• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, March 4, 2016

No comments:
 
Wauza filamu hao na maduka yao yakiwa yamefungwa na TRA.
Na Mayasa Mariwata, AMANI
DAR ES SALAAM: Kufuatia agizo la Dk. Rais John Pombe Magufuli la kutaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wapitishe msako wa kukamata CD za filamu ambazo hazina stika za mamlaka hiyo, maduka kadhaa yamefungwa Kariakoo jijini Dar es Salaam na kuacha vilio kwa wamiliki.
Zoezi hilo lilifanyika kwenye maduka yaliyopo kwenye Mtaa wa Aggrey na Liwiti ambapo kuna maduka mengi yanayouza CD, hasa za nje na wengi ambao maduka yao yamepigwa pini ni wenye filamu za nje ya nchi.
Hata hivyo, akizungumza na paparazi wetu, kijana mmoja anayeuza filamu za Kibongo ambaye hakutaka jina lake lichorwe gazetini ambaye duka lake halikukumbwa na ishu hiyo alisema kuwa, maduka yaliyofungwa ni tisa ambayo huuza filamu za nje kiholela na hazina nembo ya TRA.
“Maduka hayo unayoyaona ni yale yanayouza filamu za nje sanasana zile za Kikolea japo lile agizo la Rais Magufuli lililenga filamu ambazo hazina nembo ya TRA bila kujali ni za ndani au nje ya nchi,” alisema kijana huyo.
Ray-Kigosi-1Vincent Kigosi ‘Ray’ a.k.a "MZEE WA KUNYWA MAJI MENGI"
Akaongeza: “Tatizo filamu nyingi za nje wengine wanazichukua tu kwenye mitandao na kubani CD, sasa ni vigumu kuwa na nembo. Pia sababu nyingine iliyosababisha maduka haya kufungwa ni kutokana na wasanii wengi kulalamika kuwa, kinachochangia kuliua soko la filamu Bongo ni hizi filamu za nchi za wenzetu, ndo’ maana unaona haya maduka yamefungwa.”
Mbali na kauli ya kijana huyo, paparazi wetu alishuhudia makaratasi yaliyobandikwa kwenye milango ya maduka yaliyofungwa, wahusika wa biashara hiyo wakitoa kero mbalimbali.
Wengine waliwatupia lawama mastaa wa filamu Bongo kwamba hawatoi kazi nzuri ndiyo maana filamu zao hazina soko lakini walimtaja waziwazi Vincent Kigosi ‘Ray’ kuwa, aliwahi kulalamika kwamba filamu za nje ndiyo zinaua soko la filamu za ndani.
NapeWaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye.
Baadhi ya wamiliki walionesha kukerwa na kauli hiyo kwamba ndiyo iliyochangia TRA kuwapitishia panga la kufunga maduka yao kwa sababu Ray na wenzake wanazipiga vita filamu za nje huku wenyewe wakishindwa kuziboresha za ndani.
Nape Moses Nnauye ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo alipoingia madarakani, miongoni kwa vipaumbele vyake alisema ni kuangalia masilahi ya wasanii nchini ambapo alisema wamekuwa  akinyonywa na wajanja wachache

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ