• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Monday, September 17, 2012

Diamond Platinum: Aongea rasmi kuhusu uhusiano wake na Wema Sepetu

No comments:
 


Baada ya kuwepo na taarifa kuwa Diamond na Wema Sepetu wamerudiana na hata kuonekana pamoja mkoani Kigoma wakati wa ziara ya Kigoma All Stars, nyota huyo jana ameamua kufunguka rasmi kupitia website yake na kueleza ukweli.
"Najua watu wengi sana mnapenda Couple hii  na furaha yenu ni kutuona wawili sisi tukiwa kwenye Mahusiano ya kimapenzi.... na mmekua mkifurahi sana na story za hapa na pale mkiskia kua wawili sisi tumekua pamoja na hata pindi mkituona tuko pamoja pia Mmekua mkishangilia na kufurahi... bt ukweli ni kwamba Mimi na Wema hivi sasa si Wapenzi tumekua ni kama Dada na Kaka ama marafki tu wa kawaida ambao tunashirikiana katika kazi mbalimbali za sanaa na za n'nje ya sanaa, katika harakati za kujenga Taifa Letu... Pia ni vizuri ningependa mfahamu kwamba Wema ana Mpenzi wake ambae  namfaham na tunaheshimiana kama mtu na Shemeji yake........So das' de Truth abt me and Her!... and Get ready! kwa kazi tofautitofauti ambazo soon zitadondoka".
Ampiga kijembe Ommy Dimpoz kwa kufanya video Afrika Kusini?
Bongo Flava haijawahi kulipa kama inavyolipa sasa hivi. Hakujawahi kuwa na ushindani baina ya wasanii kama unavyoonekana sasa. Kwakuwa muziki wa Tanzania umeingia katika hatua kubwa ya kibiashara, wasanii wanaumiza vichwa kufanya ngoma na video kali kwa gharama yoyote wanayoweza kumudu ili kuendelea kukaa kileleni.
Hivi karibuni Ommy Dimpoz alisafiri hadi Johannesburg kwenda kufanya video yake ya ‘Baadaye’ japo story za kitaa zinadai kuwa video hiyo haijawashtua wengi, ni ya kawaida tu. Jumamosi ijayo Diamond atafanya usaili wa models watakaoonekana kwenye video yake mpya itakayofanyika hapa nchini na nje ya nchi. Kwa mujibu wa status yake ya Facebook ya jana Jumapili, Diamond anaonekana kama kumpiga kijembe cha kiaina mwanae Ommy Dimpoz aliyefunga safari hadi bondeni kupiga kioo chake.
“This is your opportunity to play roll in my new international music video. Will be shooting in Tanzania and abroad,off course not South Africa. Karibu at Nyumbani Lounge on 22nd Sept 11am for audition; bring your coolest bling on board. For more information or you can send your coolest photos to diamond@i-view-studios.com,” aliandika Diamond.
Hebu soma status ‘ndani ya mistari’ (read between the lines) utagundua Diamond kampiga dongo Ommy Dimpoz aliyekuwa na bajeti ndogo ya kufanya video Afrika Kusini. “Will be shooting in Tanzania and abroad,off course not South Africa!! Tumebold hiyo sentensi ili uigundue picha halisi. Maana ya Diamond ni kwamba, wasanii wengi wamekuwa wakifanyia video Afrika Kusini akiwemo Ommy, AY na Cpwaa, hivyo yeye anataka kuwaonesha kuwa ana bajeti kubwa zaidi ya zao na hivyo ana uwezo wa kufanya video ya gharama katika nchi zingine za mbele zaidi, mfano Marekani. Umeipata picha?
Aigharamia likizo ya madansa wake nchini Marekani

Speaking of US, hitmaker huyo ameamua kuwaacha dancers wake watatu nchini humo wafurahie bata na likizo fupi baada ya kuchapa kazi ipasavyo. Aliamua kutoka kauli hiyo baada ya kuwepo maswali kuwa huenda amewapiga chini. Kupitia website yake amesema, “nimeamua kuwaacha Marekani kwaajili ya mapumziko ya muda mfupi, ili waweze kurefresh akili na miili yao kwasababu kiukweli wamefanya kazi kubwa kwa muda mrefu na iliyozaa matunda makubwa...hivyo kwa upendo na heshima yangu kwao nikaona ni vizuri niwazawadie Mapumziko hayo Nchini AMERICA..... mbali na hayo kuna kingine kikubwa ambacho soon ntawajuza nini wanakifanya pia huko America ili wakirudi wazidi kuleta revolution katika Industry hii ya Muziki Africa...”

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ