Meneja
Mradi wa Ujenzi wa Daraja la Kigamboni kutoka Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF),Karim Mattaka (katikati) akionyesha sehemu ya
ujenzi wa Daraja hilo unaoendelea hivi sasa katika eneo la Kurasini
mpaka Kigamboni wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia
Maendeleo ya Jamii ilipofanya ziara ya kuona ujenzi wa Daraja hilo
leo.Watano Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama na
Kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudencia Kabaka.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF),Dkt. Ramadhan Dau
(kulia) akiuongoza ujumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia
mambo ya Maendeleo ya Jamii,iliyofanya ziara ya kutembelea eneo la
ujenzi wa Daraja la Kigamboni mapema leo.Wengine pichani toka kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo,Mh. Jenista Mhagama,Waziri wa Kazi na
Ajira,Mh. Gaudencia Kabaka na Mjumbe wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge
wa Jimbo la Mtera,Mh. Livingston Lusinde.
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya
Jamii wakiwa katika ziara ya kutembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa
Daraja la Kigambini unaosimamiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii
(NSSF),uliopo eneo la Kurasini Jijini Dar es Salaam leo.
Kamati
ya Kudumu ya Bunge inayoshughulikia mambo ya Maendeleo ya Jamii
ikipatiwa maelezo mbali mbali juu ya ujenzi wa Daraja hilo ambalo ujenzi
wake utachukua takribani miezi 36 mpaka kukamilika kabisa.Daraja hilo
lina urefu wa mita 680 na litakuwa na jumla ya barabara sita ambazo tatu
zitakuwa zinakuja mjini na zingine za kuelekea Kigamboni.
No comments:
Post a Comment