BUNGE la Tanzania limemchaguwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Dk. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dk. Tulia Mwansasu amechaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kumshinda mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, Magdalena Sakaya toka Chama cha Wananchi CUF aliyekuwa mgombea kwenye nafasi hiyo.Dk. Tulia Mwansasu ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 250 ikiwa ni sawa na asilimia 71.2 ya kura zote 351 zilizopigwa na wabunge kwenye zoezi la upigaji kura. Mpinzani wake Magdalena Sakaya ameambulia kura 101 ikiwa ni sawa na asilimia 28.8.
KABLA YA KUPATIKANA KWA NAIBUSPIKA BUNGE LILIFANYA NCHAKATO WA KUMPATA WAZIRI MKUU
Mh.Kassim Majaliwa
*Sherehe za kumuapisha Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (pichani), Waziri Mkuu Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitafanyika katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 20 Novemba, 2015 kuanzia saa 4.00 Asubuhi.* *Sherehe hizo zinafanyika siku moja baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitisha jina lake kwa kura nyingi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia uteuzi uliofanywa na Mhe. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.*

No comments:
Post a Comment