• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Thursday, May 5, 2016

Mitandao yaharibu soko la magazeti

No comments:
 
Vyombo vya habari vya asilia hususani magazeti vinakufa. Hivi sasa vvyombo hivyo vinajikongoja kutokana na mauzo hafifu  na mdororo wa mapato kutoka matangazo na kupunguza wafanyakazi.
Ila wakati idadi ya wasomaji wa habari mtandaoni ikizidi kukua, wanaoperuzi mtandaoni  humo hawatumii muda mwingi kwenye magazeti tando, utafiti wa Pew Research Centre unaeleza.
Katika utafiti wake wa hali ya vyombo vya habari 2015 (“State of the News Media 2015,”) imeonesha kwamba katika vyombo vya habari vya karatasi (print media), Digitali na TV, imeonesha Dhahiri kwamba magazeti yanaelekea kuzimu.
Utafiti huo umetolea mfano magazeti makubwa ambapo wasomaji wake wa mtandaoni wamewashinda kwa mbali kwa idadi ya wasomaji wa makaratasini, ambapo gazeti kubwa sana la New York Times la Marekani limetangaza kuwa nakala zake zipatazo 650,000 kwa wiki zimepitwa kwa mbali sana na wa mitandaoni
Hivi sasa kuna mjadala mitandaoni endapo kama Tanzania iko ama itafika huko. Mabishano ni makali ambapo wa makaratasini wanashikilia msimamo wao kuwa nchini hapa tasni ya habari mtandaoni bado ni change sana kuweza kutishia amani ya magazeti.
Upande wa digitali unajibu kwamba endapo kama kuna wahariri viburi wanaobeza kasi ya mitandao, basi wakae mkao wa kulala njaa muda si mrefu ujao, maana ni wachache wanaoendelea kupata habari kwa njia asili ya magazeti.
Upande wa digitali umeyasifia magazeti ya Global Publishers na la Mwananchi  anbayo ni dhahiri yana wahariri wanaokwenda na wakati na wanaojua nini wanachokifanya kwa kuanza na mapema kuogelea bahari ya maendeleo ya tasnia kwa vitendo kwa kuwa na vitengo vya mtandao vinavyopelekesha mbio magazeti yanayobeza technolojia hio kwa kubuni.
“Ni kweli kwamba Tanzania  bado sana kiteknolojia na miundombini kiasi cha habari za mtandaoni zikatishia uhai wa habari za makaratasini, lakini si uongo kwamba ukizingatia uharaka na gharama pamoja na kwenda na wakati muda si mrefu print media itakwenda na maji”, amesema blogger mmoja ambaye pia ni mwanahabari kwenye moja ya magazeti makubwa nchini.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ