• Instagram
  • Twitter
  • Facebook
  • Google+
  • RSS Feed

Friday, October 19, 2012

Mbunge Kenya Afikishwa Mahakamani kwa Uchochezi

No comments:
 
 
Sheikh Mohamed Dor
Mbunge wa Vitimaalumu, Sheikh Mohamed Dor akiwa mahakamani
KIONGOZI mmoja Mkuu wa Kiisilamu nchini Kenya, ambaye pia ni mbunge mteule amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa kosa la uchochezi kwenye ghasia. Mbunge huyo, Sheikh Mohammad Dor anadaiwa kutamka kuwa anajitolea kufadhili vuguvugu la MRC linalotaka kujitenga kwa eneo la Pwani.
Hatua ya kushtakiwa kwa Sheikh Mohammed Dor inakuja siku tatu baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa kundi hilo Omar Mwamnuadzi. Sheikh Dor alikamatwa jana jioni baada ya kutangaza hadharani kuwa anaweza kufadhili vuguvugu hilo, ingawa aliachiliwa asubuhi ya leo kwa dhamana ya dola 23,000 baada ya kukana mashtaka ya uchochezi.
Kesi yake itaanza kusikilizwa tarehe kumi na tatu mwezi Novemba. Sheikh Dor ambaye amelaani msako unaoendelea wa polisi dhidi ya kundi hilo mjini Mombasa, alisema kuwa kundi hilo ambalo mahakama ilisema kuwa sio haramu, kwa mtu kuamua kulifadhili sio kosa. Dor ni mmoja wa wabunge kumi na wawili wa Kenya ambao hawakuchaguliwa ingawa waliteuliwa kuwakilisha maswala kadhaa bungeni.

No comments:

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...
 
© ALLSTARTZ.BLOGSPOT.COM 2012 - 2017 | ALL RIGHTS RESERVED | CODE + DESIGN BY: DMZ