JESHI
la Polisi limewataja watuhumiwa 10, na bado linaendelea kuwatafuta
watuhumiwa wengine, ambao inadai walishiriki kumuua aliyekuwa Kamanda wa
polisi mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow.
Kati ya watu hao watano wametiwa mbaroni Mwanza na watu watano kutoka Dar es Salaam. Leo
(jana) mjini Mwanza, mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania
IGP Said Mwema, Mkurugenzi wa makosa ya Jinai Nchini (DCI) Robert
Manumba aliwataja watuhumiwa hao ni Muganizi Michael Peter (36) mkazi
wa Isamilo ambaye inadaiwa alikiri mwenyewe kumuua kamanda kwa risasi.
Wengine
ni Chacha Waitara Mwita (50), Magige Mwita Marwa, Bugazi Edward Kusota
na Bhoke Mara Mwita (42) ambao walikamatwa jijini Dar es Salaam baada
ya kuwekewa mtego kwa msaada wa wananchi.
Wanaoshikiliwa
jijini Mwanza kwa mahojiano ni pamoja na Mwalimu Doroth Moses Lyimo
aliyekuwa na RPC wakati mauaji yakitokea, Felix Felician Minde (50),
Philemon Felician (46) maarufu kama Fumo, Bahati Agustino Lazaro (28) na Amos Magoto (30) maarufu kama Bonge.
Manumba
amesema simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa
nyumbani na marehemu, ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo na
hatimaye wahusika kukamatwa.
Alisema
Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake Manumba kilijigawa
kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine
la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao
ya simu.
Marehemu
Kamanda Barlow aliuawa usiku wa Oktoba 12 majira ya kati ya saa 7 na 8
usiku katika eneo la Mianzi Mitatu, Kitangiri, kona ya Bwiru baada ya
kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, wakati alipopita
kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao
cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji.
No comments:
Post a Comment