• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Tuesday, October 20, 2015

KUNDI LA MAFIKIZOLO KUVUNJIKA? UKWELI UPO HAPA

No comments:
 
Mafikizolo
Nhlanhla Nciza na Theo Kgosinkwe wanaounda kundi la Mafikizolo

Tetesi!!!!!
Muimbaji wa kiume wa kundi la Mafikizolo la nchini Afrika Kusini, Theo Kgosinkwe ameamua kuzielezea tetesi kuwa kundi hilo lipo mbioni kuvunjika.
Tetesi hizo zilianza baada ya muimbaji wa kike wa kundi hilo, Nhlanhla Nciza kuanzisha kampuni yake fashion na Theo kudai kuwa anaanzisha lebo yake mwenyewe.
“Siondoki na hatuvunjiki kama kundi. Siku zote nimekuwa na ndoto ya kuwa producer na nataka kukuza pia vipaji vichanga. Nahisi kuwa huu ndio muda wa mimi kuanza safari mpya kama producer na mfanyabiashara,” Theo aliliambia jarida la Move!

Tayari Theo ameshamsainisha msanii wa kwanza wa kike aitwaye, Melo kwenye lebo yake, 350 Degrees Entertainment.

Credits:2 Bongo 5

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ