Mhe.
Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
katika picha ya pamoja na Mwenyeji wake Mhe. Laurent Fabius, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini Paris leo.
Mheshimiwa
Waziri Bernard K. Membe (Mb.) , Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa katika mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu wa La
Franchophonie na Rais Mstaafu wa Senegal alipofanya nae mazungumzo
ofisini kwake Paris leo. Wa kwanza kushoto ni Mhe. Begum Karim Taj,
Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa.
Mhe. Waziri Membe na mwenyeji wake Mhe. Abdou Diouf katika picha ya pamoja na ujumbe wao mara baada ya mazungumzo.
Mhe.
Waziri Membe yuko nchini Ufaransa kuwasilisha ujumbe maalum wa Mhe.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa Ulinzi
na Usalama kwa Mhe. Francois Hollande, Rais wa Ufaransa. Mhe. Waziri
Membe amewasili leo asubuhi na kufanya mazungumzo na Mwenyeji wake Mhe.
Laurent Fabius, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa ofisini kwake jijini
Paris.
Mhe.
Membe aliwasilisha ujumbe wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete,
Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama kwa Mhe.
Francois Hollande, Rais wa Ufaransa. Tanzania ni Mwenyekiti wa Asasi ya
Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC, chombo kinachoshughulikia migogoro na
usuluhishi katika ukanda wa SADC.
Baadaye,
Mhe. Waziri Membe alifanya mazungumzo na Mhe. Abdou Diouf, Katibu Mkuu
wa La Francophonie na Rais Mstaafu wa Senegal. Mhe. Waziri Membe
anatarajia kumaliza ziara yake kesho kwa kukutana na Mshauri wa Rais
Hollande wa Masuala ya Afrika.
No comments:
Post a Comment