• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, July 8, 2016

Views Ya Drake Yafikia Rekodi Ya Thriller Ya Michael Jackson

No comments:
 
Hakuna ubishi kwamba kwenye chati za muziki mwaka huu, Drake, anafanya maajabu. Tangu alipotoa album yake ya VIEWS, amekuwa akivunja rekodi baada ya rekodi. Mtandao wa Billboard unazo rekodi zote ambazo Rapper huyu kutoka Toronto,Canada ameshazivunja au kuzifikia.
Kwenye mtiririko huo, album ya VIEWS sasa imekaa juu ya chati za Billboard 200 na Hot 100 kwa wiki 7 mfululizo. Kwa maana hiyo VIEWS imefikia rekodi iliyowekwa na Michael Jacksonmwaka 1983 alipotoa album ya Thriller. Drake anakuwa msanii wa pili wa kiume kufikia rekodi hiyo.
Whitney Houston na bendi ya The Beatles wao wanashikilia rekodi ya kuwa katika chati hiyo kwa wiki 12 mfululizo. Je, Drake atampita Michael Jackson? Je anaweza kuendelea mpaka kufikia rekodi ya Whitney Houston na The Beatles? Tuendelee kusubiri. Vyovyote vile Drake anastahili pongezi.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ