Wakazi wa eneo la Mapinga Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.
No comments:
Post a Comment