Gari ya P-diddy baada ya kupata ajali |
Siku
moja baada ya taarifa ya ajali ya gari aliyoipata CEO wa Bad Boy
Records maeneo ya Los Angeles kushtua ulimwengu wa burudani, sasa
taarifa kuhusu hali yake kiafya imewekwa wazi rasmi na kusambaa kwenye
mitandao mbalimbali.
P-diddy akiwa amejilaza kwenye majani baada ya ajali |
Muwakilishi
wa rapper huyo mkongwe amesema, “Sean Combs alipata injuries mbalimbali
katika ajali ya gari aliyopata jana ikiwa ni pamoja na shingo lake na
mbavuni. Sasa hivi anaendelea na matibabu kwa daktari wake kwa ajili ya
hizi injuries na angependa kuwashukuru fans wake wote kwa sapoti yao
kubwa tangu alipopata ajali.
Jumatano
hii police wa Los Angeles wametoa taarifa rasmi na kuthibitisha hilo
imesema, “ Sean “Diddy” Combs amepata injuries katika ajali ya gari
ambayo ilitokea mbele ya Hotel ya Beverly Hills, na kwamba boss huyo wa
Dirty Money na Bad Boy Records alisema atatafuta matibabu yake binafsi.”
Diddy akitoa maelezo kwa polisi waliofika eneo la ajali |
Katika
ajali hiyo iliyotokea jumatano hii P.Diddy alikuwa anaendeshwa na
dereva wake, ambapo gari lake aina ya Cadillac Escalade iligongana na
Lexus RX mbele ya hotel ya Beverly Hills na ambulance iliitwa haraka
katika eneo la tukio.
Kwa
mujibu wa mtandao wa X17 online wahudumu wa hotel hiyo walitoka haraka
na kwenda kuwasaidia P.Diddy na dereva wake na alionekana akiwa
amejilaza mbele ya garden ya hotel hiyo. Lakini baada ya muda alikataa
kupelekwa hospitalini na ambulance na kwamba atatibiwa na mganga wake
binafsi.
Mungu
ameepusha ajali hii kuwa na madhara makubwa, tumuombee apone haraka
aendelee kufanya kazi ya kuwapa shangwe fans kupitia spika kwa hits
kibao toka Bad Boys.
No comments:
Post a Comment