Shirika la India linalohusika na ubora wa vyakula limepiga marufuku utengenezaji wa chakula aina ya tambi ziitwazo ''Maggi Noodles'' baada ya kugunduliwa kuwa na kiwango kikubwa cha madini hatari aina ya lead.
Shirika hilo pia limeitaka kampuni ya Nestle inayotengeneza tambi hizo kuondoa bidhaa hizo kote nchini India zilikokuwa zikiuzwa.
Kulikuwa na aina tisa ya ''Maggi Noodles'', bidhaa iliyotokea kushabikiwa na walaji wengi hivyo kununuliwa kwa wingi.Bidhaa hiyo inashikilia asilimia 80% ya soko la tambi nchini humo.
Kampuni yenyewe ilikuwa imejitetea kwa kusema inaamini chakula hicho ni salama lakini wanaziondoa sokoni tambi hizo kama hatua ya tahadhari.
Wakati huohuo Singapore imesitisha mauzo ya tambi hizokutoka india nchini mwao.
Kufuatia tukio hilo soko la tambi za Nestle limeporomoka huko India .
No comments:
Post a Comment