• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Thursday, October 18, 2012

Ney wa Mitego aelezea sababu za kutoa ‘Wamenichokoza’

No comments:
 


Kila atoapo wimbo, Ney wa Mitego huanzisha mijadala vijiweni, redioni mpaka kwenye mitandao ya kijamii.
Baada ya kusababisha mgongano mkali na wasanii wa Bongo Movies na wimbo wake Nasema Nao, rapper huyo hivi karibuni ameachia single yake mpya aliyoipa jina la ‘Wamenichokoza’ na amezungumzia lengo la kutoa wimbo huo.
“Baada ya kutoa wimbo ‘nasema nao’ pametokea vitu vingi sana vya kufanya labda kama kunikatisha tamaa hivi au kunitia uoga nisiendelee kufanya mimi ambacho nakifanya, so kumetokea walokole ambao ndio wanajidai walokole ambao mimi naimani kama walitumwa hivi ili kunikwamisha kwamba wanajua kifo changu mimi nitakufa lini, sijui tarehe30 nitachomwa kisu au kupigwa risasi,” ameiambia Bongo5.
“Yeah yametokea mambo mengi vurugu vurugu Bongo Movie wakasema hivi, kuna wengine wakafanya hivi aaah zile ni harakati za kunikwamisha.”
Aliendelea kwa kusema kuwa yale ambayo huwa anayaongea huyaandika wakati akiwa na akili yake timamu na sio bangi wala pombe ndio maana akaandika ‘Wamenichokoza’.
“Kwahiyo wazo la ‘’Wamenichokoza ‘’limetokea na matukio yaliyonitokea hapo katikati. Kuhusu video ya nimeshamaliza kupanga script na Juma tano nitaanza kushoot,”alisema.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ