Gari la kusambaza magazeti ya kampuni ya Mwananchi lapata ajali, watu 3 wapoteza maisha, 5
Gari
linalosambaza magazeti ya kampuni ya Mwananchi mikoa ya Kilimanjaro na
Arusha,limepata ajali wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro na kusababisha
vifo vya watu watatu na wengine watano kujeruhiwa.
Kamanda
wa Polisi mkoani Kilimanjaro Afande Robert Boaz, amethibitisha kutokea
kwa ajali hiyo Oktoba 26 majira ya saa 11 alfajiri katika eneo la
Kirinjiko, wilayani Same, barabara kuu ya Tanga-Moshi.
Kamanda
alisema Gari hilo lenye namba za usajili T336 BFU Isuzu Pick-up
linalosafirisha magazeti ya kampuni ya Mwananchi Communication
(MCL) ililigonga gari lenye namba za usajili T 415 AAM/ T 411AAM Scania
na kusababisha vifo vya watu watatu papohapo.
Kamanda
Boaz amewataja waliofariki kuwa ni Ibrahim Mrutu (65) mkazi wa
wilayani Same, Abdalla Rajabu(49) mkazi wa Majengo Mkoani Arusha ambapo
wote ni madereva wa Simba Truck pamoja na Robert Mnyeki (39).
Aliwataja
waliojeruhiwa kuwa ni Rahim Bakari (28)mkazi wa Kinondoni jijini Dar es
Salaam mfanyakazi wa kampuni ya Mwananchi,Juma Said (37)Dereva wa Simba
Truck mkazi wa Arusha kwa Mrombo,Gasino Nguma(40) mwalimu mkazi wa
Mlandizi jijini Dar es salaam, Hamza Omary (31) mfanyabiashara mkazi wa
Buguruni jijini Dar es salaam pamoja na Sekero Musa (30) ambaye hali
yake inaelezewa kuwa mbaya.
Watu
hao walikuwa ni abiria katika gari lililokuwa likisafirisha magazeti
ambapo Majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na KCMC
kwa ajili ya matibabu.
Chanzo
cha ajali hiyo kamanda alisema ni mwendo kasi wa gari dogo na kwamba
dereva wa gari hilo Wambura Ramadhani anashikiliwa na jeshi la polisi
kwa mahojiano na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo bado
unaendelea.
No comments:
Post a Comment