Waigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu na Aunt Ezekiel wamewaomba
radhi watanzania kwa picha zao mbaya walizopigwa kwenye show za Fiesta.
Wasanii hao wamezungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa
habari maelezo jijini Dar es Salaam kwaajili ya kuomba radhi kwa kupigwa
picha hizo za nusu utupu walizopigwa kwenye show hizo.
Wakiongena waandishi wa habari Aunty Ezekiel amesema ameumizwa na
kitendo hicho kwakuwa wao kama wanawake katika jamii, wana wazazi, ndugu
jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wao wanaowapenda na kuwaheshimu.
Aunt Ezekiel
Hivi karibu Aunty Ezekiel alijitetea na kunukuliwa kwenye chanzo
kimoja akisema, “Ni kweli nilikuwa ninacheza katika Jukwaa (Stage) na
nilikuwa nimekunywa, lakini sikuwa nimedhamiria kukaa uchi bali ni mbinu
za wapiga picha ambao walitumia njia ya kuamua kunidhalilisha kwa
kunipiga picha wakiwa chini ya Jukwaa (Stage) ili wapate kuuza magazeti
yao, hata ukiangalia picha zenyewe zimepigwa kiujanja sana.”
Waigizaji hao waliongozana na katibu Mkuu wa shirikisho la filamu Tanzania, TAFF, Wilson Makubi
No comments:
Post a Comment