• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, November 11, 2016

Kampuni ya Reli yaanza ujenzi wa Reli ya Kisasa

No comments:
 
Kampuni Hodhi ya rasilimali za reli nchini (RAHCO) imeanza utekelezaji wa ujenzi mkubwa wa reli ya kati ya kisasa kwa kiwango cha Standard Gauge, ukijumuisha maandalizi ya hatua za mwanzo, sanifu na kuwapata makandarasi, ambapo awamu ya kwanza ya ujenzi kutoka Dar es salaam kwenda Isaka na Mwanza imegawanyika katika awamu ndogo nne.

**Mkurugenzi Mtendaji wa RAHCO Injiania Masanja Kadogosa, amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwamba awamu hiyo ya kwanza itajumuisha makandarasi wanne katika awamu hizo nne, ikiwemo Dar es salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Makutupora, Makutupora hadi Tabora na Tabora hadi Mwanza.

na Kadogosa amesema ujenzi wa reli mpya ya kiwango cha standard gauge katika mtandao mzima wa reli utajengwa sambamba na reli iliyopo yaani meter gauge ukitoa tu maeneo korofi kwa mafuriko, kona kali na mteremko mkali na tayari zabuni zimekwishatangazwa.
Ujenzi wa reli hiyo yenye upana wa mita 1.345 utaruhusu treni kutembea kwa spidi ya kilomita 120 kwa saa na utakamilika baada ya miaka mitatu ukitarajiwa kuchochea maendeleo katika sekta ya kilimo, biashara, madini na viwanda hususan maeneo ambapo reli hiyo itapita pamoja na kwa nchi  jirani hasa Rwanda, Burundi, Uganda, DRC na Kenya.

Mtandao mzima wa reli nchini unaotegemewa kujengwa kwa kiwango cha standard Gauge una jumla ya kilometa 2,561 ukitarajiwa kugharimu Dola za Marekani Bilioni 7.683
 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Reli Tanzania akizungumza na waandishi wa Habari jijin

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ