na machapisho yao mbalimbali.
Hii itakuongezea hali ya kujiamini kwa kuwa unamfahamu vizuri mwajiri wako.
Fahamu kiundani majukumu yote ya nafasi unayowania
Hapa simaanishi tu kukariri majukumu uliyoandikiwa kwenye tangazo la nafasi ya kazi, bali kufahamu kwa kina kinachotegemewa kutoka kwako.
Muajiri wako anatarajia mtu atakayemuajiri awe anajitambua vizuri na amejiandaa kuyakabiri majukumu yake. Anatarajia kuona nia na uwezo wa mtu anayemhitaji kwenye usaili husika.
Ukiyafahamu vizuri majukumu yako na mipaka yake, utakuwa na uwanja mpana wa kujibu maswali yako kwa kumshawishi muajiri kuwa majumu husika unaweza kuyakabili kwa ufanisi zaidi. Kila swali litakaloelekezwa kwako, lijibu ukiwa na picha ya majukumu yako pamoja na kampuni yako.
Kwanini unahitaji kazi hiyo na kwanini unadhani wewe ndiye mhusika 
Mwajiri anahitaji sana mtu anayejielewa kama nilivyosema awali, ‘self determined and focused’. Unapaswa kujiuliza vizuri kwanini unahitaji kazi husika, huku ukilizingatia pia swali kuwa unadhani kwanini wewe ndiye mtu unayefaa zaidi kuliko wote.
Kama hufahamu kwanini unahitaji nafasi hiyo, sio kwa sababu unahitaji pesa, hilo linajulikana na ni vyema usiligusie kabisa. Zungumzia upande wa pili wa ‘Career’ yako hasa na unavyotaka kuleta mabadiliko kwenye kazi husika. Ni muda mzuri wa kujinadi.
Ifahamu vizuri, imeze CV yako
Curriculum Vitae (CV), ni maandishi yanayokueleza wewe ulivyo na uhusiano wako na kazi husika. Isome vizuri CV yako baada ya kuandika mambo muhimu unayopaswa kuyaandika. Tutaelezea siku moja kipi hakipaswi kuwekwa lakini huwekwa na wengi.
Usiiache nukta iliyo kwenye CV yako ikupite bila kuielewa vizuri. Isome tena na tena na uelewe kwanini umeandika yote uliyoandika na namna ya kuyaelezea.
Kumbuka katika usaili, CV yako inaweza kuzaa maswali mengi na ikakuinua au kukuangusha. Kumbuka ku-update CV yako kila unapotaka kazi fulani, usiitupe tu kwa kazi yoyote, mengine yanaweza kuwa yanakuinua kwenye kazi A, lakini  yakawa chanzo cha kukukoseha kazi B.
Screenshot_2016-02-19-15-41-37-1[1]
Hivi karibuni ilisambaa voice note ya msanii Dogo Janja akiliilalamikia menejimenti yake ya Tip top kuwa inataka kumshusha kimuziki kwa sababu alizosema wanashindwa kumtoa wakati nyimbo tayari karekodi tena nyingi tu.
‘’Tukisema tuendelee kuhoji tayari tushakuwa tushapata hasara kwa sababu tumeshalipia audio,video tumeshafanya kila kitu kipo tayari ila kauli yake imewapa watu ‘shock’ ndio maana nasema kauli yangu peke yangu nashindwa kuamua,nitajaribu kukaa na Babu Tale na uongozi kwa ujumla lakini pia lazima turudi upande wake tujue alikuwa akitamka maneno yale sehemu gani na alikuwa akitaka nini’’Madee.
Ngoma mpya ya Dogo Janja inatarajia kutoka kesho

Ray C ameweka wazi kuwa yuko taabani kiuchumi, hali inayompelekea kukosa hata pesa ya usafiri wa kwenda hospitali kupata dozi ya tiba ya maradhi yanayomkabili kutokana na kuathirika na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea na Planet Bongo ya EATV hivi karibuni, Ray C alieleza kilio chake akidai kuwa sio tu kwamba amekosa pesa ya kuendelea kusapoti muziki wake baada ya aliyeahidi kumsaidia kumkimbia, bali inamlazimu kupanda daladala akiwa ndani ya vazi la ‘ninja’ kutokana na kushindwa gharama za usafiri.

“Jamani kiukweli haya maisha ya wasanii nyie acheni tu, yaani inabidi tumuombe tu mungu, mtu akikuona msanii kwenye daladala nani atanunua albamu yako, nani atakuja kwenye show yako, lakini mama ananiambia vaa ninja mwanangu nenda kapate tiba.  Kwa sababu kila siku kukodi taxi ni gharama sana, kutoa elfu 25,000 kutoka Bunju mpaka hospitali kila siku ni nyingi sana," alieleza.

“Sometimes namwambia mama inabidi tutoke mapema saa 11 hivi nivae ninja twende kwanza kanisani then naweza nikachukua hata bajaji kwenda hospitali. Haya ni maisha sio kitu cha kucheka ni lazima nifanye hivyo ili niweze kumaliza dozi,” aliongeza.

Ray C alieleza kusikitishwa na namna ambavyo baadhi ya magazeti yanamuandika na kumchafulia jina kwa kile alichodai ni habari za kutungwa kuwa amerudia dawa za kulevya, badala ya kuandika habari njema zinazomhusu.

Mwimbaji huyo ambaye album yake imekwama studio, aliwaomba wadau na wananchi kwa ujumla kumsaidia hata kwa kumchangia kiasi kidogokidogo cha fedha ili aweze kumudu gharama za maisha na hata kurejea jukwaani.

WAZIRI MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wakurugenzi wa vitengo na wakuu wa taasisi katika Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) wapate nakala ya hansard ya hotuba ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuzindua Bunge la 11, waisome na kufanyia kazi maeneo yote aliyoyaainisha.

“Katibu Mkuu hakikisha umepata hansard ya hotuba ya Mheshimiwa Rais wakati akizindua Bunge na uhakikishe kila mkurugenzi ana nakala na kila mmoja wenu lazima ahakikishe anafanyia maeneo ambayo Mheshimiwa Rais ameyaainisha. Ni lazima tuelewane ni nini tunapaswa tufanye,” alisema.

Ametoa kauli hiyo jana (JANA) mchana (Jumanne, Novemba 24, 2015) wakati akizungumza na wakuu wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) kwenye mkutano uliofanyika ofisi ndogo ya TAMISEMI, barabara ya Kivukoni, jijini Dar es Salaam.

“Ninatamani kuona mabadiliko ya utendaji kazi Serikalini katika kipindi kifupi. Natamani kila mmoja asiridhike na uzembe unaofanywa huku chini. Ni nyote ni wataalamu, kwa hiyo mnapaswa kudhirisha elimu yenu na ujuzi mlionao,” aliwasisitizia Wakurugenzi hao.

Alisema kila mkurugenzi na mkuu wa taasisi anapaswa kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa kazi kwenye sekta yake kwani hilo litasaidia kukidhi matarajio ya Watanzania ya kuona mabadiliko ya utendaji kazi kwenye Serikali ya Awamu ya Tano. 
  
“Ninyi wakurugenzi siyo desk officers bali ni field officers. Nataka muweke utaratibu wa kwenda vijijini mkasimamie watu wenu, pia mhimize uadilifu, uaminifu na weledi wa kazi,” alisisitiza.

“Mambo ninayotaka mhimize watendaji waliopo chini yenu ni pamoja na haya yafuatayo: muda wa kuripoti kazini uzingatiwe, muda wa kukaa kazini uzingatiwe, utokaji kazini kwenda kwenye chai na chakula cha mchana udhibitiwe, na mipango na malengo ya kazi kwa siku ni lazima yafikiwe,” alisema.

“Tunataka kujua mtumishi amefanya nini tangu alipoingia ofisini. Suala siyo kukaa tu ofisini, kwani kuna mtu anakaa ofisini, hajaenda hata kunywa chai lakini ukiuliza amefanya nini hupati jibu la kueleweka. Sisi kama vongozi wao ni lazima tujue wanafanya kazi gani wanapokuwa maofisini,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa ameitisha kikao ofisini kwake kesho (LEO )saa 4 asubuhi akitaka kupatiwa taarifa ni kwa nini mradi wa mabasi yaendayo kasi (DART) haujaanza kazi hadi sasa.
  
 “Kesho( LEO)  saa 4 asubuhi Katibu Mkuu, Mkurugenzi Mkuu DART na watendaji wako mje ofisini. Nataka kupata maelezo ni kwa nini mabasi hayajaanza kazi hadi leo, je ni lini yataanza kazi, je ni nani anakwamisha. Na hata kama ni sheria, ni kwa nini tusiziharmonise ili kuondoa hivyo vikwazo,?” alihoji Waziri Mkuu.

“Ninataka kupata haya maelezo kwa sababu Watanzania na hasa wana-Dar es salaam, wamesubiri kwa muda kuona mradi ukianza kazi ili uondoe kero ya usafiri. Wao wanajua anayehusika ni TAMISEMI,”aliongeza.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na watumishi na viongozi wa TAMISEMI, Katibu Mkuu wa OWM-TAMISEMI, Bw. Jumanne Sagini alimweleza baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo wizara hiyo imekabiliana nazo katika utendaji wake wa kazi.

Kuhusu ujenzi wa vyumba vya maabara kwa ajili ya kuimarisha ufundishaji wa masomo ya sayansi, Bw. Sagini alisema vyumba hivyo vimeongezeka kutoka 247 mwaka 2005/2006 na kufikia 6,161 mwaka 2014/2015. Pia alisema vyumba 4,228 viko kwenye hatua za kukamilika ujenzi wake.

Kuhusu utengaji wa madirisha ya kuhudumia makundi yenye msamaha kama wazee na watu wenye ulemavu hospitalini na kwenye vituo vya afya, Katibu Mkuu alisema nayo yameongezeka kutoka madirisha 5,074 mwaka 2010 na kufikia 7,903 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 55.

Msikilize waziri hapa!!

Kile kiwanda kikubwa cha Africa mashariki na Africa kwa ujumla kwa mara ya kwanza kimeanza kuzalisha kusambaza cement  tarehe 21/02/ 2016.

Kiwanda hicho ambacho ni tegemeo jipya kwa wakazi wa mikoa kusini Mtwara na Lindi kiliahidi ajira nyingi ya wakaanzi wa mikoa hiyo na watanzania kwa ujumla
Cement tayari iko maduka kwa bei nafuu ya sh 13,500 tofauti na cement ya viwanda vingine.

Tunawakaribisha wateja wa cement hiyo na wenye magari makubwa kufungua office mkoani Mtwara ili kuongeza ajira za madereva hapa mkoani.

 
 
Mgombea  urais wa Chama cha Republican, Donald Trump ameshinda katika Jimbo la Nevada nchini Marekani, na kuzidi kuimarisha uongozi wake katika mchujo wa kuwania tiketi ya chama hicho.

Tajiri huyo aliyewahi  kutamka  hadharani  kuwa atawafunga  jela  Rais  Mugabe  na Mseveni, sasa ameshinda mara tatu, kufuatia ushindi wake katika Jimbo la New Hampshire na Carolina Kusini.

Seneta Marco Rubio na Ted Cruz ambao wamekuwa wakishambuliana wiki hii wanapigania nafasi ya pili.

Maofisa wa chama hicho wamesema wanachunguza  ripoti za watu kupiga kura mara mbili huku eneo moja likidaiwa kuwa na vifaa vichache vya kupigia kura.


Baadhi ya wapiga kura  pia walidaiwa kuvaa nguo zenye picha za Trump, lakini maofisa wamesema kuwa hatua hiyo siyo kinyume na sheria

 

MKALI wa Bongo Fleva, ambaye wimbo wake wa ‘Shika Adabu Yako’ umefungiwa na Baraza la Sanaa Nchini (Basata), Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’, ameibuka na kudai kwamba ameamua kuchukua R/B kituo kidogo cha polisi ili kuwadhibiti watu anaodai wanamfuatilia kwa nia ya kumtendea mabaya.

“Kiukweli sina ugomvi na mtu na hii ni dunia haina siri, kama kuna mtu ananifanyia hivyo vitu basi itajulikana maana mimi nimeimba kama wimbo mwingine na sina ugonvi nao, sasa kama wananitafuta nitawatafuta kwa R/B,” alieleza.

Aliongeza kwamba, kwa sasa mtoto wake wa kike amefanyiwa upasuaji wa uvimbe katika koo na maendeleo yake ni mazuri, huku akisisitiza kwamba Ijumaa ya wiki hii atatoa video ya wimbo wake huo.
“Mwanangu alikuwa anaumwa lakini kwa sasa nashukuru Mungu hajambo na wiki hii nitatoa video ya wimbo wangu, mtaona tofauti na mnavyofikiria tofauti katika wimbo wenyewe,’’ alimaliza

http://www.habarileo.co.tz/images/Frequent/makontena.jpg


WADAIWA 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.
Mkurugenzi wa Mtendaji wa Kampuni ya Udalali ya Yono, iliyopewa kazi ya kufuatilia wadaiwa hao wakiwemo baadhi ambao wamekamilisha malipo, Yono Kevella alisema hayo Dar es Salaam jana.
Akizungumza na gazeti hili, Kevela alisema kuanzia leo wanakaa na vyombo vya dola, kuanza utaratibu wa kukamata na kufilisi mali za wahusika na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Kevela alisema hadi sasa hakuna zuio lililotolewa, linazowazuia kutekeleza wajibu wao katika kukusanya madeni hayo. Hata hivyo alisema, wengi wa wadaiwa baada ya kutolewa kwa muda huo wa siku 14, wameonesha moyo wa kulipa.
Wadaiwa 16 hawajamaliza madeni Alitaja wadaiwa 16 ambao hawajalipa madeni yao wala kupunguza, ambao watafilisiwa wasipojitokeza kufanya malipo ni Said Ahmed Said Sh 28,249,352.50, Strauss International (45,393,769.95), Farid Abdallah Salum (52,185, 614.97).
Wengine ni Nasir Saleh Mazrui (60,105,873.77), Simbo Yona Kimaro (64,221,009.10), Ally Masoud Dama (102,586,719.22) na Juma Kassem Abdul (130,182,395.12), Salum Link Tyres (233,447,913.31) na Tybat Trading Co.Ltd (448,690,271.90).
Pia wamo IPS Roofing Co.Ltd (966,723,692.10), Tuff Tyres General Co Ltd, (7,435,254,537.03), Swalehe Mohamed Swalehe (34,687,165.00), Rushwheel Tyre General Co Ltd, (1,802,988,679.20), Said Ahmad Hamdan (68,362,558.31), Ahmed Saleh Tawred ( 59,237,578.40) na Farida Abdullah Salem Sh 75,334,871. 85.
Akizungumzia wadaiwa waliolipa ndani ya siku 14 walizopewa na zikaisha juzi, alisema wanane kati ya 24, ndiyo walijitokeza kulipa madeni baada ya kampuni yake kuwafuatilia.
Kevela alisema hadi jana zaidi ya Sh milioni 200 zimelipwa na wadaiwa hao.
Wadaiwa hao 24 walishindwa kulipa kodi kwa wakati kama walivyotakiwa kufanya, ndipo TRA ilimpa dalali huyo kazi ya kuwafilisi. Kampuni hiyo ya udalali ilitoa siku 14, kuanzia Februari 10, mwaka huu wawe wamekamilisha; muda ambao umeisha juzi.
Kevela alisema katika siku hizo 14, kati waliojitokeza kulipa,wanne kati yao wamemaliza madeni na wengine wanne wamepunguza madeni na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki. Waliomaliza madeni yao Wadaiwa waliolipa madeni yao yote ni Issa Ali Salim aliyekuwa akidaiwa Sh 94,543,161.96, Libas Fashion (26,593,245.78), Omary Hussein Badawy (21,346,615.40) na Zulea Abas Ali (16,760577.24).
Waliopunguza madeni yao Waliopunguza madeni yao ni Zuleha Abbas Alli aliyelipa Sh milioni 47 na kubakiwa na deni la Sh 28,508,551, awali alikuwa akidaiwa Sh 75,508,551.88, mwingine ni Ally Awes Hamdani aliyelipa Sh milioni 17.26 awali alikuwa akidaiwa Sh 55,485,904.07).
Wengine waliopunguza kidogo ni Tifo Global Trading Co Ltd waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 1,573,300,644.58, Lotai Steel Tanzania Ltd, waliolipa Sh milioni mbili ilhali deni lao ni Sh 5,476,475,738.19.
“Tulikabidhiwa wadaiwa 24 na TRA, waliokwepa kodi kwa kutorosha kontena katika bandari kavu ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, sasa walipewa muda wa kulipa ila walikaidi, tukakabidhiwa tuwafilisi mali zao zote ili kulipia madeni na wamejitokeza hao na kuanza kulipa wengine wamemaliza”, alisema Kevela.
Awali wadaiwa 24, walikwepa kodi ya Sh bilioni 18.95 kwa kutorosha makontena 329 ya bidhaa zao kutoka Kampuni ya SSB ambayo ndiyo mmiliki wa bandari kavu ya (Azam ICD) na kampuni ya Regional Cargo Services.
Mapema Desemba mwaka jana aliyekuwa Kaimu Kamishna wa TRA, Dk Philip Mpango alizungumza na waandishi wa habari na kusema kampuni 15 kati ya 43, zilizokwepa kodi baada ya kutorosha kontena 329 katika ICD ya Azam, wamelipa.
Dk Mpango alisema Desemba 12, mwaka jana ndiyo ilikuwa siku ya mwisho aliyotoa Rais John Magufuli ya siku saba kwa wakwepa kodi hao 43, kulipa wenyewe kwa hiari, vinginevyo sheria zitachukua mkondo wake. Kufuatia kauli hiyo ya Rais Magufuli, wadaiwa 15 walijitokeza na kulipa na waliobaki hawakujitokeza kulipa


Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpigapicha wa gazeti la Mwananchi aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha.

Wasira, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa Serikali ya Awamu ya Nne (SA4), alifanya kitendo hicho akitoka kwenye jengo la Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupwa na Mahakama Kuu.

Katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Wasira, ambaye amekuwa mbunge wa Mwibara tangu mwaka 1970 na baadaye mbunge wa Bunda hadi mwaka 2015, aliangushwa na Ester Bulaya wa Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari akiwamo walishuhudia tukio hilo.

“Wasira alimkimbiza Jamson akitaka kumnyang’anya kamera, lakini hakuweza,” alisema Nyange,mwandishi  wa  gazeti  la  Mtanzania.

“Baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.”

Akisimulia tukio hilo, Jamson alisema Wasira, ambaye amefanya kazi na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na kitendo chake cha kumpiga picha.

“Wasira alinifuata na kuniuliza sababu za kumfuatilia kila mara. Aliniuliza picha nazopiga nazipeleka wapi,” alisema Jamson.

“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako.Hivi mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira

Jitihada za Wasira kumnasa Jamson ziliendelea hadi nje ya eneo la mahakama ambako alimfuata kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser (namba tunazihifadhi).

Katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa barabara.

Juhudi za kumpata Wasira kuzungumzia sababu za kutaka kumshambulia mpiga picha huyo kwa kuchukua picha za tukio hilo, hazikuzaa matunda.

Awali, Jaji Sirilius Matupa alitupilia mbali maombi ya ruhusa ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kufuta shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa Bunda baada ya kubaini waliowasilisha maombi hayo, Magambo Masato na wenzake wanne, hawakufuata sheria.

Uamuzi huo ulisomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Eugenia Rujwahuka kwa niaba ya Jaji Matupa.

Katika maombi yao ya msingi, Magambo Masato na wenzake waliiomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi Bulaya wakidai licha ya Wasira kunyimwa haki kuhakiki na kuhesabu upya kura, mchakato wa uchaguzi huo pia uligubikwa na vitendo vya rushwa.

Akisoma maamuzi hayo kwa niaba ya Jaji Sirilius Matupa, Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Eugenia Rujwahuka alisema maombi hayo yamewasilishwa kwa kutumia kifungu cha sheria kisichohusika.

“Badala ya kuwasilisha maombi yao kwa kutumia kifungu cha 15 (c) cha Sheria ya Uchaguzi Sura namba 141, waleta maombi wametumia kifungu cha 15 (a) (b),” alisema Rujwahuka akimnukuu Jaji Matupa.

Wakati huohuo, shauri la kupinga matokeo ya uchaguzi wa jimbo la Nyamagana, iliyofunguliwa Ezekiah Wenje, imesikilizwa jana na kuahirishwa hadi Februari 29, mwaka huu.

Akiahirisha shauri hiyo iliyoahirishwa mara mbili mfululizo Jumatatu na Jumanne iliyopita, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga, Kakusulo Sambo aliziagiza pande zinazohusika kuhakikisha zinakamilisha taratibu zote za kisheria ili shauri hilo lianze kusikilizwa mfululizo.

‘Lupela’ is Alikiba's smash hit release through his global ambassadorship and partnership with WildAid and his worldwide exclusive partnership with his record label and management company 'ROCKSTAR4000' and publishing partnership with 'Rockstar Publishing', and the music video directed by Kevin Donovan
Tanzania  imedhihirisha kuwa ni tajiri mkubwa wa rasilimali ya gesi asilia baada ya kugundulika kwa gesi nyingine katika bonde la mto Ruvu yenye ukubwa wa ujazo wa futi trilioni 2.17.

Ugunduzi huo wa gesi asilia umefanywa na Kampuni ya Dodsal Hydrocarbons and Power Tanzania Limited ambayo imekuwa inafanya shughuli za utafutaji wa gesi na mafuta katika Mkoa wa Pwani.

Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Pilavullathil Surendran alisema jana katika mkutano wa wawekezaji wa gesi na mafuta ulioandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuwa, thamani ya gesi iliyoko katika eneo hilo inafikia Dola za Marekani bilioni sita sawa na Sh trilioni 12.

Ugunduzi huo mpya unafanya hadi sasa Tanzania kuwa na amana ya gesi yenye ukubwa wa futi za ujazo trilioni 57.27.

Kwa upande wake, Profesa Muhongo alithibitisha kugundulika kwa gesi hiyo tangu Julai mwaka jana, lakini akaeleza kuwa Serikali imechelewa kutangaza ugunduzi huo kama inavyoagizwa na Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 kutokana na shughuli za uchaguzi.

“Sheria mpya inatutaka kabla ya waziri mwenye dhamana ya gesi kutangaza ugunduzi mpya wa gesi na mafuta ni lazima athibitishiwe na mamlaka ya udhibiti wa bidhaa za Petroli na Gesi (PURA).

“Wizara yangu itawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kupata ushauri wa kisheria kuhusu jambo hilo na bahati nzuri tayari PURA imeshaanza kushughulikia jambo hilo na naamini kuwa nitatangaza ugunduzi huo mpya hivi karibuni,” alifafanua Profesa Muhongo.

Licha ya ugunduzi huo mpya tayari gesi imegundulika katika maeneo ya kisiwa cha Songo Songo mkoani Lindi na eneo la Mnazi Bay huko Mtwara na katika Wilaya ya Mkuranga, Pwani pia kumegundulika kiasi kikubwa cha gesi.

Tuesday, February 23, 2016

I don't have any familial or genealogical history from any part of the Caribbean, so at times I have to resort to various lyrics websites to totally understand what Rihanna is saying in her new single "Work." The one thing I do know about people from the Caribbean: they throw some of the best parties in the world. Go to Carnival in either Jamaica or Trinidad & Tobago for proof.
If you can't afford to do that? Simply go to a bashment party, such as the one on full display in the visual treatment for Rih's ANTI single. Filmed by Director X (what's funny? I suggested that the sneak peeks of the video reminded me of Sean Paul's "Get Busy," and it turns out that the two videos are directed by the same guy), the clip - which is actually two videos in one - takes place in Toronto (same as Sean Paul's!), in the basement level of a well-known restaurant The Real Jerk (those prices are about to go sky-high now). The whole thing is a dynamic clash of colors, hot and heavy dutty wines, and a proud display of the Caribbean culture. Not to mention...
Look at the stress on Aubrey's face.
rihanna-work-drake-video-2
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ