jeshiniphoto1.    Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linawatangazia vijana wa Kitanzania wito wa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya pili na Vijana wa Kujitolea.
2.    Vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo ni kama ifuatavyo:-
      a.   Vijana wa Mujibu wa Sheria Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.
Kundi hili linahusisha wanafunzi wote waliomaliza kidato cha sita mwezi Mei mwaka 2016, ambao hawakuchaguliwa kwenye mafunzo ya JKT Mujibu  wa Sheria Operesheni Magufuli awamu ya kwanza na hawakupata nafasi ya kujiunga vyuo vya elimu ya juu. Aidha, orodha kamili ya majina na makambi waliyopangiwa inapatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Kujenga Taifa, ambayo ni www.jkt.go.tz  na Tovuti Kuu ya Serikali www.tanzania.go.tz
      b.      Vijana wa Kujitolea
Kundi hili linahusisha Vijana wote waliosailiwa mwezi Mei na  Juni mwaka 2016 katika ngazi za wilaya na mkoa  na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.
3.   Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na Kujitolea wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT waliyopangiwa wakiwa na vifaa vifuatavyo:
a.  Bukta ya rangi ya bluu iliyokoza (Dark blue) yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma isiyo na zipu, iwe na urefu  unaoishia magotini.
b.  Raba ngumu za michezo zenye rangi ya kijani au nyeusi.
c.  Shuka jozi mbili za kulalia zenye rangi ya bluu bahari ukubwa wa 4×6.
d.  Soksi za michezo jozi mbili rangi nyeusi.
e.  Chandarua moja ya duara rangi ya bluu au kijani ukubwa wa 4×6.
f.  Nguo za michezo (truck suit) jozi moja rangi ya kijani au bluu.
g.  Fulana (T-shirt) ya kijani isiyokuwa na maandishi yoyote.
h.  Mavazi hayo yasiwe ya kubana mwili.
4.  Inasisitizwa kuwa vijana wa kujitolea wanaotakiwa kuripoti makambini ni wale tu waliopita katika usaili kwenye ngazi
za wilaya na mikoa na kuchaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT.

5.  Vijana hao wa Mujibu wa Sheria na  Kujitolea wanatakiwa kuripoti kwenye makambi ya JKT waliyopangiwa kuanzia
tarehe 01 mpaka 05 Desemba 2016 kwa kujitegemea nauli ya kwenda na kurudi.

BOFYA JINA LA KIKOSI HAPO CHINI  KUANGALIA MAJINA YA VIJANA KWA MUJIBU WA SHERIA AWAMU YA PILI  2016  

BULOMBORA JKT-KIGOMA                           RWAMKOMA JKT -MARA                  MSANGE JKT-TABORA

KANEMBWA JKT-KIGOMA                                  MTABILA-KIGOMA                      RUVU JKT-PWANI

MAKUTUPORA JKT- DODOMA                      MGAMBO JKT-TANGA              MARAMBA JKT- TANGA

MAFINGA JKT- IRINGA                                         MLALE JKT -RUVUMA


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya JKT
Tarehe 17 Novemba 2016