• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, October 26, 2012

Heineken yatisha na uzinduzi wa Skyfall Mlimani City

No comments:
 


Ukiwa na Dress Code ya ‘The Bond in You’ jana uzinduzi wa filamu mpya ya James Bond, Skyfall ulikuwa kama ulivyotegemewa na watu wengi, ulitisha. Kabla ya kuoneshwa kwa filamu yenyewe, waalikwa na watu wengine mbalimbali wakiwemo watu maarufu kwenye showbiz ya Tanzania walijumuika pamoja kwenye ukumbi uliopo jirani na makao makuu ya Vodacom pale Mlimani City kwa cocktail ya nguvu na upigaji picha.
Mavazi yaliyotawala yalikuwa kama yule mpepelezi maarufu James Bond kwenye kisa cha mwandishi wa kitabu wa Uingereza, Ian Fleming. Suti nyeusi na mashati meupe pamoja na neck tie zilionekana kupamba muonekano maridhawa wa ukumbi huo. Baada ya bata mbili tatu ndipo kila mmoja alijongea kwenye ukumbi wa Century Cinemax cinema Mlimani City, kuiangalia kwa mara ya kwanza filamu hiyo ya Skyfall.
Baada ya James Bond (Daniel Craig) kupotea na kudhaniwa kuwa amekufa, bosi wake M, (Judi Dench) akiwa kama mkuu wa MI6 anajikuta katika pressure nzito ya kuonekana kama ameshindwa kuiongoza secret service hiyo lakini kuonekana tena kwa Bond kunampa matumaini M ya kumtafuta Raoul Silva, mhalifu hatari ambaye ni tishio kwa usalama wa nchi.
Pamoja na kuwa na action na stunt za kufa mtu, wengi waliohudhuria uzinduzi huo wamesikitishwa na kifo cha M ambaye ameonekana kwenye filamu saba za James Bond.
Haya ni baadhi ya maoni ya watu tuliozungumza nao kuhusiana na jinsi walivyoiona Skyfall.
B12: Kama nilivyotegemea, James Bond hajawahi kuniangusha ila nimechukia M amekufa bana sasa itakuaje kwenye zile movie nyingine ya James Bond inayokuja, sijui nani atamreplace kwenye hiyo nafasi yake so imeisha kwa masikitiko lakini imeisha fresh.
Izzo B: Uishaji wake sijaupenda sana lakini labda The Return wamekuja na style mpya lakini pale yule bibi (M) ametaka kufa ile ndio ending yangu. Vitu nilivyojifunza vikubwa sana inabidi tuwe na mtu kama director wa movie pia sababu kuna mashots yanapigwa ya hatari sana pia sound unajua unamsikia mtu fresh, kuna vitu vingi ambavyo inabidi tuwe na director wa movie unayocheza, kuna vitu vingi vya kiufundi zaidi.
Reuben Ndege: One tumeambiwa kwamba huyu ni Bond wa kisasa sio but movie imeisha sijamuona kwenye Twitter, sijamuona kwenye Facebook, sijamuona akipiga picha Instagram kwahiyo naona kama Bond kidogo anapitwa na wakati halafu sijui, nimemuona Bond akilia sijui kama ndio Bond wa kisasa sababu kwenye kupitia pitia kwenye internet nimekuta sehemu yule the main actor wa Bond anazungumzia mara ya kwanza ameiona Skyfall ile ngoma aliyofanya Adele alitoa machozi, sasa nashindwa kujua huyu Bond wa sasa ni wa kulia kulia, Bond girl mwenyewe hatujaona akifanya manjonjo yoyote kama kawaida halafu I credit the director more shots ambazo alikuwa anachagua. Story ilikuwa katikati haijanichanganya sana.
Mwisho I didn’t want M to die but nimeona kama mwisho was forced ,umewekwa ili tujue kuna Bond nyingine inakuja. Thanks for Heineken kwa kutualika, thanks for Heineken kutupa opportunity kuwa watu wa kwanza kuiona hii kitu.
Jokate: Nimependa the cameras, sites I loved the creation of sites, dialogue, yule script writer alikuwa ametulia sana.
Fetty: Ofcourse nimefurahia, it’s what I expected kuanzia hata pale nilipoangalia trailer kabla sijaja leo. Ningependa kuiangalia tena sababu ninajua kabisa there are some parts zitakuwa zimenipita ili niweze kuielewa zaidi na zaidi ili kwamba unaweza ukakaa ukamsimulia mtu comfortably so I have to watch it again, sitachoka kuiangalia tena. One iko na action za kutosha, two iko na a bit of humor ukisikiliza vizuri unaweza ukacheka, three iko na quality poa, four sounds poa, five the music is good inside.
Bila shaka utakuwa na hamu ya kuiona pia Skyfall, usisite kutuambia utakavyoiona. Kwa sasa furahia kuangalia picha hizi za watu waliohudhuria uzinduzi huo.
Dj Fetty na marafiki wakibadilishana mawazo Am I looking hot!! Ambwene Yesaya alikuwepo pia AY na Madam Rita Captain G na mshkaji wakifurahia Heineken Elligiver na Martin Kadinda Feza Kessy Happy people IMG_7919 (800x533) IMG_7930 (800x533) IMG_7989 (800x533) IMG_7998 (800x533) IMG_8027 (800x533) IMG_8061 (800x533) IMG_8063 (800x533) IMG_8084 (800x533) IMG_8087 (800x533) IMG_8090 (800x533) Izzo B, B12, Quick Rocka na mshkaji Kibonde na mdau wakipiga story Lotus, Vanessa Mdee na Abby Madam Rita akihojiwa na Capital TV Master Jay akibadilishana mawazo na mdau Muda wa kufurahia Heineken Nancy Sumari na Luca Neghesti Nancy Sumari na Shaa Reuben Ndege na Jokate Sade na Jokate Salama Jabir hakuachana na swahiba wake Madam Rita Sam Misago na Shaa Sam Misago Ticket time Umetuona!! Wapenzi wa movie wakifurahia Heineken Watangazaji kwenye pozi Watangazaji wa The Weekend Chat Show (Clouds TV)

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ