• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Saturday, October 20, 2012

IJUMAA -Tishio la Maandamano ya Waislamu; Ukimya Watawala Dar, Shughuli Zasimama, JWTZ Waingia Mitaani

No comments:
 
Baadhi ya magari ya Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) wakionekana kudhibiti ulinzi maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
HALI ya ukimya hapo jana ilitawala katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam hasa kati kati ya jiji na hata maeneo ambayo kikawaida huwa na misongamano mikubwa ya watu. Maeneo ya Kariakoo ambayo huwa na idadi kubwa ya watu hata kwa siku za Siku Kuu leo haikuwa hivyo, kwani yalionekana matupu na makundi ya askari wakionekana kuweka kambi ama kuzunguka hapa na pale kuimarisha ulinzi.
Hali hii imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya Waislamu kutaka kuandamana kuelekea Ikulu mara baada ya swala ya Ijumaa wakipinga kitendo cha kukamatwa kwa mmoja wa viongozi wa taasisi za Uislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda na kushikiliwa kwa baadhi ya Waislamu ambao walikamatwa katika vurugu za uvamizi wa makanisha hivi karibuni eneo la Mbagala Jijini Dar es Salaam.
Shughuli za kibiashara hasa za maduka na nyinginezo ambazo huendeshwa pembezoni mwa Barabara ya Uhuru, Mitaa ya Kongo, Msimbazi, Mnazi Mmoja, Lumbumba na maeneo mengine ya katikati ya Jiji la Dar es Salaam leo zilisimama na maduka kuonekana yamefungwa kutokana na kuhofia vurugu za waandamanaji.
Ulinzi wa Askari Polisi wa Kawaida, Askari wa Kutuliza Ghasia (FFU) ulikuwa mkali maeneo yote ya jiji, na baadhi ya maeneo mengine yalionekana magari ya wanajeshi waliokuwa wamevalia mavazi ya kutuliza ghasia wakionekana tayari kuongeza nguvu kwa Jeshi la Polisi.
Kama hiyo haitoshi polisi walitumia helkopta kufanya doria kuangalia usalama maeneo mbalimbali ya jiji. Helkopta ya Polisi ilisikika ikipita angani kwa kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam kuangalia hali yoyote ya machafuko. Hali ya wasi wasi pia ilionekana kwa baadhi ya watu na kujiami muda wote, kuhofia kujikuta wakiingia katika vurugu hizo.
Kwa mujibu ya kipeperushi ambacho mtandao huu umekipata kikionekana kuwa kimeandaliwa na baadhi ya washawishi wa maandamano ya leo kinasema; Waislamu wanapaswa kuandamana wakipinga kitendo cha kushikiliwa kwa Sheikh Ponda, kutoweka kwa Sheikh Farid Mjini Zanzibar juzi na kitendo cha kushikiliwa na kufunguliwa kesi Waislamu waliokamatwa katika vurugu zilizotokea hivi karibuni maeneo ya Mbagala na kuchomwa moto kwa baadhi ya makanisa.
Hata hivyo licha ya Jeshi la Polisi kuweka ulinzi huo maeneo mbalimbali jioni baadhi ya Waislamu waliokuwa wakitoka kuswali walipambana na askari polisi pale walipojaribu kuandamana wakidai wanakwenda Ikulu. Askari walidhibiti maandamano maeneo ya Kariakoo na kuwakamata watu waliojaribu kupambana na askari waliokuwa wakilinda usalama.
Eneo la Ikulu Jijini Dar es Salaam na makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani napo ulinzi ulihimarishwa ili kuzuia vurugu zozote ambazo zingeweza kuibuka. Baadhi ya waandamanaji mmoja mmoja walijikuta wakikamatwa na polisi pale walipopenyeza na kujaribu kuibukia Ikulu huku wakiwa wameficha kanzu zao.

Askari Kanzu akimsindikiza kwa teke mmoja kati ya watuhumiwa waliokamatwa wakati wa operesheni maalum iliyowekwa katika jiji la
Dar es Salaam,leo mchana ili kuwadhibiti baadhi ya waliodaiwa kuwa ni waumini wa dini ya kiislam, waliokuwa wamepanga kufanya maandano mchana wa leo baada ya Swala ya Ijumaa kuelekea Ikulu kwa lengo la kushinikiza kiongozi wao, Katibu wa Jumuiya za Taasisi za Kiislam, Sheikh Ponda, aliyekamatwa majuzi,aachiwe. Hata hivyo jitihada za watu hao ziligonga ukuta baada ya wao kujipanga kutokea kila kona na kukutana maeneo ya Ikulu, lakini la Askari pia walijiandaa na kujipanga vyema kila kona ya jiji na kuwadhibiti watu hao. 
Vurugu kubwa ilikuwa katika maeneo ya Kariakoo ambako pia walijitokeza baadhi ya vijana waliojichanganya na makundi hayo na kuanza kuvamia maduka na kupora mali za watu na kuwatishia wenye maduka, jambo ambalo liliwafanya Polisi kuwatawanya kwa kupiga risasi hewani na waliokaidi amri hiyo walianza kushughulikiwa kama picha hizi zinavyoonyesha Pata Mkanda Kamili.
Twende garini.....
Akaaaa sio mimi jamaniiiiiii, Babu (kulia} akijitetea...
Askari wakimdhibiti babu...
Babu akishuhshwa garini kuingizwa kituoni.....
Mgambo wa kike akipambana na kijana kumburuta kumpeleka garini, baadaye mgambo huyu CHALIII
Mgambo chaliii,lakini wapi anaye tuuuu....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Watuhumiwa wakipandishwa garini....
Jamaa akijaribu kueskep ambapo alikula bonge la mtama na kutambaa kama hivi na kudakwa na mgambo wa kike....

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakiwa katika Maeneo ya Kariakoo na viunga vyake kuhakikisha usalama wa raia na mali zao unaimarika .




Watu hao walifika mmoja mmoja maeneo ya Ikulu kabla ya kudhibitiwa na Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na kupelekwa Kituo Kikuu cha Kati. Kukamatwa kwa watu hao kunafuatia Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuwatawanya waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa na nia ya kufanya maandamano.



Muumini wa dini ya Kiislamu akishahadia kwa mola wake na kusema nipo tayari kufa kwa ajili ya kutetea dini ya Allah baada kukamatwa na Askari wa Kikosi cha Kutulia Ghasia katika viunga vya eneo la Ikulu. (Picha zote na Happiness Mnale)

 Barabara ya kuingia katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi zikiwa zimefungwa na Askari Polisi kufuatia vurugu zilizotokea leo

Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki.



Magari ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakiwa katika doria katika barabara ya Msimbazi ambako kulitokea vurugu zilizosababishwa na waislamu waliotaka kuandamana.
 


Waandishi wameshuhudia gari mbili za jeshi la Polisi zikiwa zimebeba wanajeshi waliokuwa na silaha. Katika maeneo ya Kariakoo vikosi vya Jeshi la wananchi wa Tanzania vimekuwa vikifanya doria ili kuimarisha hali ya ulinzi.Picha  kwa hisani ya Happiness Mnale

 Askari wa jiji wakishiriki kikamilifu katika zoezi la kuwakamata watu waliokuwa wamekusanyika kwa nia ya kutaka kuandamana katika eneo la Kariakoo

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ