• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Thursday, March 31, 2016

King Kaka pours his heart out as he speaks about his relationship with his late father and now that he is a father of 2 daughters. a celebration soundtrack to all fathers. 


Wednesday, March 30, 2016

"Chukua muda wako wa kufikiri na kutafakari,na wakati ukifika fanya ulilopanga"

Hili ni somo kubwa kukumbuka wakati tuko katika vita ya nafsi yako wenyewe; wakati tunajua nini tunapaswa kufanya lakini tunashindwa kufanya.

Labda tunaliweka mbali kwa saa. Labda kwa siku. Na inaweza hata kuwa wiki . Lakini hatukufanya kwa wakati.

Kusitasita kunaweza kuwa ndio nyenzo kubwa inayokumaliza na kukukandamiza.ingawa kuna watu walioweza kuishinda nafsi yao ya kusita na kufanya mambo yakafanikiwa na kuwa mazuri.Je walifanikiwa kivipi?

Hizi ndizo Nguzo Tano(5) ambazo wengi waliofanikiwa huzitumia.

1.Wanatambua thamani ya Muda wao waliochelewa.
    Wengi hudhani katika kila wafanyalo wanataka lilete  matokeo ya papo kwa papo jambo ambalo si kweli.

    Wengi waliofanikiwa hufurahia matunda yao na huweza kufanya jambo ambalo hutumia mudawao mwingi kulijua na     kulifanya kwa uhakika.Hufanya kazi inayoonekana ni kubwa kwa Tathmini na baadae kuonekana kuwa Ndogo          kimuonekano ambapo hufurahia mafanikio hayo mapema na mara kwa mara.”Mafanikio huja kwa kufanya,na sio          Matokeo”

Anza kujipongeza kwa Uvumilivu.Furahia mafanikio yako kwa Uvumilivu wa kila ufanyalo.Itakusaidia kupunguza mambo mengi uliopanga kuyafanya na kufanya kila jambo kwa wakati.

 2.Hujali zaidi Muda wao wa kila siku. 
Unadhani shughuli itakuchukua masaa matatu kukamilika,lakini huna mpangilio wa swala hilo kulimaliza kwa masaa hayo matatu.Unataka kuliacha hadi hapo baadae utakapokuwa na muda wa ziada.

Wakati shughuli hiyo isingekuchukua masaa matatu bali Saa moja na nusu tu.Watu makini huanza katika muda walionao na huendelea mpaka hapo wanapofanikisha.
Huogopa kuangukia katika kundi la watu wavivu,ingawaje inaweza kuwachukua muda wao wote kufanya wafanyalo na kulijua vizuri,huchukua muda wao wanaokuwa nao hata muda wa baadae katika swala moja hata watakapolifanikisha.Na hilo ndilo lengo lao.

3.Hufanya katika umakini wa hali ya juu na kwa ufanisi mkubwa.
Ni kweli ufanisi na umakini kwa kila tulifanyalo huleta matunda mazuri.watu ambao hufanya tufanye kazi kwa ufanisi mkubwa na umakini ni MARAFIKI WAZURI na sio tu MARAFIKI.Umakini hukaa katika mawazo yako na kukufanya ujione unalofanya sio kwamba linakutosheleza bali utataka kufanya zaidi navizuri.Utakufanya kila ufanyalo kuonekana gumu zaidi ya linavyotakiwa kufanywa ili lifanikiwe.
Acha kuwa mpinzani wa nafsi yako.Hutakiwi kufanya kazi mbaya usiyoipenda,ili kuzuia hili jipe moyo kwa kila ufanyalo na kuamini litafanikiwa.

4.Ni wazuri na makini katika kupangilia.
Je unadharau kidogo na kutaka makubwa?Hili ni jaribu kubwa,kwasababu linakupa ujasiri wa kutaka kufanya makubwa na mengi wakati mudawako haujafika.Acha kuwa na mpangilio wa kufanya mambo mengi kwa wakati mchache.
Ingawa kwa watu Makini huwa tofauti,
Watu makini hupendelea kulichukua Jambo kubwa na Gumu,Jambo Muhimu huanza kwanza katika kila Mambo yao.

5.Hawajipingi wenyewe,wala kujikatisha Tamaa.
Mambo mengi ambayo wengi hujiuliza ni kwamba,Itakuwaje wakishindwa baada ya kujaribu kufanya jambo fulani au shughuli fulani,Je Bosi wake atamchukia?Itakuwaje ikimchukua mudawake wote katika kufanya Jambo moja?
Watu makini huondoa uoga wa kufanya jambo gumu  na uoga wa  kushindwa pia kama “Roger Babson” alivyosema “Keep in mind that neither success nor failure is ever final.”
Usiweke uoga wako wa kushindwa kwa mambo au shughuli ulizopanga kufanya,zaidi zaidi tilia mkazo na utafanikiwa.

Tuesday, March 29, 2016

Niger Delta 1
Indigenes of Olomu Kingdom in Ughelli South area of Delta State have reasons to celebrate their revered monarch, HRM Ovie Richard Layeguen Ogbon Ogoni-Oghoro I JP, the Ohworode of Olomu Kingdom.
Interestingly, the Ohworode, the oldest educated monarch in Delta state, who turned 99 years in January is so blessed that he still reads without glasses, walks unaided and displays the strength of a horse.
The monarch in company of his immediate family recently caused a stir when he drove himself in a black Lexus jeep to St. Andrew’s Anglican Church, Ogoni-Olomu for a special thanksgiving service.
Secret of longevity
Acknowledging God as the secret behind his longevity, the monarch urged all Nigerians, especially Urhobos to turn to God in solving her problems stressing that no human effort can permanently eradicate the problems plaguing the country.
According to him, “God has been magnanimous to us as a people, yet we are crawling and sleeping. Am urging every one of us to learn how to give our hearts and soul to God as this is the only way we can succeed in life.” Speaking on the secret of his longevity, the monarch said: “God is the secret of my longevity and that is why at my age, I can still drive.”
“Nigerian Afrobeats artiste Runtown presents the official music video for his song “Lagos to Kampala” featuring Wizkid.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefika nyumbani kwake katika kijiji cha Mlimani, Wilaya ya Chato Mkoani Geita kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais, ambapo akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Chato, ametoa wito kwa kila mtanzania kuchapa kazi kwa juhudi ili nchi iondokane na utegemezi wa misaada ya wafadhili ambayo huambatana na masharti.

Dkt. Magufuli amesema jukumu kubwa lililo mbele ya watanzania kwa sasa, ni kushikamana na kujisimamia katika maendeleo ili kila mmoja ahakikishe anaongeza uzalishaji na utendaji kazi mahali pake pa kazi.

"Kwa hiyo ni lazima tujisimamie sisi wenyewe, na tukijisimama sisi wenyewe kwa kila mmoja kuwajibika mahali alipo, kama ni mfanyakazi afanye kazi kwelikweli, kama ni mkulima afanye ukulima wake kwelikweli, kama ni mfanyabiashara afanye biashara kwelikweli, kama ni mfugaji afuge kwelikweli, kama ni mvuvi avue kwelikweli, Tanzania hii tutavuka" Amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema serikali yake imeamua kuchukua hatua kudhibiti nidhamu serikalini, kwa kuhakikisha inawachukulia hatua watumishi wa umma wanaolisababishia taifa upotevu mkubwa wa fedha, na ameahidi kuwa hatua hizo maarufu kwa jina la "Kutumbua Majipu" zitaendelea kuchukuliwa hadi tatizo hilo likomeshwe.

Dkt. Magufuli pia amekumbusha viongozi wote wakiwemo Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala na Wakurugenzi, kutekeleza wajibu wao ipasavyo na ameweka bayana kuwa mahali popote ambapo hapatakuwa na ufanisi, kiongozi husika atakuwa amedhihirisha kuwa hatoshi kuendelea na wadhifa aliopewa.

Rais Magufuli amewapongeza walimu kote nchini kwa kufanya kazi nzuri ya kufundisha, licha ya changamoto ya ongezeko kubwa la wanafunzi waliojiunga darasa la kwanza mwaka huu, lakini ametaka Wazazi na kamati za shule kushirikiana na walimu kuwasimamia wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.

"Niziombe kamati za shule zote Tanzania nzima, kama haziwezi kusimamia nidhamu ya wanafunzi shuleni, zile kamati za shule zijiuzulu. Lakini pia kama wewe ni Mwalimu Mkuu, shule yako kila siku inatoa divisheni ziro nyingi kila mwaka, sioni sababu ya wewe kuendelea kuwa Mwalimu Mkuu" Alisisitiza Dkt. Magufuli.

Kuhusu tatizo la wafanyakazi hewa, Rais Magufuli amesema uhakiki mdogo uliofanywa hivi karibuni, umebaini wafanyakazi hewa 1,680 waliokuwa wakilipwa shilingi bilioni 1 na milioni 800, na kwamba ni matarajio kuwa uhakiki unaofanywa nchi nzima utaisaidia serikali kubaini wafanyakazi hewa wengi zaidi na kunusuru fedha nyingi zaidi za watanzania.

Ametolea mfano wa mfanyakazi mmoja wa Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ambaye alikuwa akilipwa mishahara ya watu 17, na kueleza kuwa mfanyakazi huyo atafikishwa mahakamani.

Pia Rais Magufuli amesema serikali yake imejiandaa kuboresha maslahi ya wafanyakazi kwa kupunguza kodi kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 10 au 9 kuanzia bajeti ijayo, lakini amesema kwa wale wanaolipwa mishahara mikubwa ambayo inafikia hadi shilingi milioni 40, itapunguzwa na kuweka kima cha juu cha mshahara usiozidi shilingi milioni 15.

Inabidi ujue Tanzania inao watu wenye pesa zao na wanayo malengo au mipango mikubwa zaidi ya kibiashara ambayo kama ikienda inavyotakiwa wanaweza kuifanya nchi hii kutajwa zaidi kuwa na matajiri miongoni mwa nchi zenye Mabilionea Afrika.

Kituo cha Television cha Marekani CNN kilimuhoji Mtanzania huyu na kikaweka kichwa cha habari ‘kutana na Bilionea mwenye umri mdogo Afrika‘ ni Mohammed Dewji ambaye ameajiri watu karibu elfu ishirini na nane kutokana na viwanda na biashara zake.

Mbunge huyu wa zamani wa Singida mjini amesema ‘nimekua nikitaka kununua Benki kwa miaka minne mitano iliyopita, sasa hivi nimeamua nataka kuanzisha Benki yangu kabisa japokuwa hii ishu ya Benki ya Barclays Afrika kuuzwa imekuja na nashawishika japo sijajua kama wanataka mnunuzi atakaeichukua Afrika nzima‘

‘Nimeshawishika kuinunua Barclays upande wa Afrika Mashariki na ninayo pesa tayari, sijajua wanaiuzaje lakini sina mpango wa kuichukua Barclays yote kwa Afrika, ningependa kuinunua upande wa Afrika Mashariki kwenye nchi za Kenya, Uganda, Tanzania yaani kwenye nchi nne au tano hivi’ – Mo
Dewji

March 24 2016 Mohammed Dewji aliandikwa na CNN kwamba anataka kuingia kwenye soko la ushindani Afrika na kushindana na Coca cola kupitia kinywaji chake cha Mo Cola na namnukuu akisema ‘tunashindana na Red Bull kupitia Mo Energy Drink’
Naona Kigamboni ikibadilika kabisa. Inapaswa kuweka mipango Miji bora kuendana na uwekezaji huu wa Daraja. Haya ndio Maendeleo. Vitu vinaonekana badala ya porojo tu. 
Barabara zinazotoka na kwenda darajani ziboreshwe sasa. Vinginevyo itakuwa white elephant

Monday, March 21, 2016

Chukua dakika zako chache kusikiliza single hii mpya kutoka B.O.B Micharazo,Ngoma imefanywa na Maneck kutoka A.M Records.
Enjoy!!!!



AKOTHEE “GIVE IT TO ME” FEAT. FLAVOUR. Kenyan singer Akothee releases new single: Give It To Me featuring Nigerian singer – Flavour. Give It To Me is a certified banger that will set ablaze dance doors across Africa. Produced across Kenya and Nigeria by Nigerian finest producer Masterkraft with the video being filmed in South Africa by Godfather Productions. Akothee says, It was a lot of fun and hard work while recording Give It To Me. Hope my fans love it!

Saturday, March 19, 2016

A video posted by Joh makini (@joh_makini) on
SINGLE YENYEWE HII HAPA!!!

Thursday, March 17, 2016


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mh. Profesa Makame Mbarawa

Serikali imesema imesema daraja la Kigamboni lenye urefu wa mita 640 litafunguliwa rasmi, Aprili 16, mwaka huu.

Daraja hilo, linajengwa kwa ushirikiano kati ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na serikali kwa gharama ya dola za Marekani milioni 143.5 (Sh. bilioni 216), ulipangwa kumalizika ndani ya miezi 36 tangu kuzinduliwa kwake Septemba, 2012.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, aliyasema hayo jana kupitia taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini cha wizara hiyo.

Mbarawa alisema kazi inayoendelea sasa ni kupitisha magari maalum kwa ajili ya kupima ubora wa daraja ili kujiridhisha kabla ya kukabidhiwa rasmi serikalini.

Januari 27, mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mhandisi Joseph Nyamhanga, aliwahi kunukuliwa na vyombo vya habari akisema daraja hilo lingeanza kutumika Machi Mosi, mwaka huu.

Mbarawa amewataka watumiaji wa daraja hilo kuwa waangalifu, kulinda miundombinu na kuepuka vitendo vya hujuma ili lidumu kwa muda mrefu.

Daraja la Kigamboni likiendelea katika ujenzi. Linatoka Kurasini hadi Kigamboni. Lina urefu wa mita 640

“Daraja hili lina urefu wa mita 640, barabara sita, tatu zinapanda na tatu zinashuka, hivyo tunawaomba wananchi watakaovuka kuzingatia usafi na ustaarabu,” alisema Mbarawa.

Waziri Mbarawa alisema serikali pia itaweka sheria kali kwa wote watakaokiuka matumizi sahihi ya daraja hilo na kusisitiza umuhimu wa madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani wanapovuka katika daraja hilo.

Naye Meneja Msimamizi wa Ujenzi wa daraja hilo, Karim Mattaka, alisema wataalamu wanaendelea na taratibu ili kujiridhisha kama linamudu kupitisha uzito uliokusudiwa, kabla ya kulikabidhi kwa serikali.

Alisema awamu ya kwanza ya kulipima daraja hilo imekamilika na sasa wanaendelea na awamu ya pili hadi watakapomaliza awamu nne ili kujiridhisha kabla ya kuanza kutumika.

Wakati huohuo, Waziri Mbarawa amemteua Profesa Ninatubu Lema kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Usajiliwa Wahandisi (ERB) kwa kipindi cha miaka mitatu hadi Machi 10, 2019.

Pia amewateua Profesa Esnat Chaggu, Mhandisi John Ngowi, Mhandisi Gema Modu, Mhandisi Othman Khatib, Mhandisi Nuberis Nyange, Mhandisi Paul Basondole, Mkadiriaji Majenzi Samweli Marwa na Evelyn Marwa kuwa wajumbe wa ERB.

Monday, March 14, 2016

Sauti Sol (Kenya) and Alikiba (Tanzania) release UNCONDITIONALLY BAE, a danceable love ballad. In the song, Sauti Sol and Alikiba sing about the difficulty of finding love in the modern day world. The music video is poised to unite fans across East Africa and Africa at large, through dance and its strong message. #SautiSolAlikiba #UnconditionallyBae 
2nite Music Group presents, Flavour ft Chidinma- MAMA (official video).
Enjoy!!!

Wednesday, March 9, 2016


Tuesday, March 8, 2016



DAWASCO WAFICHUA NYARAKA ZA SERIKALI ZILIZOPATIKANA ENEO LA MANZESE UZURI JIJINI DAR ES SALAAM WAKATI WA MSAKO WA WEZI WA MAJI JIJINI
CENTRAL PARK BEES COMPANY LIMITED
Bonyeza Link hapo juu kupata Taarifa zoote za Bidhaa za Kufugia nyuki,pia asali yenye ubora wa hali ya juu inapatikana.

Hizi ni Baadhi ya Products zao:

1.Propolis

2.Royal Jelly

3.Honey


Hizi ni Baadhi ya Services zao:

PIA WANATOA TRAINING KATIKA UFUGAJI WA NYUKI

WASILIANA NAO KWA:
NYUKI NI KILIMO
1.0 Kutunza na kuhifadhi maji na udongo
Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania hujikimu kupitia kilimo. Ni asilimia 17 pekee ya ardhi nchini Tanzania inayofaa kwa kilimo. Kutokana na ukosefu wa nafasi na kuwepo kwa watu wengi uharibifu wa mazingira ni jambo ambalo haliwezi epukika. Hii ndio sababu katika sehemu hii ya ufugaji wa nyuki, tunaangalia njia za kutunza na kuhifadhi udongo na maji ili kuimarisha uzalishaji na kulinda mazingira
2.0 Hatua zinazostahili kufuatwa unapoanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki
• Hatua ya kwanza katika mikakati ya mradi wa ufugaji wa nyuki ni kupata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako.Zungumza na wale wanaojihusisha na nyuki.Andamana nao wakifanya kazi na nyuki.
• Ikiwa hauna ujuzi wa kufanya kazi na nyuki,kuna uwezekano wa kujifunza mengi kutoka kwa wafugaji wa nyuki katika eneo lako.Kwa kufahamu jinsi wanavyofanya kazi,unaweza kutoa maoni ya kuboresha kwa kustahilika,na itakuwa rahisi kutumia teknolojia ya ufugaji wa nyuki inayofaa katika eneo lako.
• Pia ,unafaa kupitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki. Kung’atwa na nyuki ni sehemu muhimu katika ufugaji wa nyuki.Mfugaji wa nyuki anapaswa kukabiliana nayo.
• Pindi tu unapoelewa uhusiano baina ya nyuki wa kienyeji na mwanadamu,mawazo ya kuanzisha utaratibiu ulioboreshwa unaweza kuundwa.Yafuatwayo ni maswali yanayofaa kutiliwa maanani:
1.Ni nani wa kufanya kazi naye?
2.Vifaa gani vinafaa kutumiwa?
3.Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?
• Ikiwa ndio unaanza na nyuki itakuwa bora ikiwa unafanya kazi na mtu mmoja ama wawili katika eneo lako.Kwa kuchagua wakulima wanaoheshimika na uhusiano mzuri na jamii ,juhudi zako zitaongezeka maradufu.Ukifuga nyuki mwenyewe na kutumia utaratibu tofauti na ule unaotumiwa katika sehemu yako
• Ni hatua katika mwelekeo unaofaa. Habari zitasambaa na punde ama baadaye utakuwa ukizungumza na marafiki ama majirani zako kuhusu ufugaji wa nyuki.
• Mara kwa mara anza ufugaji wa nyuki na angalau mizinga miwili.Hii itakupatia fursa kulinganisha maendeleo baina ya mizinga,na la muhimu zaidi,inaruhusu mradi kuendelea ikiwa koloni moja itaangamia.Pia,udhibiti wa mizinga yote badala ya mzinga mmoja binafsi unaweza kusisitizwa.
• Mabadiiliko huchukua muda.Ni lazima kuanza na wazo.Utoaji wa kufanikiwa wa wazo ni matarajio yanayoweza kutimilika ili kuanzisha utaratibu bora kwa uhusiano baina ya nyuki na binadamu katika maeneo mengine.
• Katika kupanga mradi,weka malengo yanayoweza kutimilika.Mradi mdogo,unaofaulu,una maana kuliko mkubwa uliojaribiwa na haukufaulu.
• Vifaa vitakavyotumiwa kwenye mradi hutugemea hali iliyoko.Unafaa kutathmini uwepo wa vifaa vinavyohitajika vile vile pia msaada wa kiufundi uliopo katika kuchagua aina ya ama aina za vifaa vya mzinga vinavyofaa.
• Tambua watu katika sehemu yako wanaoweza kutengeneza vifaa vya ufugaji wa nyuki ujenzi wake unaweza kuwa mafanikio kivyake.Inawza kuhitaji uvimilivu unaporatibu kupata vifaa pamoja.
• Milango ya uuzaji iliyopo kwa bidhaa za mzinga katika maeneo mengi.Tafuta watu ambao tayari wanatumia asali ama nta ya nyuki.Mara kwa maara wana hamu ya usambazaji thabiti wa bidhaa za hali ya juu.Ikiwa hawatumii asali,waoka mikate na watengenezaji wa peremende wana uwezekano wa kutoa soko.Watafute pia wale ambao wanaweza kutoa soko kwa nta ya nyuki.
3.0 Mazao kutoka kwa ufugaji wa Nyuki
Ufugaji wa nyuki huzalisha mazao mengi ya msingi lakini yale yanayotambulika sana ni asali na nta, lakini chavua,propolisi,jeli,sumu,malkia,nyuki na viluwiluwi ni mazao ya nyuki ya msingi yanayoweza kuuzwa.Ingawaje mengi ya mazao haya yanaweza kutumika au kuliwa jinsi yalivyotolewa na nyuki,kuna matumizi mengi ya ziada ambayo bidhaa hizi hutengeneza sehemu ama kiambato cha bidhaa zingine.Mingi ya mazao ya msingi ya ufugaji wa nyuki hayana soko hadi yaongozwe kwenye thamani ya bidhaa zinazotumika kwa wingi. Hata thamani ya bidhaa za msingi inaweza kuongezeka ikiwa utumizi mzuri utafanywa kwenye bidhaa zingine,hiyo kuongeza faida kwa mingi za shughuli za ufugaji wa nyuki.
• Asali: Asali hutumiwa kama chakula, kiambato cha chakula,dawa,na katika kiwanda cha tumbaku kuboresha na kuhifadhi harufu na unyevu,katika vipodozi kama matibabu ya ngozi,kuhifadhi maji na,kulainisha ngozi na katika krimu,sabuni,shampuu na rangi za mdomo.
• Chavua : Chavua hutumika kama chakula,dawa na vipodozi
• Nta: Hutumiawa katika utengeaneazaji wa mishumaa,vipodozi,kutengeneza vyakula,nguo,katika vanishi na polishi,upigaji chapa,katika dawa na kufinyanga na kuchonga vinyago
• Propolisi Propolisi ni mchanganyiko wa nta ya nyuki na utomvu unaokusanywa na nyuki anayetengeneza asali kutoka kwa mimea haswa maua na kichomoza cha jani. Nyuki hutumia propolisi kulainisha kiota na masega na kurekebisha nyufa ndani ya mzinga. Propolisi hutumiwa katika vipodozi,dawa na katika teknolojia ya vyakula.
• Jeli ya kifalme: (Hiki ni kitu chenye wingi wa madini ya protini ambacho nyuki wafanya kazi hutumia kulisha viluwiluwi katika kipindi cha awali cha kukua na viluwiluwi vya nyuki malkia katika vipindi vyao vyote vya kukua) Nyuki wafanyakazi wachanga ndio hutoa jeli ya kifalme ili kulisha viluwiluwi wachanga na nyuki malkia aliyekomaa.Jeli ya kifalme hutumiwa kama nyongeza kwa vyakula,na kama kiambato katika bidhaa za vyakula,dawa,vipodozi na kwa lishe ya wanyama.
• Sumu: Nyuki hutoa sumu wanapouma kama njia ya kujilinda.Sumu ya nyuki hutumiwa kama dawa kutibu mzio unao sababishwa na kuumwa kwa nyuki.
4.0 Ufugaji wa nyuki kama shughuli muhimu
Ufugaji wa nyuki ni shughuli,I nayowiiana vyema na miradi mingine ya maendeleo ya ukulima na mashambani. Miradi ya maendeleo katika maeneo pia hutoa uwezekano kwa utekelezaji wa ufugaji wa nyuki. Mimea fulani ikipandwa katika miradi Kama hii inaweza kuzalisha asali kwa mfugaji wa nyuki vile vile kunufaika kutoka kwa shughuli za uchavushaji za nyuki.Ufugaji wa nyuki unaweza kumtolea kipato cha ziada mkulima mdogo anayepanda mimea hii ama ana nyuki karibu.
Mimea ifuatayo inajulikana kwa kuwa ya manufaa kwa uchavushaji wa wadudu.Ile iliyowekwa alama ya nyota pia ni vyanzo vizuri vya mbochi kwa nyuki wanaotoa asali.
Mkonge,korosho,chai,paipai,nazi,kahawa,boga,tango,mawese,lichi,mchungwa/mdimu/mlimau,tufaha,parachichi,klova,tikitimaji,mpichi,mberimweusi ufuta,alizeti,maharage ya soya(baadhi ya aina) na alfalfa.
Mimea hunufaika kutoka kwa uchavushaji wa wadudu kwa ongozeko la seti ya mbegu.Hii husababisha ongezeko la mbegu na matunda ya hali ya juu.Nyuki ni wa manufaa kama wachavushaji katika hizo sehemu ambazo wadudu halisi wa uchavushaji hawapatikani ama hawatoshi kuchavusha sehemu kubwa zilizotengewa mmea mmoja.(kumbuka hata hivyo nyuki hawavutiwi na mimea yote)
Watu wanaojihusisha na na miradi ya misitu huwa wanavutiwa sana na ufugaji wa nyuki.Ufugaji wa nyuki ni kazi inayoleta mapato ikiwekwa kwenye raslimali ya msiti,hata hivyo sio haribifu kwa rasilmali hiyo.Mtu anayepata kipato kutoka kwa ufugaji wa nyuki kwa haraka anaweza kuwa mtetezi wa uhifadhi wa raslimali ya msitu.Ufugaji wa nyuki pia unapunguza uwezekano wa mto wa vichaka inayoashwa na wawindaji wa nyuki wanapochoma nyuki kutoka kwenye koloni za mbugani. Aina ya miti inayotumiwa katika juhudi za upandaji wa misitu ambayo ni chakula kizuri cha nyuki inaweza kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda cha ufugaji wa nyuki. Ufugaji wa nyuki ni sehemu ya kutumia rasilmali ya msitu yenye maiumizi chungu mzima.
Miti inayotumika kwa madhumuni ya kuni,kinga ya mimea na kivuli,pia hutoa mbochi wa kutosha kuzalisha asali katika maeneo mengine.Kama ilivvyo utokaji wa mbochi hutegemea mambo mengi(tabia ya nchi(hali ya joto,baridi ,mvua n.k),hali ya anga na ardhi),mti labda hauwezi kuwa mtoaji mzuri wa mbochi unapopelekwa katika eneo jipya.Angalia ikiwa aina ya mti ni nzuri katika utoaji wa mbochi katika hali utakaokuwa ukimea kabla ya kupigania utumizi wake kama chanzo kizuri cha mbochi kwa nyuki.
5.0 Ufugaji wa nyuki
Ufugaji wa nyuki ni shughuli muhimu inayosaidia jamii kujipatia mapato ya ziada ili kuboresha maisha yao. Nchini Tanzania, takriban asilimia 90 ya ardhi inafaa katika ufugaji wa nyuki.
Ufugaji wa nyuki ni mfumo wa kilimo unaohimili na wenye manufaa kwa mazingira. Ufugaji wa nyuki huwapatia watu walio ndani ya umaskini mapato ya ziada ya mara kwa mara,husaidia mazingira na huwa na manufaa mengine:
• Si ghali. Watu binaafsi ama mashirika ya kibinafsi kama makanisa,makundi ya wanawake,makundi ya vijanasna vyama vya mashirika vinaweza kuanza na kiasi kiodogo cha pesa.
• Haihitaji ulishaji wa jumla wa nyuki kwani nyuki hujitafutia chakula chao kwa mwaka mzima.
• Mizinga inaweza kutengenezwa na mafundi wa humu nchini ingawaje baadhi ya vifaa vinafaa kuagizwa kutoka ng’ambo.
• Haihitaji ardhi, kwa hivyo wale wenye rasilmali chache wanaweza kushiriki.
6.0 Kushiriki kwa Jamii katika ufugaji wa nyuki
Ingawaje ufugaji wa nyuki unachukuliwa kuwa shughuli ya mtu binafsi,imeleta wakulima wengi pamoja katika jamii nyingi,kugawana vifaa na kujifunza mengi kutoka kwa matukio yao.Katika baadhi ya vijiji,wafugaji wa nyuki wamekuja pamoja kuunda makundi na vyama.Mafunzo waliojifunza kwa kufanya kazi,pamoja imetumika katika maisha yao.+
7.0 Viota na mizinga ya nyuki
Kiota cha nyuki kina mfululizo wa masega ya nyuki yaliyo sambamba, kila sega likiwa na mistari ya nta ndani ya vyumba vya kuhifadhia asali,chavua, ama vya kukulia viwiliwili vya nyuki.Vyumba hivi vina umbo la pembe sita.Masega haya ni changamani na hutumiwa na nyuki kuwatunza watoto wao,kuhifadhi asali na kumlinda malkia.mzinga ni chombo chochote ambacho hutolewa kama makaazi kwa nyuki watoao asali.Wazo ni kuwahimiza nyuki kujenga viota vyao kwa njia ambayo ni rahisi kwa mfugaji wa nyuki kudhibiti na kuvuna masega ya asali.Mizinga ya nyuki ienaweza kugawanywa katika makundi matatu –kitamaduni,fremu inayosonga na mzinga wa kisasa wa teknolojia finyu.
• Mizinga ya kitamaduni ni ile ambayo imetengenezwa nchini kwa kutumia vitu tofauti,magogo yenye shimo kwa sehemu ya ndani ama chungu,lakini unapotoa asali,nta ,nyuki wengi huuawa.
• Mizinga yenye viunzi ni ile yenye viunzi ambavyo nyuki ujenga masega kulingana na nafasi iliyopo katika viunzi. Mizinga hii ni bora kuliko mizinga ya kitamaduni kwa kuzalisha asali nyingi na nta bora pia wakati wa kuvuna nyuki hawauwawi .Gharama za utengenezaji wa mizinga hii ni nafuu na mafundi seremala vijiji wanamudu kutengeneza mizinga hii.
• Mizinga yenye Fremu (mizinga ya ghorofa) inayosonga ni njia iliyoendelea ya kufuga nyuki. Hii hutumiwa kuzalisha asali maradufu kila msimu na kupunguza usumbufu kwa koloni ya nyuki. Idadi kubwa nyuki inaweza kuwekwa katika mzinga wa aina hii; hifadhi ya asali huwa kwa haraka wakati wa msimu wa maua. Ili kuunganisha udhibiti na ufanisi wa mavuno katika mzinga wenye fremu inayosonga,na manufaa ya kutokuwa ghali kutoka kwa mizinga ya kitamaduni. Nyuki wanahimizwa kucjenga masega chini ya mfululizo wa pao za juu. Pao hizi huruhusu kila sega kubebwa kutoka kwenye mzinga na mfugaji wa nyuki. Mizinga ya teknolojia finyu inaweza kutengenezwa ukitumia raslimali zinazopatikana nyumbani.

8.0 Kuvuna Asali na Nta
Asali huvunwa mwisho wa msimu wa maua. Mfugaji wa nyuki huchagua masega yenye asali iliyokomaa ,iliyofunikwa na rusu laini ... Vifaa Vingi vya vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji mdogo wa nyuki vinaweza kutengenezwa na mafundi vijijini. Smoker ...
9.0 Matatizo ya uzalishaji
• Ukosefu wa ujuzi na jinsi ya kupata vifaa na mbinu bora
• Mazao yenye ubora duni kutoka kwa wafugaji wengi.
• Kutokuwepo kwa utaratibu wa udhibiti ukaguzi wa ubora wa mazao
• Kutokuwepo kwa msaada kwa wafugaji nyuki
• Upatikanaji wa mitaji kwa watu wanaojishughulisha na shughuli zote za ufugaji nyuki.
10.0 Matatizo ya Masoko
• Ukosefu wa taarifa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
• Ukosefu wa huduma za usafirishaji wa mazao ya nyuki kutoka maeneo mbalimbali ya uzalishaji.
• Uuzaji wa asali na nta ghafi badala ya mazao yaliyoongezwa thamani.
• Kukosekana kwa utaratibu muafaka wa ulipaji wa kodi na ada kisheria kwa sababu ya ukosefu wa uratibu kati ya serikali na taasisi za kibiashara.
11.0 Kwa wakati huu kuna mifumo mikuu mitatu inayotumika katika uzalishaji na masoko ya mazao ya nyuki.
a) Wafugaji nyuki wengi hufanya kazi kila mtu peke yake bila kupata msaada wa vitendeakazi na namna ya kufikisha mazao yako kwenye masoko.
b) Wafugaji nyuki mmoja mmoja hujiunga katika vikundi ambavyo hujiunga pamoja kuunda vyama vya ushirika. Vyama hivi hutoa misaada mingi ikiwa ni pamoja na usafiri na vifaa vya kuhifadhia mazao ya nyuki.
c) Wapo wawekezaji Wakubwa binafsi huwapa wafugaji nyuki huduma zote wanazohitaji ili wazalishe na kuchakata asali yenye viwango vya juu vya ubora. Uzalishaji na masoko vinaweza kuboreshwa kwa kiwango cha juu kwa kuboresha mfumo wa (a) na (c).
SHULE BILA ADA: KILIMO NDIO UNGA MPYA!
Laki tano, Mshahara wa Ma-Teller wa Benki hapa mjini Laki Tano, Bei ya TECNO PHANTOM mpya kabisa kwa kujishau Snapchat na Istagram Laki Tano, Bajeti ya Mafuta ya SUBARU mwezi Mzima.... Laki Tano , Bajeti ya HEINEKEN 100 KWA wanywaji wa Pombe... HELA FLANI MBUZI TU ambayo wengi wanaona HAINA ISHU .

Lakini , Laki Tano hii ina uwezo wa kukodi shamba Ekari 13 pale Kiteto au Mpwapwa na ikakutengenezea Million 15 baada ya Miezi MITATU kwa kulima Matikiti maji.

Laki Tano hii hii ina uwezo wa kununua SIMTANK la lita 5000 ( ndoo 250 za lita 20) ambal inaweza kutumika kusolve shida ya maji mtaani kwako kwa kuuza ndoo 1 Sh 500 na ukaingiza 125,000 kwa kila SIMTANK unalouza.

Laki tano hii hii inaweza kulima Ekari 2 za Maharage pale Simanjiro na baada ya Miezi Minne ukavuna si chini ya Million 3 ambazo zitaexpand kilimo chako MARA 6 zaidi ya Mwanzo na Kuexpand Kipato chako mara 6 zaidi ya Mkupuo wa kwanza!
Laki Tano hii ina uwezo wa kulima Matikiti Maji Ekari 2 na zikakupa si chini ya Milion 2 na nusu baada ya SIKU 90!

SHIDA NI: Kila mtu anataka akae mjini AONEKANE SAMAKI SAMAKI, aonekane Muvi Mlimani City, Apost akiwa Escape 1, Apige Snapchat akiwa 777 ... Kila mtu anataka aonekane MDARISALAMA... Yuko mjini

MDADA yupo radhi aishi mjini kwa kuuza mwili wake kuliko kwenda Ruaha Mbuyuni Kuinvest kulima Vitunguu... Ataonyesha saa ngapi CROP TOP yake Mpya kutoka YAHYA BOUTIQUE? Sistaduu alime vitunguu?? Hapana, bora atafute Danga la Laki 2 akalale nalo!!

Big Up kwa wadada wote wajanja WALIOINVEST KWENYE KILIMO., kila Jumamosi wakati wewe unaona sifa kwenda HIGH SPIRIT LOUNGE Wadada wenzako wako RUVU wamekodi mashamba wanalima mpunga, unashangaa Huyu mdada anafanya nini kumbe mwenzio analima.

KUDOS kwa wanaume wenzangu ambao wamegundua siri kwamba kuuza Sura hakulipi na wameinvest Shamba, kila weekend wanapotea kwenda kusimamia nyanya na pilipili Bagamoyo.

Utaendelea kuwashangaa wenzio wanatajirika na kudhani kila mtu anauza UNGA hapa mjini, Kilimo ndio unga mpya... nnadhani @mkandamizaji amenuunua ile BMW X6 kwa episode za ORIJINO COMEDY? Thubutu, nenda MBARARI umkute amejaa Matope akipalilia Mpunga wake ndo utajua na wewe kwa nini unapanda Bajaji mpaka leo na kubaki kulalamika tu.

Written, Produced and Directed by Banky W, for EME & TILT Productions. Shot in NYC, and co-starring Adesua Etomi.
ujasiliamali
Na; Joseph Mayagila, AJTC
Kwanini unapanga kufanya biashara hiyo? Au Kwanini unafanya biashara hiyo unayoifanya? Je ulikuwa umepanga kufanya biashara hiyo au umejikuta tu unafanya biashara hiyo kwasababu ya ugumu wa maisha au kwasababu huna namna nyingine? Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha watu kufanya biashara wanazofanya. Ila katika kanuni za uchumi, ni vema unapochagua biashara uzingatie vigezo vifuatavyo:
ujaasil
Kigezo cha kwanza ni manufaa linganishi. Manufaa linganishi ni uwezo, ama ubora, au umahiri au upekee ulionao wewe kwaajiri ya kufanya biashara ya aina furani kwa umahiri zaidi ukilinganishwa na wafanyabiashara wengine ambao wanafanya biashara kama hiyo au watakaofanya biashara kama yako hapo baadaye.
Tuchukulie kwa mfano watu wawili wanaoishi maeneo tofauti wamepata taarifa kuwa bei ya mchicha imepanda thamani katika soko la dunia. Kati ya watu hao wawili mmoja anaishi Tanzania, na mwingine anaishi Zambia.
Mazingira ya mtu anayeishi Tanzania ni kwamba Tanzania kuna udongo wenye rutuba, kuna mito ya maji mwaka mzima, kuna mvua za kutosha, hali ya hewa ni nzuri, na sehemu kubwa ya nchi mazao yake hayahitaji mbolea. Hali hii ya Tanzania si kwamba labda kuna mtu aliileta, bali ni hali ya asili tangu enzi za mababu na mababu.Watanzania wote tumezaliwa tukaikuta ikiwa hivyo. Yaani ni urithi wa asili.
Na kwa upande wa Zambia, hali ya mazingira ya huko ni kwamba kuna mawe mawe, hakuna udongo laini unaofaa kwa kulima, nchi ile ni kame, mvua hakuna, kama unataka kulima lazima ununue kifusi cha udongo ili ukimwage shambani. Zambia hakuna mito inayotiririka maji mwaka mzima. Hali hii ya Zambia si kwamba labda wamelaaniwa, la hasha, bali ni mazingira yao ya asili ambayo Wazambia wote wameyakuta tangu mababu na mababu.
Iwapo Mtanzania na Mzambia wataamua kutendea kazi habari ya soko la mchicha Ulaya, mwisho wa siku wote watalima mchicha. Mtanzania atatumia gharama kidogo kulima bustani za mchicha kwa kuwa maji yapo, udongo mzuri upo,na hali ya hewa iko vizuri kuliko mzambia. Kwa hiyo inawezekana kwamba ili mtanzania apate faida ya shilingi elfu nne kwa fungu nmoja, atauza fungu moja la mchicha kwa shilingi elfu 5.
wajasiri
Lakini Mzambia kutokana na mazingira yake ambayo yanasababisha gharama za uzalishaji kuwa juu ili apate faida ya shilingi elfu nne kwa kila fungu itabidi auze fungu moja la mchicha kwa shilingi elfu 30. Je kati ya hawa wawili nani mwenye uwezekano wa kufanikiwa kibiashara sokoni? Wataalam wanasema if you have no a competitive advantage don’t compete, because the . world does not pay for average!
Ni kweli kwamba Mtanzania ana nafasi kubwa ya kufanikiwa kibiashara, na Mzambia ananafasi kubwa ya kufilisika
Hii ni kwasababu Mtanzania anayo manufaa linganishi ya kufanya biashara kiasili kuliko Mzambia. Mzambia naye anatakiwa atafute manufaa linganishi katika mazingira yake hayo ya kiasili ili na yeye apate biashara ya kufanya. Labda inaweza ikawa ni biashara ya kuchimba madini aina mbalimbali, au kuuza kokoto na kutengeneza barabara za rami, au kuanzisha viwanda vya sementi. Manufaa linganishi kwa lugha nyingine ni wito wa kufanikiwa kiuchumi.
SONY DSC
Je wito wako wa kufanikiwa kiuchumi ni nini?
Wito wa kufanikiwa kiuchumi ni hali au uwezo wako wa asili uliozaliwa nao wa kufanya jambo furani kwa ubora zaidi ya watu wengine. Unafanya jambo hilo vizuri si kwasasabu labda una akili kuliko watu wengine, bali ni kwasababu unauwezo wa kiasili katika kufanya jambo hilo. Mbwa kiasili anauwezo wa kubweka ili kutishia watu kuliko mbuzi. Kwa hiyo mbwa akipata mafunzo ya ULINZI, anaweza akawa askari mahiri kuliko mbuzi akisomea ulinzi. JE WEWE UNA ASILI YA KUFANIKIWA KATIKA KUFANYA BIASHARA GANI?
TAFAKALI YANGU KATIKA MAKALA HII
1. CHANGAMOTO KUBWA NI KUBUNI BIASHARA AMBAYO HANA ASILI NAYO, KISHA UNABAKI KUSHANGAA KWANINI MAMBO HAYAENDI.
2. NADHANI NI MUDA MUAFAKA KWAMBA MWANAFUNZI ANAPOMALIZA DARASA LA SABA AWE TAYARI ANAJUA ASILI YA MAFANIKIO YAKE NI KATIKA KUFANYA MAMBO GANI DUNIANI. ILI ANAPOENDELEA NA MASOMO AJIKITE KUSOMEA KITU AMBACHO KINAKUZA ASILI YAKE YA KUFANIKIWA. ELIMU NI KUKUZA UWEZO TULIONAO NA SI KUTULETEA UWEZO AMBAO HATUNA!
3. HIVI MBUZI AKIFUNDISHWA KUFANYA KAZI ZA UWINDAJI KAMA ZA SIMBA, MASOMO HAYO YATAMFAA AKIPATA MWALIMU MZURI?

“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhi. Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” ameeleza Makonda. Unakubaliana nayo hii au unaipinga??

1] P Square, ‘Peter Okoye, Paul Okoye’ wamefanya muziki toka 2001, wote wana lebel zao wenyewe na ni mabalozi wa kubwa wa bidha tofauti Nigeria
2] Don Jazzy aka Michael Collins Ajereh, Anafanya kazi hii toka mwaka 2004, ni msanii na anamiliki lebel kubwa ya Marvins, balozi wa bidha kubwa Nigeria kama MTN, Loya Milk, Konga, na Johnny Walker, ana wasanii wakubwa zaidi ya watono kwenye lebel yake ka Tiwa Savage na Koredo Bello.

3] 2 Face aka Innocent Ujah Idibia , anafanya muziki toka 1996
4] Wizkid aka Ayodeji Ibrahim Balogun anafanya muziki toka mwaka 2001
5] Davido aka David Adedeji Adeleke boss wa lebel kubwa yenye wasanii zaidi ya watano HKN. anafanya muziki toka 2011
6] D’banj aka Oladapo Daniel Oyebanjo, msanii wa kimataifa liye chini ya lebel ya Kanye West, anafanua muziki toka mwaka 2004
7] Tiwa Savage aka Tiwatope Savage-Balogun, anafanya muziki toka 2006
8] Banky W aka Olubankole Wellington anafanya muziki toka mwaka 2003
9] M.I Abaga aka Jude Abaga, Boss wa lebel kubwa ya Chocolate City, anafanya muziki toka 2006
10] Olamide aka Olamide Adedeji ,anafanya muziki toka mwaka 2010
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ