• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Wednesday, January 21, 2015

JUICE YA KAROTI NA FAIDA ZAKE MWILINI

No comments:
 
Nimejikuta napenda sana juisi ya karoti ambayo nakunywa walau mara moja tu  kila siku.Watu wengi hawaipendi wanasema sio tamu lakini inategemea imetengezwaje.Katika utengezwaaji ili uenjoy juice yako lazima iwe haina maji yaliyoongezwa wala sukari.Ni juice tuu ya karoti pekeee.
KWAKUNYWA JUICE YA KAROTI UTAPATA FAIDA ZIFUATAZO.
1.Karoti ina carotine ambayo hukupa uwingi wa vitamins A,B,na E
2.Kwa sababu ya uwingi wa madini juice ya karoti inasaidia sana afya ya macho katika kuona vizuri,uimara wa mifupa,meno na kucha.
3.Pia ngozi nyororo nayenye afya bila kusahau nywele.
4.Juisi ya karoti inasaidia kupunguza uwezokano wa kupata kansa ya ngozi na matiti.

5.Ukosefu wa vitamini A husababisha ngozi kukauka,kucha na nywele kuwa dhaifu sasa juisi ya karoti ina uwingi wa vitamin hivyo jusi hii ndio mpango mzima.
6.Kwa sababu ya uwingi huo wa vitamin A husaidia ini kufanya kazi yake ipasavyo.Na inasemekana ili ipatikane vitamin A ya kutosha kunywa juisi hii kila siku sio ukijisikia.
7.Haina cholestral
8.Madini kibao yanapatikana kwenye karoti  Calcium,Potassium,Copper, Iron, Magnesium, Manganese, Phosphorous
9.Kwa mama anaenyonyesha karoti itamsaidia kupata maziwa yenye afya kwa mtoto.
Hizi ni baadhi zipo kibao,kunywa juisi ya karoti kwa afya yako. 

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ