• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, October 19, 2012

Maonesho ya Sanaa ya ‘Sober House’ Alliance Francaise Yazinduliwa

No comments:
 

Pichani ni kazi za Ubunifu zilizofanywa na Vijana waliobadili mwelekeo wa maisha waliopo katika taasisi ya Sober House ya visiwani Zanzibar.
Pichani ni kazi za Ubunifu zilizofanywa na Vijana waliobadili mwelekeo wa maisha waliopo katika taasisi ya Sober House ya visiwani Zanzibar.
Kamishna kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher Shekiondo akizindua rasmi maonyesho ya sanaa ya Sober House jijini Dar amesema kwa niaba ya tume ya kudhibiti dawa hizo Zanzibar na kwa Serikali kwa ujumla wanatambua mchango wa wadau mbalimbali uliosaidia vijana kuachana na tabia hiyo na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakukikisha asilimia kubwa ya vijana wanabadilika kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo sera madhubuti za Serikali na mipango mikakati ikiwemo utekelezaji wa Kampeni za ufahamu wa madhara ya madawa hayo.
Ameongeza kusema kuwa mikakati ya kupambana na matumizi ya dawa za kulevya inakabiliana na changamoto nyingi kutokana na uhaba wa vituo na wataalamu lakini Serikali haijakata tamaa na inaahidi kutimiza lengo hilo katika muda muafaka ikishirikiana na wadau mbalimbali na kuomba wadau wengine wajitokeze.
Mkurugenzi wa Alliance Francaise Tanzania Bw. Sullivan Benetier akitoa hotuba ya kumkaribisha mgeni rasmi katika uzinduzi wa maonyesho ya sanaa ya Sober House Zanzibar ambapo amesema wao wamekuwa wadau wakubwa wa kusaidia mpango wa kuwawezesha vijana kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kujirudi na kutumia vipaji walivyonavyo kufanikisha maisha yao na kujipatia kipato.
Baada ya kufanikiwa kwa mpango wa kuwawezesha watu wenye ulemavu wa ngozi sasa wamejikita katika kuhakikisha vijana Tanzania wanaachana kabisa na wimbi la matumizi ya dawa za kulevya kwa kuunga mkono shughuli hii ambapo vijana walioonyesha mfano kwa kubadili tabia wanapata fursa ya kuonyesha sanaa zao za kuchora na kuchonga na pia kutokuwa na vipindi vingine vya kutoa ushauri nasaha wa kiakili utakowasaidia kujitambua na kuwafanya kuwa mabalozi watakaoelimusha vijana wenzao kuachana na tabia za matumzi ya dawa hizo.
Mgeni rasmi katika maonyesho ya Sanaa ya ‘Sober House’ yaliyozinduliwa jijini Dar es Salaam Kamishna wa Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya visiwani Zanzibar Dkt. Shekiondo (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja na wadau wanaondesha mkakati wa kuwasaidia vijana kubadili tabia na kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na badala yale kuonyesha vipaji walivyo navyo katika sanaa.
Muasisi wa Sober House Visiwani Zanzibar Bw. Suleiman Maulid akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake ambapo ametoa wito kwa vijana wote Tanzania wanaojihusisha na utumiaji wa dawa za kulevya kuachana na tabia hiyo na kisha kujiunga na Sober House kwa msaada zaidi wa kimawazo, kifikra na kielimu. Pia ameitaka Serikali kuongeza nguvu zaidi kwa taasisi zinazopambana na dawa za kulevya nchini katika kuwawezesha kufanikisha mipango ya kuwawezesha vijana kujirudi.

Mkurugenzi wa Chama cha maafisa Ustawi wa Jamii Bi. Anna Swai akionyesha Sanamu ya Msanii Mkongwe nchini Bi. Kidude iliyotengenezwa na mmoja wa vijana waliobadili muelekeo na kuamua kuachana na dawa za kulevya Zakaria Mwiru (kushoto) wakati wa ufunguzi wa kazi za sanaa
Baadhi ya Wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi wa Maonyesho ya Sanaa ya Sober House Recovery yanayoendelea katika ukumbi wa Alliance Francaise jijini Dar na kiingilio ni Bure kwa wote.
Raia wa kigeni akitazama bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na vijana waliobadilika na kuamua kuacha tabia za utumiaji wa madawa ya Kulevya na kujishughulisha na sanaa.
Mbunifu wa Mavazi nchini na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House (TMH) Khadija Mwanamboka a.k.a Kubwa la Maadui alikuwa ni miongoni mwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa maonyesho hayo.Pichani akipozi na moja ya mkoba uliosukwa na mkeka ikiwa ni kazi za vijana waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya na kujifunza fani mbalimbali na mwishowe kuvionyesha kwa jamii.
Maonyesho haya ni bure, Tujitokeze kuwaunga vijana wetu walioamua kubadili tabia na tujifunze kutoka kwao. “Tanzania bila madawa ya kulevya inawezekana”.
Kijana Zakaria Mwiru akionyesha ubunifu wake wa kinyago chenye taswira ya Msanii maarufu wa muziki wa taarab hapa nchini Bikidude ambayo ilimchukua muda wa wiki moja kutengeneza na alifanya hivyo kutokana na kuvutiwa na kazi za muziki za msanii huyo zilizoenea kote visiwani Zanzibar na kuamua kuchonga kinyago hicho. Kinyago hichi kilianza kupigwa mnada kwa Dola 550 mwenye kuvutiwa nacho ajitokeze.
Pichani Juu na Chini ni kazi za Ubunifu zilizofanywa na Vijana waliobadili mwelekeo wa maisha waliopo katika taasisi ya Sober House ya visiwani Zanzibar.
Kamishna kutoka Tume ya Kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya nchini Bw. Christopher Shekiondo (kushoto) akionekana kuvutiwa na moja ya sanamu ilyotengenezwa na vijana waliobadili mwelekeo na kuamua kuachana na dawa za kulevya na kuendeleza vipaji vyao ikiwemo sanaa ya uchongaji. Ahmed Awadhi.
Wadau waliohudhuria Uzinduzi wa Maonyesho ya Sanaa yaliyoandaliwa na Sober House Zanzibar yanayoendelea katika Ukumbi wa Alliance Francaise wa jijini Dar es Salaam na kiingilio ni bure.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ