• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Monday, October 15, 2012

‘BABY J’ AWATOA KASORO WANAUME WA TANZANIA BARA, ADAI HAWANA MAPENZI YA DHATI KAMA WA ZENJI…!!

No comments:
 


MSANII wa ngoma ya ‘Bwashee’, Baby J, amedai kuwa wanaume wengi wa Tanzania Bara si wapendaji bali wengi ni wale wanaotaka kumchezea mwanamke na mwisho wa siku wanamtema tofauti na wanaume wa Visiwani ambao hupenda na huwa na mapenzi ya dhati kwa mwanamke.

Mtandao wa DarTalk ulifanya mazungumzo mafupi na msanii huyo juu ya muziki wake pamoja na maisha kwa ujumla ndipo alipoitoa ishu hiyo, kwa madai kuwa wenaume wengi Bara wanapenda kutoka na mwanamke mrembo mwenye kila aina ya mvuto na ndiyo maana wanakuwa na tabia ya kuacha acha hovyo.



Baby J stejini

Alidai kuwa Zanzibar wanawake wengi ni wale ambao wanaovaa baibui muda wote na hawana tabia ya kuonyesha miili yao na ndiyo maana unakuta hata wanaume hawana tamaa ya kutamani kila mwanamke wanayemuona mbele yao.

“Hakuna wahalibifu kama wanaume wa Dar yani ukicheka tu umekwisha, unajua hii ni tofauti sana na wanaume wa Visiwani na nahisi inatokana na wadada wenyewe kuvaa nguo za mitengo mno ambazo huacha sehemu kubwa za mwili zikiwa wazi hivyo humfanya mtoto wa kiume atumie kila njia kukupata,” alidai.

Source   :     DarTalk

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ