• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Monday, October 15, 2012

WANACHAMA, WADAU PPF, WATEMBELEA MBUGA YA WANYAMA TARANGIRE

No comments:
 


Mkurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kulia), akiongoza wanachama na wadau wa Mfuko huo kutembelea mbuga ya wanyama Tarangire, kilomita 120 kutoika Arusha mjini Jumamosi Oktoba 13, 2012. Wanachama na wadau hao walikuwa wakishiriki mkutano wa 22 wa Mfuko ambapo mkutano umetoka na maazimio 10 ya kufanya ili kuboresha huduma na ustawi wa mfuko.
Wakurugenzi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Robert Mtendamema, (Aliyenyoosha mkono), ambaye anasimamia mifumo ya komputa ya Mfuko huo, Julius Mganga, nayesimamia utawala, (Kulia), na Steven Alfred, (Nyuma kulia), anayesimamia uwekezaji, wakitembelea mbuga hiyo Jumamosi Oktoba 13,2012.



Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dkt. Adolf Mkenda, (Wapili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, William Erio, (Kushoto), Mkurugenzi wa Utawala wa Mfuko huo, Julius Mganga, (Watatu kushoto), Mkurugenzi wa Mifumo ya Komputa ya Mfuko huo, Robert Mtendamema, (Wanne kushoto), na mjumbe wa bodi hiyo ya wadhamini, Frank Godfrey Mtosho, wakibadilishana hili na lile, kwenye mapumziko mafupi ya safari ya kilomita 120 kutoka mjini ASrusha kwenda mbuga ya wanyama Tarangire Jumamosi Oktoba 13, 2012. Wanachama na wadau wa mfuko huo waliokuwa wakishiriki mkutano wa 22 walipata fursa ya kutembelea mbuga hiyo baada ya kazi ya siku tatu kupeana taarifa na kuweka mikakati mipya juu yab maendeleo yab mfuko huo mjini humo
Mshiriki akisoma kipeperushi chenye maelezo ya kina ya Mbuga ya Wanyama Tarangire, kwenye eneo la maelezo kwa wanaofika kutembelea mbuga hiyo Jumamosi Oktoba 13, 2012
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Jannet Ezekiel, (Kulia), ambaye pia ni mratibu msaidizi wa mkutano wa 22 wa wanachama na wadau wa Mfuko huo uliomalizika Ijumaa mjini Arusha, akiwa na mwenzake, mapema Jumamosi nasubuhi, wakiandaa safari ya washiriki wa mkutano huo kwenda kutembelea mbuga ya wanyama Tarangire mjini Arusha
Wafanyakazi, wanachama na wadau wa Mfuko huo wakijipatia mlo kwenye mgahawa wa Tembo ulio ndani ya hifadhi ya mbuga ya Tarangire.

Wafanyakazi, wanachama na wadau wa Mfuko huo wakijipatia mlo kwen ye mgahawa wa Tembo ulio ndani ya hifadhi ya mbuga ya wanyama Tarangire
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Adelgunda Michael Mgaya, (Kushoto), na Mwamini Tulli, wakibadilishana mawazo wakati wa mapumziko mafupi ya safari ya kilomita 120 kuelekea mbuga ya wanyama Tarangire mkoani Arusha Jumamosi Oktoba 13, 2012
Wadau, wafanyakazi na wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakitembelea mbuga ya wanayama, Tarangire Jumamosi Oktoba 13, 2012.Picha na K-VIS Blog

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ