Prince Harry ameamua kuifunga page yake ya Facebook ikiwa ni wiki moja baada ya picha zake akiwa uchi kusambaa kwenye internet .
Hata hivyo page hiyo ilikuwa na jina tofauti ili kuepuka watu kumsumbua.
Jina alilokuwa anatumia Facebook ni Spike Wells ambalo mara nyingi lilikuwa likionesha habari kuhusu Harry pamoja na picha zake.
Kingine ni kuwa jina la utani la Harry ni “Spike,”kwa mujibu wa gazeti la Telegraph, ambalo limesema kuwa anajulikana sana kwa jina hilo.
Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa Us Weekly kuwa Prince Harry atakaa kimya kwa muda kwenye mtandao huo kwakuwa alishauriwa kujiondoa kwanza mpaka scandal hiyo ipungue.
No comments:
Post a Comment