• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Monday, February 13, 2017

KIDATO CHA KWANZA WANATEGEMEA KUPIMWA NA NECTA KWA MITIHANI MAALUM

No comments:
 
Hii imeafikiwa kutoka Baraza la mitihani la Taifa (Necta) kuwa Kidato cha kwanza watakuwa wakipimwa na Necta kwa mitihani maalum,Upimaji huu maalum wa Stadi na Maarifa kwa utafanywa kwa wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu shule za Serikali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana kutoka Necta na Kusainiwa na Kaimu Mtendaji,Dr.Richard Kasuga,Makatibu tawala Tanzania Bara wanajulishwa kuanza kufanikisha mchakato huo na Upimaji huo unatarajiwa kuanza February 28,Mwaka huu.

Ilifafanua kuwa wanafunzi wote waliofaulu kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu wanatakiwa kufanyiwa mtihani maalumu kwa ajili ya kuwapima ili kubaini uwezo wao waliouonesha katika mitihani yao ya Shule ya Msingi.

Iliongeza kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuwabaini Wanafunzi waliofaulu kwa njia ya Udanganyifu na watakaobainika wataondolewa Shuleni.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ