• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Saturday, October 27, 2012

Bondia Rashid Matumla na Patrik Amot wa Kenya kupambana mtwara kesho

No comments:
 
Bondia Rashid Matumla na Patrik Amot wa Kenya wanatarajiwa  kupanda ulingoni kesho katika ukumbi wa Makonde mkoani Mtwara. Mabondia wote wamepima na kuwa na afya njema na wote kuwa katika uzani sawa wa kilo 73 kila mmoja.

Zoezi zima la upimaji lililoendeshwa na katibu mkuu wa TPBO Ibrahim Kamwe na Dkt.  Madono lilienda vema. Pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kati ya Bakari Mohamed wa mtwara na Abdala Mohamed wa Dar es salaam katika pambano la ubingwa kg57.

Pia kutakuwa na mapambano mengine mengi ya utangulizi kati ya mabondia toka Black Mamba Club ya Mtwara na mabondia toka Dar es salaam.kama Haruna Mnyalukolo atacheza na Ashraf Abdala, Issa Matumla (mtoto wa Rashid Matumla) atacheza na Mamis Mtupeni, wakati Hamis Ali Mkupa wa Mtwara atacheza na Ide Mnali katika mapambano la raundi nane nane.
Rashid Matumla akipima uzito tayari kumkabili Mkenya  huko Mtwara
Patrik Amot wa Kenya akipima uzito leo
Maofisa wa TPBO wakitafakari kitu baada ya upimaji wa mabondia Mtwara leo

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ