• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Thursday, December 26, 2013

NE -MO ft.OMMY DIMPOZ - MY NUMBER ONE (OFFICIAL VIDEO)

No comments:
 
Mkali wa R&B ambaye aliwahi pia kushiriki shindando la BSS Nemo, amesema Ommy Dimpoz ndiye aliyemshauri kufanya wimbo wenye mahadhi ya Afro Pop tofauti na R&B, na kwamba wazo hilo lilipelekea yeye kurekodi ‘My Number One’.
Nemo amefunguka wakati akipiga story na Jabir Saleh na Dj K_U kwenye ‘The Jump Off’ ya 100.5 Times Fm.
“Ommy Dimpoz ni mshikaji wa karibu pia huwa anafanya kazi zake pale Combination Sounds, kwa hiyo alivyokuja pale kuna beat tukawa tumeisikiliza tukapata mizuka. Akasema kwa nini tusifanye hii kitu Nemo, ingawaje najua wewe ni professional R&B… na najua unania sana ya kutaka kuwakilisha, lakini unaonaje ukafanya hata African Style?” Alielezea Nemo.
Akisimulia jinsi ngoma hiyo ilivyopikwa, Nemo amesema aliuelewa ushauri wa Ommy Dimpoz na ndipo wakakaa chini wakaandika ‘My Number One’ na kuurekodi pale Combination Sound chini ya producer Man Walter ambaye ni binamu yake.
Mwimbaji huyo alielezea mfanano wa jina la wimbo wake na ule wa Diamond na kusema kuwa yeye haoni tatizo la mfanano wa majina ya nyimbo hizo ambazo zote ni kali.
“Naweza kusema kwamba jina sio tatizo, kila mtu ana number one wake, kila mtu anamuelezea…hata R. Kelly ana ‘My Number One’. Ili mradi tu wewe katika wimbo wako umeongelea vipi ‘My Number One wako’. Kwa hiyo hilo jina halipimi.”
Hata hivyo Nemo amesisitiza kwamba yeye ndiye alianza kurekodi wimbo huo kabla ya Diamond na kwamba aliurekodi mwaka jana (2012), na baadae akaanza kusikia nyimbo nyingine nyingi zenye jina hilo.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ