Kama imekupita Hekaheka ya leo MAY 02 2015 inahusu mwanamke mmoja ambaye amesema kwamba mume wake alikuwa anamdai kila siku mtoto.. akaamua aingie Hospitali ya Mwananyamala kwenye wodi ya Wajawazito, akajifanya na yeye ni mjamzito.
Baada ya kukaa kwa muda wanawake wenzake walimshtukia alikuwa kwenye pilika pilika za kutaka kuiba mtoto, walipopeleleza wakajua kwamba hakuwa mjamzito na alikuwa na mpango wa kuiba mtoto.. ishu ikafika Polisi na kwa sasa bado kesi iko mikononi mwao.
Geah Habib anaifuatilia hii na tutasikia zaidi kuhusu ishu hiyo kwenye Hekaheka zinazofuatia.. kilichosimuliwa leo kiko kwenye hii sauti hapa. Audio






No comments:
Post a Comment