• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Wednesday, July 27, 2016

Yanga Yaaga Michuano Ya Kombe La Shirikisho Kwa Kipigo Cha 3-1 Dhidi Ya Medeama

No comments:
 
Mabingwa wa soka wa Tanzania, Yanga ya Dar-es-salaam, imekubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Medeama FC ya nchini Ghana na hivyo kimsingi kuiaga michuano ya Kombe la Shirikisho la Chama Cha Soka barani Afrika (CAF).
Katika mchezo huo wa marudiano uliofanyikia katika Uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi-Takoradi huko Ghana, Yanga ilikubali magoli hayo matatu yaliyofungwa na Daniel Amoah dakika ya saba aliyemalizia kona ya Enock Atta Agyei na Abbas Mohammed mawili dakika ya 23 na 37, wakati la Yanga lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 25 kwa penalti baada ya Obrey Chirwa kuangushwa kwenye boksi.
Kwa ujumla Yanga haijafanya vizuri katika michuano hii. Katika michezo minne iliyocheza, Yanga imefungwa mitatu na kutoka sare katika mchezo mmoja. Yanga ilianza kwa kufungwa na 1-0 na Mo Bejaia nchini Algeria kabla ya kufungwa tena 1-0 na TP Mazembe na kutoka sare ya 1-1 na Medeama mjini Dar es Salaam kabla ya kukubali kipigo cha leo ambacho ni kikubwa kwa Yanga.
Matokeo hayo yanamaanisha kwamba TP Mazembe ambao kesho wanapambana na Mo Bejaia mjini Lubumbashi wanaendelea kuongoza kundi hilo. Wanafuatiwa na Mo Bejaia na Medeama. Michezo ya Yanga iliyobakia itakuwa ni ya kukamilisha tu ratiba kwani hakuna tena matumaini ya kusonga mbele.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ