• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Thursday, August 2, 2012

MIKATABA YA RINGTONE ZA WASANII WA BONGO INATUMIA SHERIA ZA NIGERIA

No comments:
 
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema baadhi ya mikataba ya makampuni yanayohusika na uuzaji wa ringtone(Aggregators)zinazotokana na Nyimbo za wasanii wa Tanzania,inatumia sheria za Nigeria.
Amesema pamoja na mikataba hiyo kutokuwa wazi,imeandikwa kwa lugha mbaya kiasi cha wasanii wengi kushindwa kuielewa.
Akiongea na Clouds Fm,Zitto amesema kama kiongozi atahakikisha masuala hayo anayapigania kwa dhati ili wasanii wapate haki yao.
"Maamini kabisa kwamba baada ya Bunge kuwa limeshatoa maagizo,na kwasababu tuna Waziri kijana pale,ndugu January Makamba,jambo hili litaisha haraka,nina imani kabisa na ndugu Makamba"alisema Zitto.
Ameongeza kuwa anatarajia wizara ya Mawasiliano,Sayansi na Technolojia itaita wadau mwezi huu wa Nane ili kulizungumzia suala hilo ambao ni pamoja na wasanii wenyewe,Taasisi mbalimbali kama Cosota na Basata ambazo amesema nazo zina matatizo pamoja na makampuni ya simu.
Juzi Umoja wa wasanii nchini uliyaandikia barua makampuni ya simu nchini kusitisha mara moja mikataba ya matumizi ya nyimbo zao kama Ringtone hadi pale watakapokaa chini na kukubaliana malipo mengine yenye maslahi zaidi.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ