• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Tuesday, January 5, 2016

KIKAO CHA WASANII WOTE WA TANZANIA KIMEFANYIKA LEO TAREHE 05/01/2016 NA HAYA NDIO YALIYOAZIMIWA KWA COSOTA NA CMEA

No comments:
 
Baada ya maumivu ya muda mrefu ya wasanii wa Tanzania kutopata haki zao za msingi kwa kazi zao wanazotoa kila kukicha iwe Muziki,Filamu,Maigizo na Uchongaji wa Vinyago.Sasa suluhisho karibia lipatikane baada ya mambo haya kuadhimiwa.

Msanii wa Tanzania amekuwa akinyonywa kwa muda mrefu kutokana na Mfumo mzima wa wasimamizi waliopewa dhamana ya kuwasimamia kutofanya kazi itakiwavyo ikionesha mfumo ulivyo mbovu unaoonyesha mianya ya kunyonywa kwa hapa na pale kwa kazi za wasanii, pia waliadhimia kuvunjwa kwa Bodi ya Cosota na CMEA(Copyright Management East Africa) kikao hiki pia Kiliziomba Radio Stations zote na TV stations kuendelea kucheza Nyimbo zao kama kawaida na si kama ilivyoamuliwa siku chache zilizopita kuwa ifikapo Tarehe moja mwezi huu kuwa mwisho wa kucheza muziki bila malipo kwa wasanii ila ziendelee kupiga muziki wao mpaka watakapotangaza wasanii wenyewe baada ya makubaliano kuafikiwa.

Kutokana na hayo yoooote maoni ya wadau wa Muziki Tanzania walikuwa na haya ya kusema:-
- Godwini Gondwe anaona kunamaono tofauti juuya issue hii nzima mapungufu ni mengi ktk malipo na issue nzima ya ukusanyaji wa mapato.
- Wasanii inabidi wafanye vizuri sana katika kazi zao la si hivyo watapotea wengi sana katika ramani ya Muziki.

Wasanii walimalizia kwa makubaliano kwamba:-
-Bodi ya Cosota ihusishe wasanii kuwapo katika bodi kama ma board-members
-CMEA ilikuwa kama "Push Mobile" kutokana na ugumu wa ufuatiliaji wa mirabaha ya wasanii kwahiyo wameadhimia CMEA nayo kuvunjwa kuwapa mwanya wa kuunda Mfumo utakaowasaidia zaidi wasanii na sio watu wachache.


No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ