• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Wednesday, October 17, 2012

Balozi wa Tanzania nchini Japan awakaribisha Watanzania Chakula cha jioni

No comments:
 

Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimkaribisha rasmi Waziri wa Fedha pamoja na ujumbe kutoka Tanzania kwa chakula cha usiku alichowaandia. kutoka kulia ni Mhe. William Mgimwa Waziri wa Fedha akifuatiwa na Waziri wa Fedha Zanzibar Mhe. Omary Yusuph Mzee akifuatiwa na Bw.Selivicius Likwilile Naibu Katibu Mkuu Wizara na Fedha na wengineo ni viongozi waliohudhuria hafla hiyo Jijini Tokyo – Japan.
Waziri wa Fedha Mhe. William Mgimwa akimshukuru Mhe. Balozi Salome Sijaona pamoja na mume wake Mzee Sijaona (aliye upande wa kulia kwa Mhe. Balozi Salome Sijaona) kwa mwaliko wa chakula cha usiku.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
Wajumbe wa mkutano wa IMF na WB wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona alipokuwa anatoa historia fupi ya ubalozi wa Tanzania.
Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe. Salome Sijaona akimwelezea Waziri wa Fedha Mhe William Mgimwa mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika katika Balozi zetu.
Afisa wa ubalozi Bi Agnes akiwakaribisha wageni chakula cha usiku hapo ubalozini jijini Tokyo Japan.
Wajumbe kutoka Tanzania wakishiriki chakula cha jioni pamoja na Balozi Mhe. Salome sijaona.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ