• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, October 19, 2012

UNDP Yaipongeza Tanzania kwa Jitihada za Maendeleo

No comments:
 




Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw. Phillippe Poinsot akielezea jinsi shirika hilo linavyoshirikiana na serikali ya Tanzania katika kufanikisha miradi mbali mbali ya maendeleo katika kuhakikisha nchi inapiga hatua kwenye kukuza uchumi. Kulia ni Mwandishi wa Radio France International (RFI Kiswahili) Bw. Ali Bilali.
Na Mwandishi Wetu
UMOJA wa Mataifa umeanza kuadhimisha wiki mahsusi kwa ajili ya Umoja huo kwa kufanya shughuli mbalimbali ambapo nchini Tanzania taasisi za Umoja wa Mataifa, Serikali ya Tanzania na mashirika ya kiraia wanakutana kuzungumzia maswala mbalimbali yahusuyo maendeleo, utawala bora na njia za kupiga vita umaskini uliokithiri.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Maendeleo nchini Tanzania UNDP Philippe Poinsot, amesema Tanzania ni nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo inawajibika vizuri kwenye umoja huo.
Mbali na hayo Mkurugenzi huyo wa UNDP amesema kuwa Umoja wa Mataifa unachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza umasikini uliokithiri nchini Tanzania ambapo takriban dola za Marekani lakini nne milioni hutolewa katika kipindi cha miaka minne.
Wiki ya umoja wa mataifa imeanza kuadhishwa Oktoba 17 na itafikia kilele Oktoba 24 mwaka huu.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ