
Wakili wa Lord Eyes jana ametoa ufanunuzi kuhusu tukio lililotokea la
msanii Lord Eyez kuhusishwa na tuhuma za wizi wa vifaa vya kwenye gari
na kusema kuwa dhumuni la kuwaita waandishi wa habari ni kutaka Jamii
itoe nafasi kwa vyombo vya sheria kutoa majibu juu ya tuhuma hizo na
baada ya hapo ndipo waanze kuongelea na kwamba kwa sasa hivi
kinachoendelea ni habari ambazo watu wanaozitoa hawana uhakika nazo.
Wakili huyo alisema kuwa Lord Eyez hana hatia hadi pale vyombo vya
sheria vitakaposema kuwa msanii huyo kweli anahusika na shutuma hizo za
wizi. Kwa upande wa Lord Eyez amesema, watu wanajua kuwa yeye ni
mwanamuziki kwa muda wote na hajihusishi na maswala ya wizi na ameomba
mashabiki wake wavumilie kipindi hichi ambacho anapigania haki na
mwishoni ukweli utajulikana....
Lord Eyez kwenye picha akizungumza na waandishi wa habari alianza kwa
kumshukuru Mungu kwa kumpa nguvu katika kipindi hiki kigumu ambacho kesi
ya kutuhumiwa kwake kuhusika na wizi wa vifaa vya gari
ikiendelea..MSIKILIZE...alichokisema ....
Wakili wa msanii Lord Eyez Bwana Peter Kibatala akielezea tukio zima
kuhusiana na Lord Eyez...MSIKILIZE akizungumzia tukio zima la msanii
huyo na dhumuni la kuitisha mkutano na waandishi wa habari
Msemaji wa kundi la WEUSI
Nikki wa Pili akizungumzia ni jinsi gani ishu ya Lord imewaathiri kundi hilo..MSIKILIZE hapo chini
No comments:
Post a Comment