"Chukua muda wako wa kufikiri na kutafakari,na wakati ukifika fanya ulilopanga"
Hili ni somo kubwa kukumbuka wakati tuko
katika vita ya nafsi yako wenyewe; wakati tunajua nini tunapaswa kufanya lakini
tunashindwa kufanya.
Labda tunaliweka mbali kwa saa. Labda kwa
siku. Na inaweza hata kuwa wiki . Lakini hatukufanya kwa wakati.
Kusitasita kunaweza kuwa ndio nyenzo kubwa
inayokumaliza na kukukandamiza.ingawa kuna watu walioweza kuishinda nafsi yao
ya kusita na kufanya mambo yakafanikiwa na kuwa mazuri.Je walifanikiwa kivipi?
Hizi ndizo Nguzo Tano(5) ambazo wengi
waliofanikiwa huzitumia.
1.Wanatambua thamani ya Muda wao
waliochelewa.
Wengi hudhani katika kila wafanyalo wanataka
lilete matokeo ya papo kwa papo jambo
ambalo si kweli.
Wengi waliofanikiwa hufurahia matunda yao
na huweza kufanya jambo ambalo hutumia mudawao mwingi kulijua na kulifanya kwa
uhakika.Hufanya kazi inayoonekana ni kubwa kwa Tathmini na baadae kuonekana kuwa
Ndogo kimuonekano ambapo hufurahia mafanikio hayo mapema na mara kwa mara.”Mafanikio
huja kwa kufanya,na sio Matokeo”
Anza kujipongeza kwa Uvumilivu.Furahia
mafanikio yako kwa Uvumilivu wa kila ufanyalo.Itakusaidia kupunguza mambo mengi
uliopanga kuyafanya na kufanya kila jambo kwa wakati.
2.Hujali
zaidi Muda wao wa kila siku.
Unadhani
shughuli itakuchukua masaa matatu kukamilika,lakini huna mpangilio wa swala
hilo kulimaliza kwa masaa hayo matatu.Unataka kuliacha hadi hapo baadae
utakapokuwa na muda wa ziada.
Wakati shughuli
hiyo isingekuchukua masaa matatu bali Saa moja na nusu tu.Watu makini huanza
katika muda walionao na huendelea mpaka hapo wanapofanikisha.
Huogopa
kuangukia katika kundi la watu wavivu,ingawaje inaweza kuwachukua muda wao wote
kufanya wafanyalo na kulijua vizuri,huchukua muda wao wanaokuwa nao hata muda
wa baadae katika swala moja hata watakapolifanikisha.Na hilo ndilo lengo lao.
3.Hufanya
katika umakini wa hali ya juu na kwa ufanisi mkubwa.
Ni kweli
ufanisi na umakini kwa kila tulifanyalo huleta matunda mazuri.watu ambao
hufanya tufanye kazi kwa ufanisi mkubwa na umakini ni MARAFIKI WAZURI na sio tu
MARAFIKI.Umakini hukaa katika mawazo yako na kukufanya ujione unalofanya sio
kwamba linakutosheleza bali utataka kufanya zaidi navizuri.Utakufanya kila
ufanyalo kuonekana gumu zaidi ya linavyotakiwa kufanywa ili lifanikiwe.
Acha
kuwa mpinzani wa nafsi yako.Hutakiwi kufanya kazi mbaya usiyoipenda,ili kuzuia
hili jipe moyo kwa kila ufanyalo na kuamini litafanikiwa.
4.Ni
wazuri na makini katika kupangilia.
Je
unadharau kidogo na kutaka makubwa?Hili ni jaribu kubwa,kwasababu linakupa ujasiri
wa kutaka kufanya makubwa na mengi wakati mudawako haujafika.Acha kuwa na
mpangilio wa kufanya mambo mengi kwa wakati mchache.
Ingawa
kwa watu Makini huwa tofauti,
Watu
makini hupendelea kulichukua Jambo kubwa na Gumu,Jambo Muhimu huanza kwanza
katika kila Mambo yao.
5.Hawajipingi
wenyewe,wala kujikatisha Tamaa.
Mambo
mengi ambayo wengi hujiuliza ni kwamba,Itakuwaje wakishindwa baada ya kujaribu
kufanya jambo fulani au shughuli fulani,Je Bosi wake atamchukia?Itakuwaje
ikimchukua mudawake wote katika kufanya Jambo moja?
Watu
makini huondoa uoga wa kufanya jambo gumu na uoga wa kushindwa pia kama “Roger Babson” alivyosema “Keep
in mind that neither success nor failure is ever final.”
Usiweke
uoga wako wa kushindwa kwa mambo au shughuli ulizopanga kufanya,zaidi zaidi
tilia mkazo na utafanikiwa.
No comments:
Post a Comment