Madhumuni
makubwa ya kozi hii ni kuwapatia vijana wanaofanya biashara ndogondogo
uwezo wa kujenga stadi katika ujasiriamali na kuongeza kipato.
YALIYOMO
1. Kuunda Vikundi
VIKUNDI ni muungano wa watu wenye nia moja wakiwa na dhamira madhubuti kuweza kukabiliana na changamoto zinazo wakabili. Changamoto hizo zinaweza kuwa za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Muundo mzuri wa vikundi.
3. Masoko
Soko ni utaratibu au mtindo uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji, na Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake. Kozi hii itakusaidia kufikiri ki- masoko na kuelewa mbinu za masoko, utafiti wa soko.
4. Ujasiriamali Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na i) Ujasiri au mshawasha wa kuwa na mali.
5. Biashara Biashara ni pamoja na hali ya kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza utaalam. Wito na makubaliano ya kipekee yenye lengo la kibiashara kwa nia ya kupata faida. Kulingana na sera ya taifa ya biashara ya mwaka 2003 mgawanyo wa biashara kwa wajasiamali ni kama ifuatavyo:
5.1 UAMUZI WA KUFANYA BIASHARA
Unategemea Sana: _
BIASHARA YA KUTOA HUDUMA KATIKA JAMII
Aina hii ya biashara inafanywa na watu wachache sana,na ambao wepesi kuangalia fursa katika jamii wanayoishi.Biashara ya kutoa huduma katika jamii unakuwa umeisaidia jamii kupata kitu ambacho kilikuwa adimu katika eneo hilo na pia wewe unapata faida kupitia huduma unayoitoa,mfano wa biashara hii ni kuchimba kisima,kuanzisha taasisi ambayo itakuwa inasaidia Vijana,walemavu wa viungo,kusafisha mitaro n.k.
5.3. MATUMIZI YA FEDHA ZA BIASHARA
Hakikisha unatumia chanzo cha mapato Kwa matumizi ya mpango uliokusudia tu si kwa vinginevyo (zitumike kwa ajili ya biashara tu)
Matumizi ya fedha biashara
Wafanyabiashara wengi hawatofautishi kati ya matumizi mtu binafsi na matumizi ya biahara hivyo kusababisha biashara kufa au kutoendelea.
Kiutendaji mfanyabiashara anakuwa ameshika vikapu viwilivilivyo na fedha ya biashara naya familia.kimsingi hautakiwi kuchanganya vikapu hivi. Mfanyabiashara lazima ajilipe mshahara.
Matumizi ya fedha katika familia/binafsi
a) Dola
b) Mteja/wateja
c) Benki
d) Wafanyakazi/vibarua
e) Msambazaji/muuzaji malighafi
5.6. SABABU ZA BIASHARA KUFA
a) Kukosamtaji wa kutosha kuendesha biashara
b) Kukosa uelewa wa biashara
c) Udhaifu wa uongozi
d) Kuweka biashara sehemu isiyofaa
e) Ushindani mkali
f) Sheria
g) Majanga na maafa
h) Taratibu mbaya
i) Kukosa dhana ya kumjali mteja
j) Kutotambua fursa
k) Kuwa tegemezi
5.7.JINSIA NA BIASHARA
1. Jinsia ni nini?
Jinsia ni mwingiliano/ mahusiano ya kijamii katika jumuia, kiuchumi, kiutamaduni n.k
2.Madhumuni
a) mume hataki mkewe afanye biashara
b) jamii kuwa na mtazamo mbaya inapotokea wanawake kutaka kuingia ubia na wafanya biashara wanaume
c) kukataliwa kuingia mikataba yoyote kama mikopo n.k bila kibali cha mumewe
d) wazazi wa ndugu wa mwanaume kuingilia maisha ,( inakuwa mbaya zaidi wanapokuwa hawamkubali mwanamke huyo katika ukoo wao)
e) kazi za nyumbani zifanywe na mwamke pekee bila ksidiwa na mumewe.
4.Ninini kifanyike ilikuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia
a) kuhimiza jamii kwamba kila mmoja anao uwezo wa kufanya kazi ya maana anapowekwa kwenye mazingira yanayomwezesha
b) kutoa elimu kwa jamii kuachana na mila na mtazamo potofu kuhusu jamii ya kike
c) kuhamasisha jamii ya kike ielewe kwamba inapaswa kuwa na mipangilio ya maisha bila kutegemea mawazo kutoka nje
d) wanawake wakuze kujiamini na kujituma
6. Mtaji
Hapa tunajumuisha aina zote za uzalishaji ambazo zinaweza kutumika katika ubunifu unaoweza kuongeza thamani katika bihaa au huduma inayotolewa .Yaani njia ya kukufikisha au haki uliyo nayo juu ya aina ya mtaji utakayoitumia kutengeneza/kuzalisha faida. Hizi zinaweza kuwa kigezo cha ofisi, zana, fedha.
7. Haki Miliki/Hataza
Haki miliki ni haki ya umiliki wa jumla inayotolewa na serikali kwa ugunduzi au kwa umiliki kwa kipindi maalumu. Kwa kawaida ni kipindi cha miaka 20 tangu umiliki ukabidhiwe kwa muhusika. Ni muhimu kama mjasiriamali kuwa na umiliki wa biashara yako.
8. Kupanga gharama na Bei
Pata uelewa na kupanga gharama mbalimbali katika biashara zako (gharama za moja kwa moja na gharama zisizo za moja kwa moja) na kuelewa jinsi ya kupanga bei ya bidhaa yako ili kupata faida na biashara yako kuendelea kukua.
9. Kuweka Kumbukumbu
Ni muhimu kuweka kumbukumbu ya biashara zako ili kukusaidia kutambua mwelekeo wa biashara yako. Pia inakusaidia kuweza kusaidika na wafanyabiashara wengine kama taasisi za kifedha. Muundo mzuri wa kuweka kumbukumbu zako ni kama huu .

2. Andiko la Biashara
Mpango wa biashara ni kauli rasmi
ya seti ya malengo ya biashara na mpango kwa ajili ya kufikia malengo
hayo.Andiko hili la biashara huonyesha pia fursa zilizopo, rasilimali na
jinsi vitakavyotumika ,mpangilio mzima wa kutekeleza biashara ikiwa ni
pamoja na uongozi na usimamizi wa biashara kwa hapo baadaye kwa upande
wa kitaasisi na kifedha.
Soko ni utaratibu au mtindo uliowekwa kwa mujibu wa kanuni /sheria kumwezesha mfanya biashara kuuza bidhaa zake kwa wateja/walaji, na Masoko ni shughuli yoyote ile anayofanya mfanyabiashara ili kuimarisha biashara yake. Kozi hii itakusaidia kufikiri ki- masoko na kuelewa mbinu za masoko, utafiti wa soko.
4. Ujasiriamali Neno ujasiriamali linatokana na maneno mawili ambayo ni UJASIRI na MALI hivyo maana ya ujasiriamali ni kuwa na i) Ujasiri au mshawasha wa kuwa na mali.
5. Biashara Biashara ni pamoja na hali ya kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza utaalam. Wito na makubaliano ya kipekee yenye lengo la kibiashara kwa nia ya kupata faida. Kulingana na sera ya taifa ya biashara ya mwaka 2003 mgawanyo wa biashara kwa wajasiamali ni kama ifuatavyo:
5.1 UAMUZI WA KUFANYA BIASHARA
Unategemea Sana: _
- Upatikaji wa malighafi
- Soko la bidhaa na matakwa ya wateja
- Gharama za uendeshaji wa biashara
- Biashara inahitaji ubia au peke yako
- Taratibu za usajiri
- Ni bidhaa ipi unataka kuuza
- Ni wateja wa aina gani unaowalenga
- Unajitofautishaje na washindani wako
- Ubora wa bidhaa yako
- Mjali mteja (kumbuka kuwa mteja ndio mwanzo na mwisho wa biashara yako)
BIASHARA YA KUTOA HUDUMA KATIKA JAMII
Aina hii ya biashara inafanywa na watu wachache sana,na ambao wepesi kuangalia fursa katika jamii wanayoishi.Biashara ya kutoa huduma katika jamii unakuwa umeisaidia jamii kupata kitu ambacho kilikuwa adimu katika eneo hilo na pia wewe unapata faida kupitia huduma unayoitoa,mfano wa biashara hii ni kuchimba kisima,kuanzisha taasisi ambayo itakuwa inasaidia Vijana,walemavu wa viungo,kusafisha mitaro n.k.
5.3. MATUMIZI YA FEDHA ZA BIASHARA
Hakikisha unatumia chanzo cha mapato Kwa matumizi ya mpango uliokusudia tu si kwa vinginevyo (zitumike kwa ajili ya biashara tu)
Matumizi ya fedha biashara
- Mshahara
- Kodi ya sehemu ya biashara
- Matangazo
- Mafunzo
- Kulipa madeni ya biashara na riba
- Kodi
- Leseni ya biashara
- Akiba
- Ununuzi wa mali ghafi na vitendea kazi
Wafanyabiashara wengi hawatofautishi kati ya matumizi mtu binafsi na matumizi ya biahara hivyo kusababisha biashara kufa au kutoendelea.
Kiutendaji mfanyabiashara anakuwa ameshika vikapu viwilivilivyo na fedha ya biashara naya familia.kimsingi hautakiwi kuchanganya vikapu hivi. Mfanyabiashara lazima ajilipe mshahara.
Matumizi ya fedha katika familia/binafsi
- Chakula
- Matibabu
- Elimu
- Nyumba
- Usafiri
- Akiba
- Mikopo na misaada kwa rafiki/ndugu
- Kulipa madeni binafsi
- Tahadhali
a) Dola
b) Mteja/wateja
c) Benki
d) Wafanyakazi/vibarua
e) Msambazaji/muuzaji malighafi
5.6. SABABU ZA BIASHARA KUFA
a) Kukosamtaji wa kutosha kuendesha biashara
b) Kukosa uelewa wa biashara
c) Udhaifu wa uongozi
d) Kuweka biashara sehemu isiyofaa
e) Ushindani mkali
f) Sheria
g) Majanga na maafa
h) Taratibu mbaya
i) Kukosa dhana ya kumjali mteja
j) Kutotambua fursa
k) Kuwa tegemezi
5.7.JINSIA NA BIASHARA
1. Jinsia ni nini?
Jinsia ni mwingiliano/ mahusiano ya kijamii katika jumuia, kiuchumi, kiutamaduni n.k
2.Madhumuni
- Kutambua nafasi na umuhimu wa kila jinsi katika biashara
- jinsia ya kike inavyoweza kuathirika zaidi katika biashara ukilinganisha na ile ya kiume
- kuwaasa wanawake wasikate tamaa kwa kutendewa tofauti na wanaume katika biashara na jinsi ya kukabiliana na vitisho
a) mume hataki mkewe afanye biashara
b) jamii kuwa na mtazamo mbaya inapotokea wanawake kutaka kuingia ubia na wafanya biashara wanaume
c) kukataliwa kuingia mikataba yoyote kama mikopo n.k bila kibali cha mumewe
d) wazazi wa ndugu wa mwanaume kuingilia maisha ,( inakuwa mbaya zaidi wanapokuwa hawamkubali mwanamke huyo katika ukoo wao)
e) kazi za nyumbani zifanywe na mwamke pekee bila ksidiwa na mumewe.
4.Ninini kifanyike ilikuleta mabadiliko ya usawa wa kijinsia
a) kuhimiza jamii kwamba kila mmoja anao uwezo wa kufanya kazi ya maana anapowekwa kwenye mazingira yanayomwezesha
b) kutoa elimu kwa jamii kuachana na mila na mtazamo potofu kuhusu jamii ya kike
c) kuhamasisha jamii ya kike ielewe kwamba inapaswa kuwa na mipangilio ya maisha bila kutegemea mawazo kutoka nje
d) wanawake wakuze kujiamini na kujituma
6. Mtaji
Hapa tunajumuisha aina zote za uzalishaji ambazo zinaweza kutumika katika ubunifu unaoweza kuongeza thamani katika bihaa au huduma inayotolewa .Yaani njia ya kukufikisha au haki uliyo nayo juu ya aina ya mtaji utakayoitumia kutengeneza/kuzalisha faida. Hizi zinaweza kuwa kigezo cha ofisi, zana, fedha.
7. Haki Miliki/Hataza
Haki miliki ni haki ya umiliki wa jumla inayotolewa na serikali kwa ugunduzi au kwa umiliki kwa kipindi maalumu. Kwa kawaida ni kipindi cha miaka 20 tangu umiliki ukabidhiwe kwa muhusika. Ni muhimu kama mjasiriamali kuwa na umiliki wa biashara yako.
8. Kupanga gharama na Bei
Pata uelewa na kupanga gharama mbalimbali katika biashara zako (gharama za moja kwa moja na gharama zisizo za moja kwa moja) na kuelewa jinsi ya kupanga bei ya bidhaa yako ili kupata faida na biashara yako kuendelea kukua.
Katika
hili hakuna kanuni imara sana, wala hakuna namna moja tu bora ya
kupanga bei, ila viko viashiria mbalimbali ambavyo vinaweza kusaidia. Ni
suala tu la kugundua bei ipi inayofaa kwa kuzingatia kwa uangalifu
vigezo mbalimbali.
Kupanga
bei ni suala muhimu sana katika maamuzi ya masuala ya masoko. Bei
unayotoza kwa bidhaa/ huduma yako inaathiri moja kwa moja faida (au
hasara) utakayopata.
Pamoja na umuhimu wote huo wa kupanga bei kwa umakini, uko ushahidi kuwa wajasiriamali wengi hawatilii mkazo suala la upangaji wa bei. Matatizo yanayotokana na kutokuwa makini katika kupanga bei ni kuwa na faida ndogo katika baadhi ya bidhaa, hasara katika uuzaji wa bidhaa hizo kutokana na kuongezeka kwa gharama, na kushindwa kupanga bei upya. Mbaya zaidi, upangaji bei usio makini unaweza kutofautisha kati ya kupata faida au kupata hasara.
Mambo ambayo yanaathiri bei zako yanaweza kugawanywa katika makundi manne yafuatayo:
• Gharama zako
• Mkakati wako wa masoko
• Udhibiti wa bei
• Hali ya soko
Ni dhahiri kuwa bei utakayopanga itapaswa kufidia gharama zote za kuendesha biashara yako.
Kufahamu gharama zako
Gharama za kuendesha biashara zinaathiri kwa kiwango kikubwa bei utakayotoza kwa hiyo bidhaa. Ikiwa utaweza kufahamu gharama zote zilizotumika katika kuzalisha bidhaa hiyo, utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kutoza bei yenye uhalisia. Hata hivyo, si jambo rahisi sana kukokotoa kwa usahihi kiasi cha gharama za bidhaa iliyozalishwa.
Ni rahisi kufahamu kiasi cha malighafi iliyotumika na gharama yake, au gharama uliyonunulia bidhaa unayouza, lakini bado linabaki suala la gharama nyinginezo. Gharama kama vile za mishahara ya wafanyakazi, Kodi ya jengo, Umeme, maji na nyinhgine nyingi lazima kuzingatia wakati wa kupanga bei.
Aina za gharama
Ili kuweza kuweka makadirio ya gharama katika hatua mbalimbali za uzalishaji tunahitaji kuelewa tabia za gharama mbalimbali kuendana na kiwango/ kiasi cha uendeshaji biashara. Kuwa iwapo biashara itakuwa kubwa gharama hizo zitaongezeka, zitapungua, au hazitabadilika. Kwa kuzingatia tabia ya gharama kuendana na kiwango cha biashara, tuna gharama zisizobadilika na gharama zinazobadilika.
Gharama zisizobadilika: hizi ni zile ambazo hazibadiliki hata kama mjasiriamali atazalisha bidhaa nyingi kwa pamoja. Gharama hizi ni lazima zilipwe kwa kiwango kile kile bila kuzingatia mabadiliko yoyote katika kiwango/idadi cha uzalishaji, yaani hamna tofauti ya gharama hizi katika kuzalisha bidhaa moja au kuzalisha bidhaa 1000.
Mifano ni kama Kodi (pango), uchakavu, riba, na bima
Gharama zinazobadilika kutegemeana na kiwango cha uzalishaji/mauzo. Hizi ni zile ambazo ukiongeza uzalishaji kufikia idadi ya vitu 1000 na gharama za uzalishaji zitaongezeka kuwa mara mbili ya ulizotumia wakati ukitengeneza vitu 500.
Mifano ni kama bei ya manunuzi, gharama za malighafi na ujira wa wafanyakazi walioko katika uzalishaji.
Kuzitambua gharama
Hatua ya kwanza katika kukokotoa gharama ni kutambua aina za gharama mbalimbali zilizochangia katika uzalishaji wa bidhaa , au bidhaa iliyouzwa, au huduma iliyotolewa. Ili ufanye hivyo, ni vema kuainisha gharama katika gharama za moja kwa moja na gharama zisizo za moja kwa moja

Gharama
za moja kwa moja ni gharama ambazo ni rahisi kufuatiliwa kuona mchango
wake katika bidhaa au shughuli fulani. Mifano ni kama bei ya kununulia
bidhaa, gharama za vibarua, gharama za malighafi. Mara nyingi gharama
hizi hubadilika kadri ya kiwango/kiasi cha uzalishaji, mauzo, au huduma
zinazotolewa. Gharama za moja kwa moja zimegawanyika katika gharama moja
kwa moja za malighafi na gharama moja kwa moja za ujira.
Gharama zisizo za moja kwa moja Hizi ni gharama ambazo haiwezekani kufuatilia na kujua mchango wake moja kwa moja katika uzalishaji wa bidhaa fulani.
Mifano ni pamoja na gharama za kifedha, matangazo, utawala.
Gharama zisizo za moja kwa moja haziwezi kuonekana/ kuhusishwa moja kwa moja na bidhaa inayozalishwa au kuuzwa, au huduma inayotolewa. Mara nyingi hazibadiliki kuendana na kiwango cha uzalishaji/ mauzo. Badala yake, kiasi cha gharama hizi huwa kile kile kwa kila kipindi husika. Gharama hizi zimegawanyika katika gharama za mauzo, za kifedha, na za kiutawala.
Baadhi ya mifano ya gharama zisizo za moja kwa moja kwa biashara ndogo ni kama:
• Kodi (pango)
• Mishahara
• Riba
• Gharama za matumizi mbalimbali ya ofisi
Gharama zisizo za moja kwa moja Hizi ni gharama ambazo haiwezekani kufuatilia na kujua mchango wake moja kwa moja katika uzalishaji wa bidhaa fulani.
Mifano ni pamoja na gharama za kifedha, matangazo, utawala.
Gharama zisizo za moja kwa moja haziwezi kuonekana/ kuhusishwa moja kwa moja na bidhaa inayozalishwa au kuuzwa, au huduma inayotolewa. Mara nyingi hazibadiliki kuendana na kiwango cha uzalishaji/ mauzo. Badala yake, kiasi cha gharama hizi huwa kile kile kwa kila kipindi husika. Gharama hizi zimegawanyika katika gharama za mauzo, za kifedha, na za kiutawala.
Baadhi ya mifano ya gharama zisizo za moja kwa moja kwa biashara ndogo ni kama:
• Kodi (pango)
• Mishahara
• Riba
• Gharama za matumizi mbalimbali ya ofisi
9. Kuweka Kumbukumbu
Ni muhimu kuweka kumbukumbu ya biashara zako ili kukusaidia kutambua mwelekeo wa biashara yako. Pia inakusaidia kuweza kusaidika na wafanyabiashara wengine kama taasisi za kifedha. Muundo mzuri wa kuweka kumbukumbu zako ni kama huu .
Namna za kutunza kumbukumbu za kifedha
Kumbukumbu
za kifedha zinaweza kutunzwa katika mfumo wa kuandika kwa mikono katika
vitabu vya fedha, au kutumia mfumo wa kompyuta ambapo unaweza kutumia
mojawapo ya programu za kihasibu za kompyuta.
Namba mbili kuu za utunzaji wa kumbukumbu za fedha ni:
- Kurekodi kwa kuzingatia miamala ya fedha taslimu tu
- Kurekodi kwa kuzingatia msingi wa muamala, hata ikiwa ni deni
Mfumo wa kurekodi fedha taslimu tu
Hii ni namna rahisi sana ya kutunza kumbukumbu za kifedha na haihitaji ujuzi wa juu katika utunzaji wa mahesabu. Sifa zake ni:
- i) Malipo yanaandikwa kwenye jedwali la fedha taslimu mara yanapofanyika, kadhalika makusanyo pia yanaandikwa katika jedwali hilo mara yanapotokea.
- ii) Mfumo huu haujishughulishi na malipo yaliyofanyika kwakati uliopita, au kiasi cha malipo ambayo bado yanadaiwa.
iii) Mfumo huu hauweki moja kwa moja kumbukumbu za madeni au mali za biashara
- iv) Mfumo huu hautunzi kumbukumbu za miamala isiyohusisha fedha taslimu moja kwa moja, mfano Uchakavu wa mitambo. .
Mfumo wa kutambua madeni katika kuweka kumbukumbu
Huu
ni mfumo rasmi wa kihasibu unaoweka kumbukumbu kwa kutambua na kuandika
pande mbili za kila muamala unaofanyika, ambazo zinahusisha kutoa na
kupokea.
Pande
mbili za jedwali hutumika, yaani upande wa kushoto na upande wa kulia.
Mfumo huu ni wa kisasa na unahitaji ujuzi wa kanuni za kihasibu.
- i) Matumizi/ gharama huandikwa kwenye kitabu kikuu cha mahesabu pale biashara inapoingia gharama hizo, na sio kusubiria hadi zitakapolipwa. Hali kadhalika, mapato hutambulika na kuingizwa kwenye vitabu pale biashara inapoyapata, na sio kusubiria hadi fedha hizo zikusanywe.
- ii) Mfumi huu unajishughulisha na aina zote za miamala.
iii) Mfumo huu hupelekea kuwa na taarifa sahihi ya mali na madeni ya biashara.
Kumbukumbu
katika mfumo huu huwa na jedwali la mapato na matumizi, ambalo
hujumuisha mapato na matumizi yote yaliyofanyika kwa kipindi fulani,
pamoja na taarifa ya hali ya kifedha ambayo huonesha, licha ya mambo
mengine, madeni inayodai na kudaiwa biashara katika siku ya mwisho ya
kipindi hicho.
Mifano ya nyaraka muhimu zinazotunzwa ni:
- Jedwali la fedha taslimu/ zilizoko benki
- Vocha (Makusanyo, Malipo na kitabu cha kumbukumbu)
- Rajisi ya malipo ya awali
- Taarifa ya benki/ uoanisho wa taarifa ya benki na taarifa ya fedha taslimu
No comments:
Post a Comment