• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Tuesday, March 8, 2016

UFUGAJI WA NYUKI NI MKOMBOZI KWA MAISHA YAKO : ANGALIA FAIDA ZAKE KIUCHUMI NA KIAFYA

No comments:
 
CENTRAL PARK BEES COMPANY LIMITED
Bonyeza Link hapo juu kupata Taarifa zoote za Bidhaa za Kufugia nyuki,pia asali yenye ubora wa hali ya juu inapatikana.

Hizi ni Baadhi ya Products zao:

1.Propolis

2.Royal Jelly

3.Honey


Hizi ni Baadhi ya Services zao:

PIA WANATOA TRAINING KATIKA UFUGAJI WA NYUKI

WASILIANA NAO KWA:
NYUKI NI KILIMO
1.0 Kutunza na kuhifadhi maji na udongo
Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania hujikimu kupitia kilimo. Ni asilimia 17 pekee ya ardhi nchini Tanzania inayofaa kwa kilimo. Kutokana na ukosefu wa nafasi na kuwepo kwa watu wengi uharibifu wa mazingira ni jambo ambalo haliwezi epukika. Hii ndio sababu katika sehemu hii ya ufugaji wa nyuki, tunaangalia njia za kutunza na kuhifadhi udongo na maji ili kuimarisha uzalishaji na kulinda mazingira
2.0 Hatua zinazostahili kufuatwa unapoanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki
• Hatua ya kwanza katika mikakati ya mradi wa ufugaji wa nyuki ni kupata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako.Zungumza na wale wanaojihusisha na nyuki.Andamana nao wakifanya kazi na nyuki.
• Ikiwa hauna ujuzi wa kufanya kazi na nyuki,kuna uwezekano wa kujifunza mengi kutoka kwa wafugaji wa nyuki katika eneo lako.Kwa kufahamu jinsi wanavyofanya kazi,unaweza kutoa maoni ya kuboresha kwa kustahilika,na itakuwa rahisi kutumia teknolojia ya ufugaji wa nyuki inayofaa katika eneo lako.
• Pia ,unafaa kupitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki. Kung’atwa na nyuki ni sehemu muhimu katika ufugaji wa nyuki.Mfugaji wa nyuki anapaswa kukabiliana nayo.
• Pindi tu unapoelewa uhusiano baina ya nyuki wa kienyeji na mwanadamu,mawazo ya kuanzisha utaratibiu ulioboreshwa unaweza kuundwa.Yafuatwayo ni maswali yanayofaa kutiliwa maanani:
1.Ni nani wa kufanya kazi naye?
2.Vifaa gani vinafaa kutumiwa?
3.Ni wapi pa kuuza bidhaa za mzinga?
• Ikiwa ndio unaanza na nyuki itakuwa bora ikiwa unafanya kazi na mtu mmoja ama wawili katika eneo lako.Kwa kuchagua wakulima wanaoheshimika na uhusiano mzuri na jamii ,juhudi zako zitaongezeka maradufu.Ukifuga nyuki mwenyewe na kutumia utaratibu tofauti na ule unaotumiwa katika sehemu yako
• Ni hatua katika mwelekeo unaofaa. Habari zitasambaa na punde ama baadaye utakuwa ukizungumza na marafiki ama majirani zako kuhusu ufugaji wa nyuki.
• Mara kwa mara anza ufugaji wa nyuki na angalau mizinga miwili.Hii itakupatia fursa kulinganisha maendeleo baina ya mizinga,na la muhimu zaidi,inaruhusu mradi kuendelea ikiwa koloni moja itaangamia.Pia,udhibiti wa mizinga yote badala ya mzinga mmoja binafsi unaweza kusisitizwa.
• Mabadiiliko huchukua muda.Ni lazima kuanza na wazo.Utoaji wa kufanikiwa wa wazo ni matarajio yanayoweza kutimilika ili kuanzisha utaratibu bora kwa uhusiano baina ya nyuki na binadamu katika maeneo mengine.
• Katika kupanga mradi,weka malengo yanayoweza kutimilika.Mradi mdogo,unaofaulu,una maana kuliko mkubwa uliojaribiwa na haukufaulu.
• Vifaa vitakavyotumiwa kwenye mradi hutugemea hali iliyoko.Unafaa kutathmini uwepo wa vifaa vinavyohitajika vile vile pia msaada wa kiufundi uliopo katika kuchagua aina ya ama aina za vifaa vya mzinga vinavyofaa.
• Tambua watu katika sehemu yako wanaoweza kutengeneza vifaa vya ufugaji wa nyuki ujenzi wake unaweza kuwa mafanikio kivyake.Inawza kuhitaji uvimilivu unaporatibu kupata vifaa pamoja.
• Milango ya uuzaji iliyopo kwa bidhaa za mzinga katika maeneo mengi.Tafuta watu ambao tayari wanatumia asali ama nta ya nyuki.Mara kwa maara wana hamu ya usambazaji thabiti wa bidhaa za hali ya juu.Ikiwa hawatumii asali,waoka mikate na watengenezaji wa peremende wana uwezekano wa kutoa soko.Watafute pia wale ambao wanaweza kutoa soko kwa nta ya nyuki.
3.0 Mazao kutoka kwa ufugaji wa Nyuki
Ufugaji wa nyuki huzalisha mazao mengi ya msingi lakini yale yanayotambulika sana ni asali na nta, lakini chavua,propolisi,jeli,sumu,malkia,nyuki na viluwiluwi ni mazao ya nyuki ya msingi yanayoweza kuuzwa.Ingawaje mengi ya mazao haya yanaweza kutumika au kuliwa jinsi yalivyotolewa na nyuki,kuna matumizi mengi ya ziada ambayo bidhaa hizi hutengeneza sehemu ama kiambato cha bidhaa zingine.Mingi ya mazao ya msingi ya ufugaji wa nyuki hayana soko hadi yaongozwe kwenye thamani ya bidhaa zinazotumika kwa wingi. Hata thamani ya bidhaa za msingi inaweza kuongezeka ikiwa utumizi mzuri utafanywa kwenye bidhaa zingine,hiyo kuongeza faida kwa mingi za shughuli za ufugaji wa nyuki.
• Asali: Asali hutumiwa kama chakula, kiambato cha chakula,dawa,na katika kiwanda cha tumbaku kuboresha na kuhifadhi harufu na unyevu,katika vipodozi kama matibabu ya ngozi,kuhifadhi maji na,kulainisha ngozi na katika krimu,sabuni,shampuu na rangi za mdomo.
• Chavua : Chavua hutumika kama chakula,dawa na vipodozi
• Nta: Hutumiawa katika utengeaneazaji wa mishumaa,vipodozi,kutengeneza vyakula,nguo,katika vanishi na polishi,upigaji chapa,katika dawa na kufinyanga na kuchonga vinyago
• Propolisi Propolisi ni mchanganyiko wa nta ya nyuki na utomvu unaokusanywa na nyuki anayetengeneza asali kutoka kwa mimea haswa maua na kichomoza cha jani. Nyuki hutumia propolisi kulainisha kiota na masega na kurekebisha nyufa ndani ya mzinga. Propolisi hutumiwa katika vipodozi,dawa na katika teknolojia ya vyakula.
• Jeli ya kifalme: (Hiki ni kitu chenye wingi wa madini ya protini ambacho nyuki wafanya kazi hutumia kulisha viluwiluwi katika kipindi cha awali cha kukua na viluwiluwi vya nyuki malkia katika vipindi vyao vyote vya kukua) Nyuki wafanyakazi wachanga ndio hutoa jeli ya kifalme ili kulisha viluwiluwi wachanga na nyuki malkia aliyekomaa.Jeli ya kifalme hutumiwa kama nyongeza kwa vyakula,na kama kiambato katika bidhaa za vyakula,dawa,vipodozi na kwa lishe ya wanyama.
• Sumu: Nyuki hutoa sumu wanapouma kama njia ya kujilinda.Sumu ya nyuki hutumiwa kama dawa kutibu mzio unao sababishwa na kuumwa kwa nyuki.
4.0 Ufugaji wa nyuki kama shughuli muhimu
Ufugaji wa nyuki ni shughuli,I nayowiiana vyema na miradi mingine ya maendeleo ya ukulima na mashambani. Miradi ya maendeleo katika maeneo pia hutoa uwezekano kwa utekelezaji wa ufugaji wa nyuki. Mimea fulani ikipandwa katika miradi Kama hii inaweza kuzalisha asali kwa mfugaji wa nyuki vile vile kunufaika kutoka kwa shughuli za uchavushaji za nyuki.Ufugaji wa nyuki unaweza kumtolea kipato cha ziada mkulima mdogo anayepanda mimea hii ama ana nyuki karibu.
Mimea ifuatayo inajulikana kwa kuwa ya manufaa kwa uchavushaji wa wadudu.Ile iliyowekwa alama ya nyota pia ni vyanzo vizuri vya mbochi kwa nyuki wanaotoa asali.
Mkonge,korosho,chai,paipai,nazi,kahawa,boga,tango,mawese,lichi,mchungwa/mdimu/mlimau,tufaha,parachichi,klova,tikitimaji,mpichi,mberimweusi ufuta,alizeti,maharage ya soya(baadhi ya aina) na alfalfa.
Mimea hunufaika kutoka kwa uchavushaji wa wadudu kwa ongozeko la seti ya mbegu.Hii husababisha ongezeko la mbegu na matunda ya hali ya juu.Nyuki ni wa manufaa kama wachavushaji katika hizo sehemu ambazo wadudu halisi wa uchavushaji hawapatikani ama hawatoshi kuchavusha sehemu kubwa zilizotengewa mmea mmoja.(kumbuka hata hivyo nyuki hawavutiwi na mimea yote)
Watu wanaojihusisha na na miradi ya misitu huwa wanavutiwa sana na ufugaji wa nyuki.Ufugaji wa nyuki ni kazi inayoleta mapato ikiwekwa kwenye raslimali ya msiti,hata hivyo sio haribifu kwa rasilmali hiyo.Mtu anayepata kipato kutoka kwa ufugaji wa nyuki kwa haraka anaweza kuwa mtetezi wa uhifadhi wa raslimali ya msitu.Ufugaji wa nyuki pia unapunguza uwezekano wa mto wa vichaka inayoashwa na wawindaji wa nyuki wanapochoma nyuki kutoka kwenye koloni za mbugani. Aina ya miti inayotumiwa katika juhudi za upandaji wa misitu ambayo ni chakula kizuri cha nyuki inaweza kuhusika katika uanzishaji wa kiwanda cha ufugaji wa nyuki. Ufugaji wa nyuki ni sehemu ya kutumia rasilmali ya msitu yenye maiumizi chungu mzima.
Miti inayotumika kwa madhumuni ya kuni,kinga ya mimea na kivuli,pia hutoa mbochi wa kutosha kuzalisha asali katika maeneo mengine.Kama ilivvyo utokaji wa mbochi hutegemea mambo mengi(tabia ya nchi(hali ya joto,baridi ,mvua n.k),hali ya anga na ardhi),mti labda hauwezi kuwa mtoaji mzuri wa mbochi unapopelekwa katika eneo jipya.Angalia ikiwa aina ya mti ni nzuri katika utoaji wa mbochi katika hali utakaokuwa ukimea kabla ya kupigania utumizi wake kama chanzo kizuri cha mbochi kwa nyuki.
5.0 Ufugaji wa nyuki
Ufugaji wa nyuki ni shughuli muhimu inayosaidia jamii kujipatia mapato ya ziada ili kuboresha maisha yao. Nchini Tanzania, takriban asilimia 90 ya ardhi inafaa katika ufugaji wa nyuki.
Ufugaji wa nyuki ni mfumo wa kilimo unaohimili na wenye manufaa kwa mazingira. Ufugaji wa nyuki huwapatia watu walio ndani ya umaskini mapato ya ziada ya mara kwa mara,husaidia mazingira na huwa na manufaa mengine:
• Si ghali. Watu binaafsi ama mashirika ya kibinafsi kama makanisa,makundi ya wanawake,makundi ya vijanasna vyama vya mashirika vinaweza kuanza na kiasi kiodogo cha pesa.
• Haihitaji ulishaji wa jumla wa nyuki kwani nyuki hujitafutia chakula chao kwa mwaka mzima.
• Mizinga inaweza kutengenezwa na mafundi wa humu nchini ingawaje baadhi ya vifaa vinafaa kuagizwa kutoka ng’ambo.
• Haihitaji ardhi, kwa hivyo wale wenye rasilmali chache wanaweza kushiriki.
6.0 Kushiriki kwa Jamii katika ufugaji wa nyuki
Ingawaje ufugaji wa nyuki unachukuliwa kuwa shughuli ya mtu binafsi,imeleta wakulima wengi pamoja katika jamii nyingi,kugawana vifaa na kujifunza mengi kutoka kwa matukio yao.Katika baadhi ya vijiji,wafugaji wa nyuki wamekuja pamoja kuunda makundi na vyama.Mafunzo waliojifunza kwa kufanya kazi,pamoja imetumika katika maisha yao.+
7.0 Viota na mizinga ya nyuki
Kiota cha nyuki kina mfululizo wa masega ya nyuki yaliyo sambamba, kila sega likiwa na mistari ya nta ndani ya vyumba vya kuhifadhia asali,chavua, ama vya kukulia viwiliwili vya nyuki.Vyumba hivi vina umbo la pembe sita.Masega haya ni changamani na hutumiwa na nyuki kuwatunza watoto wao,kuhifadhi asali na kumlinda malkia.mzinga ni chombo chochote ambacho hutolewa kama makaazi kwa nyuki watoao asali.Wazo ni kuwahimiza nyuki kujenga viota vyao kwa njia ambayo ni rahisi kwa mfugaji wa nyuki kudhibiti na kuvuna masega ya asali.Mizinga ya nyuki ienaweza kugawanywa katika makundi matatu –kitamaduni,fremu inayosonga na mzinga wa kisasa wa teknolojia finyu.
• Mizinga ya kitamaduni ni ile ambayo imetengenezwa nchini kwa kutumia vitu tofauti,magogo yenye shimo kwa sehemu ya ndani ama chungu,lakini unapotoa asali,nta ,nyuki wengi huuawa.
• Mizinga yenye viunzi ni ile yenye viunzi ambavyo nyuki ujenga masega kulingana na nafasi iliyopo katika viunzi. Mizinga hii ni bora kuliko mizinga ya kitamaduni kwa kuzalisha asali nyingi na nta bora pia wakati wa kuvuna nyuki hawauwawi .Gharama za utengenezaji wa mizinga hii ni nafuu na mafundi seremala vijiji wanamudu kutengeneza mizinga hii.
• Mizinga yenye Fremu (mizinga ya ghorofa) inayosonga ni njia iliyoendelea ya kufuga nyuki. Hii hutumiwa kuzalisha asali maradufu kila msimu na kupunguza usumbufu kwa koloni ya nyuki. Idadi kubwa nyuki inaweza kuwekwa katika mzinga wa aina hii; hifadhi ya asali huwa kwa haraka wakati wa msimu wa maua. Ili kuunganisha udhibiti na ufanisi wa mavuno katika mzinga wenye fremu inayosonga,na manufaa ya kutokuwa ghali kutoka kwa mizinga ya kitamaduni. Nyuki wanahimizwa kucjenga masega chini ya mfululizo wa pao za juu. Pao hizi huruhusu kila sega kubebwa kutoka kwenye mzinga na mfugaji wa nyuki. Mizinga ya teknolojia finyu inaweza kutengenezwa ukitumia raslimali zinazopatikana nyumbani.

8.0 Kuvuna Asali na Nta
Asali huvunwa mwisho wa msimu wa maua. Mfugaji wa nyuki huchagua masega yenye asali iliyokomaa ,iliyofunikwa na rusu laini ... Vifaa Vingi vya vifaa vinavyohitajika kwa ufugaji mdogo wa nyuki vinaweza kutengenezwa na mafundi vijijini. Smoker ...
9.0 Matatizo ya uzalishaji
• Ukosefu wa ujuzi na jinsi ya kupata vifaa na mbinu bora
• Mazao yenye ubora duni kutoka kwa wafugaji wengi.
• Kutokuwepo kwa utaratibu wa udhibiti ukaguzi wa ubora wa mazao
• Kutokuwepo kwa msaada kwa wafugaji nyuki
• Upatikanaji wa mitaji kwa watu wanaojishughulisha na shughuli zote za ufugaji nyuki.
10.0 Matatizo ya Masoko
• Ukosefu wa taarifa za masoko ya ndani na nje ya nchi.
• Ukosefu wa huduma za usafirishaji wa mazao ya nyuki kutoka maeneo mbalimbali ya uzalishaji.
• Uuzaji wa asali na nta ghafi badala ya mazao yaliyoongezwa thamani.
• Kukosekana kwa utaratibu muafaka wa ulipaji wa kodi na ada kisheria kwa sababu ya ukosefu wa uratibu kati ya serikali na taasisi za kibiashara.
11.0 Kwa wakati huu kuna mifumo mikuu mitatu inayotumika katika uzalishaji na masoko ya mazao ya nyuki.
a) Wafugaji nyuki wengi hufanya kazi kila mtu peke yake bila kupata msaada wa vitendeakazi na namna ya kufikisha mazao yako kwenye masoko.
b) Wafugaji nyuki mmoja mmoja hujiunga katika vikundi ambavyo hujiunga pamoja kuunda vyama vya ushirika. Vyama hivi hutoa misaada mingi ikiwa ni pamoja na usafiri na vifaa vya kuhifadhia mazao ya nyuki.
c) Wapo wawekezaji Wakubwa binafsi huwapa wafugaji nyuki huduma zote wanazohitaji ili wazalishe na kuchakata asali yenye viwango vya juu vya ubora. Uzalishaji na masoko vinaweza kuboreshwa kwa kiwango cha juu kwa kuboresha mfumo wa (a) na (c).

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ