Hili ni jengo la (TPA) Tanzania Ports Authority,likiwa katika hatua za mwisho za ujenzi,jengo hili Lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi , sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na maofisi mbalimbali.
lipo jirani na Majengo pacha yenye ghorofa 35 ya PSPF Towers yaliyopo mtaa wa Sokoine jijini Dar es Salaam yaliyozinduliwa Septemba 16, 2015 na Rais Jakaya Kikwete.
Picha chini zikionesha majengo pacha ya PSPF na Jengo la TPA.
Imeelezwa kuwa PSPF Towers ni moja ya majengo machache marefu barani Afrika na ndiyo jengo refu zaidi lililokamilika Afrika Mashariki na Kati, likiwa na urefu wa meta 147.
Ujenzi wa jengo hilo ulichukua miaka minne (2011 hadi 2015) na limegharimu shilingi bilioni 139.20 za Kitanzania. Lina maeneo ya ofisi na nyumba za makazi 88, sehemu ya mgahawa, mabenki, bwawa la kuogelea, sehemu za kufanyia mazoezi, maegesho ya magari na kadhalika.

Majengo mengine marefu Afrika ni Carlton Centre (meta 223) lililopo Afrika Kusini, Hassan II Mosque (meta 210) lililopo Moroko, Ponte City (meta 173) lililopo Afrika Kusini, Necon House (meta 160) lililopo Nigeria, Marble Tower (meta 152), Pear dawn (meta 152), Met Life Centre (meta 150) na 88 on field (meta 147) yote ya Afrika ya kusini.
Engineer aliyejenga Majengo pacha ya PSPF ndiye mjenzi wa Ghorofa hili la TPA lenye umbo la Meli.
Tusubiri sifakamili za jengo hili pindi wamalizapo ujenzi huo.

No comments:
Post a Comment