• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, March 4, 2016

Sababu ambazo huchangia kuvunjika kwa ndoa nyingi

No comments:
 
Ndoa ni unganiko la kimwili na kiroho baina ya jinsia KIKE na KIUME(Hizi za mashoga, *******, mahanithi si ndoa).Huu ndio ushirikiano pekee ambao una umri mrefu katika historia ya Mwanadamu. Kutokana na hayo nimekuwa nikijiuliza sana, ni nini haswa chimbuko la ndoa nyingi kuvunjika, na wimbi hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku. Zifuatazo binafsi naona ni baadhi tu ya sababu ambazo huchangia kuvunjika kwa ndoa.

  1. Kujifanya mjuaji wa kila kitu kwa wenza wetu - Hivi ushawahi kuishi na mtu asiyependa kushuka wengine huita kujishusha? Mtu wa namna hii huwa ni kero na humfanya mwenzake asijiamini "inferiority"
  2. Kujali marafiki kuliko mwenza wako wa ndani - Kumbuka mapenzi yanahitaji kujaliana baina ya wapendanao, sasa jiulize ukutane na mtu asiyemjali mwenzi wake, kutwa kushinda na marafiki au hata kuwafanya ndio nduguze.
  3. Kutaka matumizi makubwa kuliko uwezo.
  4. Uongo kwenye ndoa.
  5. Kusahau wajibu wa kila mmoja katika ndoa - Ni wazi kuwa mwanamke na mwanaume hawana wajibu sawa katika ndoa. Kila mmoja ana aina yake ya majukumu ambayo anapaswa kuwajibika kwayo...
    Mathalani jaribu kufikiria mwanaume aisiyetoa matunzo (kumbuka wajibu wa mwanaume ni kutunza familia) maridhawa kwa mke au familia, lakini kwa wakti huo huo anajijali sana yeye.
  6. Kuoana kwa sababu fulani,,,mfano Utajiri, umaarufu, shinikizo toka kwa wazazi, mimba zisizotarajiwa.
  7. Kuamini sana maneno ya watu na kuyabeba pasipo kufanya uchunguzi.
  8. Utandawazi na ukuaji wa teknohama kwa mfano Simu, mitandao ya kijamii n.k
  9. Tamaa na kutoridhika.
  10. Hasira na kutokusamehe.

Ni nini haswa tunapaswa kufanya ili kuepuka haya? au ni zipi sababu nyingine ambazo hupelekea matengano?
....Karibuni kuchangia....

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ