• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Tuesday, October 16, 2012

Stamina kuja na albam yenye nyimbo 20

No comments:
 


Siku hizi wasanii wa Tanzania hasa wanaofanya Hip Hop wengi wao hawazungumzii tena masuala ya kutoa albam. Ni wengi tayari waliowahi kuweka wazi kuwa hawatatoa tena albam kwakuwa hazina faida yoyote zaidi ya kunyonywa na wasambazaji kwa malipo ya shilingi mia mbili kwa tape moja. Lakini hili si jambo linalomkatisha tamaa rapper mchanga wa hit ya ‘Kabwela’ Stamina kutoa albam.
Stamina ameiambia 255 ya Clouds FM kuwa yuko mbioni kuachia albam yake ya kwanza itakayokuwa na nyimbo 20.
Amesema nyimbo nyingi katika albam hiyo zitakuwa na ujumbe wa kijamii yaani conscious zaidi.
Aliongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa nyimbo zake zilizotoka kama Kabwela, Alisema na Najuta Kubalehe, katika albam hiyo kuna wimbo aliomshirikisha Fid Q ambaye anamchukulia kama baba yake kisanaa katika wimbo uitwao Like Father Like Son.
Fid Q Pia atalipia gharama zote za kufanyika kwa video mpya ya Stamina ambayo hakutaja ni ya wimbo gani.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ