• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, October 26, 2012

Polisi yawataja wauaji wa Kamanda Barlow

No comments:
 
Picture
Pichani kulia ni Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba akiyataja majina ya watuhumiwa hao wa mauaji ya Kamanda Barlo,na shoto ni IGP Said Mwema.
JESHI la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.


Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza  na watu watano kutoka Dar es Salaam. Leo (jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert Manumba aliwataja watuhumiwa  hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi.

Wengine ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.


Wanaoshikiliwa jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50), Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.


Manumba amesema simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu, ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na hatimaye wahusika kukamatwa.


Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.


Marehemu Kamanda Barlow aliuawa  usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8 usiku katika eneo la Mianzi Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ