• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Sunday, April 12, 2015

Kiongozi wa Muslim Brotherhood kunyongwa

No comments:
 
Mohamed Badie

Mahakama moja nchini Misri imethibitisha hukumu ya kifo ya kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na watu wengine 13 kwa kupanga mashambulizi dhidi ya serikali.
Pia mahakama hiyo imemfunga maisha raia mmoja mwenye uraia wa Marekani na Misri na watu wengine 36.
Badie alipewa hukumu hiyo mnamo mwezi Machi na pia anakabiliwa na mashtaka mengine.
Hatahivyo anaweza kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.
Mamia ya watu wamehukumiwa kifo katika msako dhidi ya wanachama wa kundi hilo kufuatia kuondolewa kwa rais Mohammed Morsi mwaka 2013.
Hatahivyo ,kufikia sasa ni mtu mmoja pekee aliyenyongwa.
Uamuzi huo wa mahakama ulitangazwa moja kwa moja na runinga za taifa hilo.
Hukumu hizo ni za mwisho katika kesi ambayo viongozi wa kundi la Muslim Brotherhood walishtakiwa kwa kuwachochea wanachama wa kundi hilo kuanzisha ghasia dhidi ya serikali kufuatia maandamano ya mwaka 2013.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ